Huyu ndie Camilla, kutoka mchepuko mpaka Malkia.
Maisha ya ujana ya Chalesi ambaye sasa ni Mfalme wa Uingereza hayakuwa tofauti na maisha ya wanaume wengine.
Licha ya kwamba alikuwa kwenye ndoa lakini alikuwa na mchepuko wake waliyekuwa wamegandana kama ruba. Pengine kabla ya ndoa zao za mwanzo Camilla na Charles wangeowana, hata hivyo wazazi wa mwanaume waliona kwamba Camilla hakuwa mke wa kuolewa na Mfalme mtarajiwa.
Camilla aliolewa na mume wake wa kwanza mwaka 1973. Katika ndoa yake alibahatika kupata watoto wawili. Inadaiwa kwamba wakati Camilla akiwa kwenye ndoa yake bado alikuwa na mahusiano ya nje na Prince Charles.
Migogoro iliibuka kwenye ndoa yao ukizingatia kwamba wote wawili walikuwa kwenye ndoa nyingine za Kikristu, Camilla akiwa na ndoa ya Kikatoliki na Charles ndoa ya Anglikana. Mwaka 1994, Camilla alitalakiana rasmi na mume wake wa kwanza, Andrew, baada ya kuishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 21.
Hata hivyo waliiambia mahakama kwamba walikuwa wametengena kwa muda mrefu. Camilla aliolewa na Charles mwaka 2005. Kwa sasa Camilla ni Malkia. Camilla ana umri wa miaka 75 na Mfalme Charles ana umri wa miaka 73.
Katika hii ndoa yao bado Camilla hajabahatika kupata watoto na Mfalme Charles. Hata hivyo Mfalme Charles ni baba wa ubatizo wa mtoto wa kwanza wa Camilla.