Makapuku Forum

Makapuku Forum

KOCHA Mkuu wa kikosi cha timu ya wanawake cha Simba, Simba Queens, Sebastian Nkoma tayari ameshatinga kambi ya Simba iliyopo Lilongwe Malawi ili kuliongezea nguvu benchi la timu hiyo inayojiandaa kuivaana Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nkoma aliondoka asubuhi ya leo kwa usafiri wa shirika la ndege la Malawi na taarifa zilizopatikana ni kwamba tayari ameshatimba kambi ya timu hiyo iliyopo hoteli ya President Waltmont kuungana na Juma Mgunda na Seleman Matola waliotangulia mapema.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa Nkoma ameenda kuwa kama kocha wa viungo tofauti na taarifa ya awali iliyotoka klabuni humo ikieleza aliwahishwa huko ili kuokoa jahazi kutokana na sintofahamu ya kocha Mgunda mwenye kiwango cha elimu ya leseni A ya ukocha, japo ilidaiwa cheti chake kilikuwa hakijatoka.

Screenshot_20220909-164920_OGInsta%2B.jpg
 
Huyu ndie Camilla, kutoka mchepuko mpaka Malkia.
Maisha ya ujana ya Chalesi ambaye sasa ni Mfalme wa Uingereza hayakuwa tofauti na maisha ya wanaume wengine.

Licha ya kwamba alikuwa kwenye ndoa lakini alikuwa na mchepuko wake waliyekuwa wamegandana kama ruba. Pengine kabla ya ndoa zao za mwanzo Camilla na Charles wangeowana, hata hivyo wazazi wa mwanaume waliona kwamba Camilla hakuwa mke wa kuolewa na Mfalme mtarajiwa.

Camilla aliolewa na mume wake wa kwanza mwaka 1973. Katika ndoa yake alibahatika kupata watoto wawili. Inadaiwa kwamba wakati Camilla akiwa kwenye ndoa yake bado alikuwa na mahusiano ya nje na Prince Charles.

Migogoro iliibuka kwenye ndoa yao ukizingatia kwamba wote wawili walikuwa kwenye ndoa nyingine za Kikristu, Camilla akiwa na ndoa ya Kikatoliki na Charles ndoa ya Anglikana. Mwaka 1994, Camilla alitalakiana rasmi na mume wake wa kwanza, Andrew, baada ya kuishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 21.

Hata hivyo waliiambia mahakama kwamba walikuwa wametengena kwa muda mrefu. Camilla aliolewa na Charles mwaka 2005. Kwa sasa Camilla ni Malkia. Camilla ana umri wa miaka 75 na Mfalme Charles ana umri wa miaka 73.

Katika hii ndoa yao bado Camilla hajabahatika kupata watoto na Mfalme Charles. Hata hivyo Mfalme Charles ni baba wa ubatizo wa mtoto wa kwanza wa Camilla.View attachment 2351522
dah hawa kweli ilpgangwa na mungu wawe na hadhi hii
 
Wenyeji wa mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika Zalan FC ya Sudan Kusini wamewasili nchini muda huu kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Yanga inayotarajiwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Screenshot_20220909-193613_OGInsta%2B.jpg
 
Frank Kessie anashangilia kila goli lake kwa style ya kupiga saluti kwasababu Baba yake mzazi alikuwa Mchezaji kama yeye lakini baadae akajiunga na jeshi la Ivory Coast, alifariki wakati Frank ana umri wa miaka 11 tu, hivyo anapiga saluti kwa heshima ya Baba yake.
Screenshot_20220909-194209_OGInsta%2B.jpg
 
“Nitampa Binti yangu medali yangu ya UEFA kama nitashinda taji ili aweze kumpa anayempenda ambaye hajawahi kushinda taji hili” Pep Guardiola (2021)

Alisema haya baada ya taarifa za Bint yake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Dele Ali ambaye alikuwa Spurs wakati huo.

Screenshot_20220909-194318_OGInsta%2B.jpg
 
| Rais wa shirikisho la soka nchini Kenya Nick Mwenda amemwandikia barua Rais wa FIFA, Gianni Infantino kumwarifu kuwa tayari Mkurugenzi wa mashtaka wa Kenya ameondoa vikwazo dhidi yake na wapo tayari kuanza mazungumzo ya kurejea kwenye soka la kimataifa.
Screenshot_20220909-194452_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Kocha Juma Mgunda atakuwepo kwenye bench la Simba kama kawaida na baada ya kufanya utafiti wangu ni kuwa ana leseni A ya CAF hivyo amekidhi vigezo, taarifa za kuwa hana vyeti sio za kweli.

Simba pia wamemsafirisha Kocha wa Simba Queens ambaye atawasili leo saa tatu asubuhi Lilongwe kuungana na timu kwakuwa timu haina Kocha wa Viungo na Makipa hivyo wameongeza jopo ili kutia nguvu katika kipindi hiki cha mpito.

