Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Watu watano wamefariki dunia na wengine 54 wamejeruhiwa baada ya basi kugongana na lori katika eneo la Ibadakuli katika eneo la Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Leonard Nyandahu amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Septemba 3, 2022 ikihusisha basi kampuni ya Super Najimunisa likitokea Dar es salaam kuelekea jijini Mwanza na lori likitokea Mwanza kwenda Dar es salaam likiwa na mzigo wa dagaa.
Nyandahu amesema chanzo cha ajali hii ni uzembe wa dereva wa basi kwa kutozingatia vibao vya usalama barabarani na kuendesha mwendokasi.