Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma, Winfrida Michael (24), aliyekuwa anasoma Diploma ya Medical Laboratory amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa kisu na Mpenzi wake, Julius Gervas (26), RPC Dodoma Martin Otieno amethibitisha .

Winfrida alifariki wakati anapelekwa Hospitali baada ya kuwa amevuja damu nyingi na Julius baada ya kufanya tukio hilo alijaribu kujichoma kisu tumboni lakini Watu walimuwahi na kumchukua kisha kumpeleka Hospitalini ambako anaendelea na matibabu chini ya ulinzi.

Inaelezwa kuwa Winfrida alikuwa amepanga nje ya Chuo na alikuwa na mahusiano na Kijana huyo kwa muda fulani lakini walikuwa wameachana na Kijana alikuwa anamsumbua Msichama hivyo alimuahidi kuwa akimaliza mtihani atamjulisha.

Juzi Msichana alikuwa amemaliza mtihani wake wa mwisho na kwa mujibu wa Mama mwenye nyumba walikutana wakaongea sana pale ndani na ilipofika saa nne na nusu walitoka nje akawa anamsindikiza ndio lilipotokea tukio la kuchomwa kisu na akawa anaomba msaada na walimchukua na kumpeleka Hospitali lakini akawa amefariki, mwili wa Marehemu umeagwa na kusafirishwa kwenda Ukerewe kwa mazishi.
Screenshot_20220909-200434_OGInsta%2B.jpg
 
Hulda Daudi (25), ni Msichana aliyefeli kidato cha nne na kuja Dar es salaam kutafuta maisha akitokea Morogoro baada ya Baba yake kufariki na kumuachia mzigo wa kumtunza Mama yake pamoja na Wadogo zake.

Akiwa Dar es salaam aliajiriwa saluni kisha baadaye akapata mtaji wa kufungua saluni yake karibu na alipopanga, Tabata kwa Swai, mzigo wa majukumu ya Kifamilia ukamfanya akope fedha kwa zaidi ya Watu watatu wanaokopesha kwa riba ili akuze mtaji lakini mambo yameenda tofauti na amejikuta na madeni mengi, akaamua kujiunga na VICOBA viwili na kote anadaiwa zaidi ya Tsh. Milioni 3.

Hulda ameiambia @ayotv_ kwamba wanaomdai wanamsumbua hadi anapoishi, wapo waliomfungulia kesi Polisi, wapo wanaompa vitisho, hawezi tena kufungua ofisi maana kila akifungua wanaomdai hufika na kumfanyia vurugu, amekuwa ni Mtu wa kulia na kuwaza, anakosa hata hela ya kula, ameuza vitu vyake vingi huku akifikiria hata kujiua “Kuna wanaonidai wanasema wataniroga, naogopa, nisaidieni kwa pesa au hata ushauri, msisubiri nijiue muanze kunililia”

Namba zake ni 0675552385
0629630099 ( Hulda Daudi Ramsey)…. simulizi yake nzima ipo Youtube ya millardayoView attachment 2351704
Hamna mtu wa kujiua humu 😂🤣
 
Kampuni ya MeTL Group ya Tanzania na Panasonic Life Solutions ya India wametangaza muungano wa kuuza bidhaa za umeme nchini Tanzania muungano ambao unakusudia kunasa soko jipya ambalo linaangalia ubora wa bidhaa za umeme.

Mkurugenzi wa Masoko wa METL, Bi. Fatema Dewji akiikaribisha Panasonic India alisema Kampuni hizi mbili zinaamini katika kutengeneza ulimwengu bora kwa Wateja “Panasonic inasimamia maisha bora, Ulimwengu bora’ na sikuweza kuona kauli mbiu bora zaidi inayofanana na inayokamilisha "kugusa maisha ya Watu".

Akizungumza katika hafla hii, Vishal Nangalia San, Mkuu wa Biashara ya Mauzo ya Bidhaa wa Panasonic Life Solutions India alisema “Tunayo furaha kushirikiana na METL Group inayoongoza jumuiya ya biashara ya Afrika Mashariki na tunatarajia mafanikio ya kusisimua.

Aidha Mkurugenzi wa Mauzo wa MeTL, Hussein Dewji amesema ushirikiano kati ya METL na Panasonic ni wa kihistoria hapa nchini unaolenga kumsaidia Mtanzania wa hali ya kawaida kupata bidhaa za Panasonic kwa urahisi, uharaka na kwa bei nafuu kokote nchini.
Screenshot_20220909-200604_OGInsta%2B.jpg
 
Huyu ndie Princess Diana, sasa hivi ndie angekuwa Malkia.

Sio pesa wala ukuu unaoweza kufanya ndoa yako idumu, bali heshima na upendo. Kama ungekuwa ukuu au pesa basi ndoa ya Diana na Charles isingekufa. Princess Diana alikutana kwa mara ya kwanza na Prince Charles akiwa binti mdogo kabisa mwenye umri wa miaka 16, wakati huo Prince Charles alikuwa anatoka na dada yake Diana. Diana alimpenda Charles, wakafanya mafekechee wakazama penzini japo kwa siri. Baadae wakahalalisha mahusiano yao na kufunga ndoa mwka 1981, Diana akiwa na miaka 20.