Nkoma haendi kama mbadala wa Mgunda bali kuongeza nguvu kwenye timu kwakuwa bench la Simba limepungua ndio maana mechi ya KMC, Mussa Mgosi alikaa kwenye bench pia.
Screenshot_20220909-194624_OGInsta%2B.jpg
 
Kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza inayosikiliza Kesi namba 11 ya usafirishaji haramu wa Binadamu inayomkabili Diana Bundala maarufu Zumaridi, Leo Sep 09, imeshindwa kuendelea kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo kwa zaidi miezi nane.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Monica Ndiyekobora anayesikiliza kesi hiyo ameiahirisha na itatajwa tena Sept 23, 2022.
Screenshot_20220909-195215_OGInsta%2B.jpg
 
Wizara ya Kilimo imetoa taarifa kwa Umma na Wafanyabiashara wote wa mazao ya chakula kuwa, haijasitisha utoaji wa vibali wa kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Wizara ya kilimo kwa kufuata taratibu zote za kisheria imeendelea kutoa vibali vya kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi kupitia mfumo wa utoaji vibali wa kielektroniki”

“Katika kipindi cha kuanzia tarehe 27 Agosti hadi 7 Septemba, 2022, Wizara imetoa vibali vya mahindi, maharage,unga, na mchele kwenda nje ya nchi vyenye jumla ya Tani 37,450”

“Wizara inawakumbusha Wafanyabiashara wa mazao ya chakula kuwa, ili kuepuka usumbufu usio wa lazima, wanatakiwa kuwa na kibali cha kusafirisha mazao nje ya nchi(Export Permit) au kuingiza ndani ya nchi(Import Permit) kabla ya kufikisha mzigo Mpakani, Bandarini, au Kiwanja cha Ndege”
Screenshot_20220909-195443_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Mamlaka za usalama wa nchi hiyo zimemkamata Kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu (IS) anayefahamika kwa jina la Abu Zeyd.

Rais Erdogan ametoa taarifa za kukamatwa kwa Mtu huyo wakati akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kuyatembelea Mataifa ya Balkani.

Erdogan amesema jina halisi la Abu Zeyd ni Bashar Khattab al-Sumaidai na Umoja wa Mataifa unamtaja kuwa miongoni mwa Viongozi wakubwa kabisa wa kundi la itikadi kali la IS.

Erdogan amemwelezea Sumaidai kama Kiongozi wa juu wa kundi la IS nchini Syria, eneo ambako kundi hilo linadaiwa kufanya hujuma kubwa tangu lilipozuka na kupata nguvu mwaka 2014.
Screenshot_20220909-195759_OGInsta%2B.jpg
 
Hulda Daudi (25), ni Msichana aliyefeli kidato cha nne na kuja Dar es salaam kutafuta maisha akitokea Morogoro baada ya Baba yake kufariki na kumuachia mzigo wa kumtunza Mama yake pamoja na Wadogo zake.

Akiwa Dar es salaam aliajiriwa saluni kisha baadaye akapata mtaji wa kufungua saluni yake karibu na alipopanga, Tabata kwa Swai, mzigo wa majukumu ya Kifamilia ukamfanya akope fedha kwa zaidi ya Watu watatu wanaokopesha kwa riba ili akuze mtaji lakini mambo yameenda tofauti na amejikuta na madeni mengi, akaamua kujiunga na VICOBA viwili na kote anadaiwa zaidi ya Tsh. Milioni 3.

Hulda ameiambia @ayotv_ kwamba wanaomdai wanamsumbua hadi anapoishi, wapo waliomfungulia kesi Polisi, wapo wanaompa vitisho, hawezi tena kufungua ofisi maana kila akifungua wanaomdai hufika na kumfanyia vurugu, amekuwa ni Mtu wa kulia na kuwaza, anakosa hata hela ya kula, ameuza vitu vyake vingi huku akifikiria hata kujiua “Kuna wanaonidai wanasema wataniroga, naogopa, nisaidieni kwa pesa au hata ushauri, msisubiri nijiue muanze kunililia”

Namba zake ni 0675552385
0629630099 ( Hulda Daudi Ramsey)…. simulizi yake nzima ipo Youtube ya millardayo
Screenshot_20220909-195923_OGInsta%2B.jpg
 
Faines Kunga (6), Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Wanging’ombe Mkoani Njombe amefariki mara baada ya kunasa kwenye tope wakati akiogelea kwenye maji ya mashamba ya bondeni alipokuwa akitoka Shuleni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo “Mtoto huyu ambaye ni wa kike ametoka Shuleni na wenzake akaingia kwenye maji kwa ajili ya kuogelea na matokeo yake alikwama kwenye matope chini”

Kamanda Issah ametoa wito kwa jamii kuwa makini na Watoto kwa kipindi hiki ambacho Shule zimefunguliwa huku pia akiagiza Wamiliki wa bustani mabondeni kuongeza umakini kwa Watoto ili wasiweze kucheza katika maeneo yao.
Screenshot_20220909-200150_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom