Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Simba SC, MO Dewji @moodewji leo amezindua rasmi lebo yake ya kuandaa mapambano ya ngumi MO Boxing.

MO Dewji amezindua lebo hiyo na kutangaza rasmi kuandaa pambano la kimataifa Septemba 30 2022 Next Door Arena kati ya Mtanzania Ibra Classic dhidi ya Mmexico Gustavo Pina Melgar.

Mo amesema “Tumefurahi kuzindua lebo ya Mo Boxing Promosheni itakayosaidia ndondi za Afrika kwa ujumla, dhumuni kubwa ni kukuza ndondi za Afrika kwenye jukwaa la kimataifa, kuukuza mchezo wa ndondi na kuifanya Tanzania kuwa kitovu kwa Afrika”
Screenshot_20220907-180859_OGInsta%2B.jpg
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame Mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kigali nchini Rwanda.
Screenshot_20220907-181208_OGInsta%2B.jpg
 
Mtu mmoja ambaye ni Mwanajeshi, aitwae William Chacha Giriango (40) amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake aliokuwa ameutundika kwenye nondo ya dirisha katika chumba cha kulala Wageni kwenye Logde moja iliyopo Mtaa wa Hazina Jijini Dodoma.

Kamanda wa Polisi Dodoma, Martin Otieno amethibitisha tukio hilo ambalo lilitokea September 6, 2022 ambapo baada ya kupekuliwa marehemu alikutwa na meseji mbalimbali, ujumbe wa kwanza alimuandikia Mama yake ulisomeka “Mama yangu nisamehe sana nakuomba”

Kamanda Otieno amesema ujumbe wa pili alimuandikia Mke wake ulisomeka “kwako Mama Derick nisamehe sana kwa maamuzi haya, maisha kwangu hayana maana tena, nisamehe sana nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze Watoto wetu”
Screenshot_20220907-181407_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Mtu mmoja aitwaye, Peter Mwakipesile kwa tuhuma za kumuua Mkewe Aisha Ramadhani Mkazi wa Chidachi kwa kipigo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha tukio hilo ambapo amesema chanzo cha kifo ni baada ya ugomvi ulitokea pale Aisha alipochelewa kurudi nyumbani na aliporudi Mumewe alimchukua na kumfungia chumbani na kuanza kumpiga kwa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake ambapo alifariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitali.
Screenshot_20220907-181550_OGInsta%2B.jpg
 
Club ya Chelsea imetangaza kumfuta kazi Kocha wake Mkuu Thomas Tuchel ikiwa ni siku moja imepita tangu wapoteze mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Dynamo Zagreb kwa kufungwa 1-0.

Tuchel anafukuzwa ndani ya siku 100 tu tangu Chelsea ipate Mmiliki mpya Todd Boehly.

Maamuzi hayo yanafikiwa baada ya Tuchel kuiongoza Chelsea katika michezo 100 akishinda 62 toka alipojiunga nao mwaka 2021.
Screenshot_20220907-181813_OGInsta%2B.jpg
 
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Twaha Kiduku anatarajia kupanda ulingoni September 24 mwaka huu Mkoani Mtwara kupigana na Bondia kutoka nchini Misri Abdo Khaled.

Kiduku ameiambia @ayotv_ kuwa amejipanga vizuri na ana matumaini ya kuibuka na ushindi katika Pambano hilo la kuwania mkanda wa UBO pambano ambalo litachezwa kwa raundi kumi.

Kiduku amewaomba Wadau na Mashabiki wake kuendelea kumpa support kwa kipindi chote cha maandalizi ili aweze kufanikiwa katika pambanao hilo .

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Morogoro Abdulazizi Abood ameahidi kumshika mkono kwa kipindi hiki cha maandalizi hadi siku atakapopanda ulingoni ili aweze kuliwakalisha Taifs vizuri.
Screenshot_20220907-181904_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Wasichana inayojengwa katika eneo la Kanoni lililopo Wilaya ya Karagwe ikiwa ni wiki mbili tu tangu atoke kwenye mradi huo unaogharimu Tsh. Bilioni 4 za Kitanzania.

Baada ya kufika kwenye mradi huo hakuridhishwa na kasi ya Mkandarasi hali iliyopelekea kuagiza akamatwe na kuweka ndani huku utaratibu mwingine ukiendelea ili kuhakikisha mradi huo unaenda kwa kasi ili malengo yaweze kutimia kwa muda uliopangwa.
Screenshot_20220907-182110_OGInsta%2B.jpg
 
Mwili wa Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, George Chiteto umeagwa jana Chuo cha St. John jijini Dodoma, Askofu Chiteto alifariki September 03, 2022 muda mfupi baada ya kutoa mahubiri katika Ibada ya mazishi ya Mke wa Askofu mwenzake iliyofanyika, Muheza Tanga.

@ayotv_ imepata nafasi ya kuzungumza na kijana Zacharia Mbogoli ambaye Askofu huyo, alikuwa akifanya naye shughuli mbalimbali kwa ukaribu kwa zaidi ya miaka nane ambapo amesimulia jinsi ambavyo Askofu Chiteto alivyokuwa akijitabiria mara kwa mara kuwa kauli yake ya mwisho ataitoa akihubiri Madhabahuni “Kwa zaidi ya miaka mitano alikuwa akiniambia hatamani kufa kifo cha kuwatesa Watu yaani kwa kuumwa na kuwasumbua Madaktari badala yake alitamani afe akiwa anahubiri”

Zacharia ameongeza kuwa Askofu alikuwa akisisitiza kifo cha namna hiyo alikuwa anakipenda sana na hata alipolazwa kipindi cha nyuma alimwambia hawezi kufia Hospitalini bali lazima afie Madhabahuni.

Mara ya mwisho Askofu Chiteto alikuwa akitoa mahubiri kanisani mbele ya umati wa waombolezaji na alipomaliza alikaa kwenye kiti kama kawaida ya wahubiri na baada ya muda mchache waliona anaishiwa nguvu na kuanguka na alipofikishwa Hospitalini ilibainika amefariki.
Screenshot_20220907-182212_OGInsta%2B.jpg
 
Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati 25 - 28 amekutwa ameuawa katika msitu wa miti uliopo kwenye eneo la Muungano katika Kijiji cha Kifanya Halmashauri ya Mji wa Njombe akiwa na jeraha kubwa eneo la shingoni na michubuko sehemu za usoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema mwili huo umepatikana September 03,2022 mara baada ya Watoto kutoa taarifa walipoona mwili huo lakini hata hivyo Mwanamke huyo hajatambulika kuwa ni mkazi wa wapi na tayari Polisi wanamshikilia Mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.

“Mtu huyu ameuawa na baada ya kuwatangazia Wananchi hajatambulika, amepoteza maisha akiwa amevaa dela la rangi ya bluu lenye michirizi ya njano akiwa amesuka rasta”

Aidha Kamanda Issah ametoa wito kwa Wananchi wa maeneo ya karibu kama kuna Mtu amepotea katika maeneo yao akiwa amevaa mavazi ya aina hiyo aweze kufika katika Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena sehemu ulipohifadhiwa mwili huo kwa ajili ya kuutambua.
Screenshot_20220907-182313_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini, bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 7 Septemba 2022.

“Bei za Mafuta katika soko la dunia za Julai 2022 zimepungua ikilinganishwa na bei hizo kwa Juni 2022, hivyo bei za mafuta katika soko la ndani zimepungua vilevile kwa kati ya shilingi 271/lita na shilingi 362/lita kwa petroli na kwa shilingi 430/lita kwa mafuta ya taa ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022”

“Kwa mafuta ya dizeli, ukiiacha bei ya Tanga ambayo inashuka kwa shilingi 13/lita, bei za Septemba 2022 zimeongezeka kwa shilingi 37/lita na shilingi 86/lita kwa Dar es Salaam na Mtwara, sawia, ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022”

“Ili kuendelea kupunguza madhara ya ongezeko la bei za dizeli hapa nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea dizeli na pia ili kupunguza tofauti kati ya bei za petroli na dizeli, Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 65 ili kupunguza bei za mafuta za mwezi Septemba 2022”

Kwa kutoa ruzuku hiyo, Serikali imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba 2022 kama inavyoonekana
Screenshot_20220907-182400_OGInsta%2B.jpg
 
Watu 15 wamefariki dunia baada ya kutokea maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa huko Kasese, magharibi mwa Uganda.

Baadhi ya nyumba pia zilisombwa na maji ya mafuriko ambayo yalipitia eneo lililo chini ya milima ya Rwenzori.

Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Uganda amesema watu sita walijeruhiwa katika maporomoko hayo kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Taarifa zinaeleza kuwa watu wengine ambao idadi yao haijulikani hawajulikani walipo.
Screenshot_20220907-182508_OGInsta%2B.jpg
 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeelezea namna unavyokabiliana na wimbi la ubadhirifu unaofanywa na watoa wahuduma, wanachama na baadhi ya watumishi wake.

Akizungumza jana katika mahojiano maalumu yaliyofanyika makao makuu ya Mwananchi Communications Limited (MCL), iliyopo Tabata relini jijini Dar es Salam, Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NHIF, Hipoliti Lello alisema changamoto ya ubadhirifu wa fedha za mfuko zilizoibuliwa siku za hivi karibuni, ni za kweli lakini tayari wanaendelea kuzifanyia kazi.
Screenshot_20220907-182617_OGInsta%2B.jpg
 
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs atashtakiwa upya kwa makosa ya kutumia nguvu nyumbani, Jaji wa Uingereza ameamua leo Jumatano baada ya mahakama kushindwa kufikia uamuzi mwezi uliopita.

Jaji Hilary Manley wa mahakama ya Manchester amepanga tarehe ya kusikiliza upya kesi hiyo kuwa Julai 31 mwakani, baada ya wanasheria kushindwa kufikia uamuzi katika kesi hiyo iliyosikilizwa kwa wiki nne.

Giggs, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Wales mwenye miaka 48, alikana kuwa na tabia ya udhibiti na kutumia nguvu dhidi ya mpenzi wake wa zamani, Kate Greville pamoja na kumtukana yeye na mdogo wake wa kike.
Screenshot_20220907-182805_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Nishati wa Tanzania, January Makamba amesema Serikali itaanzisha ofisi maalumu itakayosimamia utekelezaji wa mradi wa uchakataji na usindikaji gesi asilia (LNG), wenye thamani ya Sh70 trilioni.

Makamba ameeleza hayo leo Jumatano Septemba 7, 2022 alipotembelea ofisi za kampuni ya Shell, nchini Uholanzi na kuzungumza na viongozi wakuu wa kampuni hiyo kuhusu utekelezaji wa LNG nchini.

Waziri huyo yupo Uholanzi kwa ziara ya kikazi.

Katika mazungumzo hayo, Makamba alisema mchakato wa ofisi hiyo utakamilika Novemba 2022 ili kuratibu, kuharakisha na kurahisisha hatua za utekelezaji wa mradi huo.
Screenshot_20220907-182922_OGInsta%2B.jpg
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho.

Kikao hicho kimefanyikia leo Jumatano, Septemba 7, 2022 katika Ofisi ndogo za chama, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Screenshot_20220907-183037_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom