Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Mtoto Jovin Simon (10) Mkazi wa Mtaa wa Elimu Wilaya ya Geita amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na teke tumboni na Haruna Amini (16) Mkazi wa Mtaa wa Elimu.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Ally Kitumbu amesema Jovin alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Geita huku akisema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi kati yao wawili .
"Huyu Mwanafunzi alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu na kiini cha tukio ni ugomvi mwili umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi wa Daktari”
Aidha Kaimu Kamanda amewaomba Wazazi kuhakikisha wanawakanya Watoto wao kucheza michezo isiyokuwa na staha wawapo majumbani na kusema mwili wa Mtoto huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Geita.

unaambiwa utajilambaaaa...