Sio kwamba Diana alitoka katika familia isiyokuwa na heshima, hapana, familia yake ni mojawapo ya familia zenye hadhi ya juu nchini Uingereza. Baada ya ndoa Diana alikuwa ni mwanamke wa Tatu mwenye heshima nchini Uingereza, baada ya Malkia na Mama yake Malkia.

Licha ya ukuu aliokuwa nao lakini Princess Diana hakuwa na furaha kwenye ndoa yake. Mume wake kuwa na mahusiano ya nje ilimtesa sana Diana. Mimba ya mtoto wake wa kwanza ikiwa na wiki 12, Diana alijirushwa kutoka kwenye ngazi na kuanguka, hata hivyo mimba haikurabika. Diana alisema alifanya hivyo kwa sababu alikuwa mpweke sana. Baada ya kujifungua mwanae wa kwanza Diana aliugua ugonjwa wa Sonona.

Baada ya miaka 5 ya ndoa kulikuwa na migogoro mikubwa sana ambayo haswa ilichangiwa na tofauti ya umri. Diana alikuwa na mchepuko wake wakati huo mumewe pia mahusiano yake na Camilla yalikuwa yamenoga. Migogoro na utofauti iliendeleq kukuwa na kupelekea ndoa yao kuvunjika miaka 15 baadae.

Akizungumza na mwandishi wa BBC, Diana alisema waliamua kutengena kwa sababu mahusiano yao yalikuwa kama ofisi ya umma, siku hizi mnasema Azam Burudani kwa Wote. Pia Diana alisema alikuwa ana mashaka sana kama Prince Charles alikuwa anafaa kuwa Mfalme wa Uingereza.

Baada ya kutengana Princess Diana alinasa kwenye penzi zito la mtoto wa Kiarabu, penzi lao halikudumu sana. Princess Diana alifariki dunia kutokana na majeraha aliyopata kutokana na ajali ya gari. Alifariki mwaka 1997, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutalakiana na Charles. Princess Diana alifariki akiwa na umri wa miaka 36, katika ndoa yao walibahatika kupata watoto wawili ambao ni Prince William na Prince Harry.
Screenshot_20220909-201313_OGInsta%2B.jpg
 
Huyu ndie Camilla, kutoka mchepuko mpaka Malkia.
Maisha ya ujana ya Chalesi ambaye sasa ni Mfalme wa Uingereza hayakuwa tofauti na maisha ya wanaume wengine.

Licha ya kwamba alikuwa kwenye ndoa lakini alikuwa na mchepuko wake waliyekuwa wamegandana kama ruba. Pengine kabla ya ndoa zao za mwanzo Camilla na Charles wangeowana, hata hivyo wazazi wa mwanaume waliona kwamba Camilla hakuwa mke wa kuolewa na Mfalme mtarajiwa.

Camilla aliolewa na mume wake wa kwanza mwaka 1973. Katika ndoa yake alibahatika kupata watoto wawili. Inadaiwa kwamba wakati Camilla akiwa kwenye ndoa yake bado alikuwa na mahusiano ya nje na Prince Charles.

Migogoro iliibuka kwenye ndoa yao ukizingatia kwamba wote wawili walikuwa kwenye ndoa nyingine za Kikristu, Camilla akiwa na ndoa ya Kikatoliki na Charles ndoa ya Anglikana. Mwaka 1994, Camilla alitalakiana rasmi na mume wake wa kwanza, Andrew, baada ya kuishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 21.

Hata hivyo waliiambia mahakama kwamba walikuwa wametengena kwa muda mrefu. Camilla aliolewa na Charles mwaka 2005. Kwa sasa Camilla ni Malkia. Camilla ana umri wa miaka 75 na Mfalme Charles ana umri wa miaka 73.

Katika hii ndoa yao bado Camilla hajabahatika kupata watoto na Mfalme Charles. Hata hivyo Mfalme Charles ni baba wa ubatizo wa mtoto wa kwanza wa Camilla.



View attachment 2351522
Sasa akifa huyo chalz nani atakuwa mfalme wakati hajazaa!?
 
Screenshot_20220909-201955_OGInsta%2B.jpg


FOOTBALL ECONOMY || Mishahara
.
Kwa mujibu wa kijana mwenzetu @kenedymosestz huo ndio mpangilio wa mshahara wa Mchezaji wa Yanga Fiston Mayele baada ya kusaini mkataba mpya.
.
Nami nimeingia mzigoni ili kujua malipo ya wachezaji wanaocheza ligi kuu na ligi ya Championship. Nitawajulisha nani analipwa sana na nani analipwa kidogo kutoka vilabu vyote.
.
Nitawajulisha mzawa gani anakula pesa ya kutosha na nani anakula Pesa kiduchu na kisha kuwaletea bajeti ya mishahara ya klabu kwa ujumla na kadirio la matumizi kwa msimu.
.
Che Guevara
.
NB:
Kuna timu zitakwambia mshahara ni siri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom