Mwanamke mmoja wa Melbourne nchini Australia aitwae Thevamanogari Manivel ametakiwa kulipa kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya milioni sita (Tsh. zaidi ya bilioni 16) kwa kampuni moja iitwayo CRYPTO ya nchini Singapore baada ya kampuni hiyo kukosea muamala na kumuwekea fedha hizo kwenye account yake ya benki.
Baada ya kuziona pesa hizo kwenye account yake Manivel alivumilia kwa muda wa miezi saba bila kuzitumia ambapo baada ya kuona kipindi hicho kimepita bila Mtu yoyote kujitokeza kuzidai alimua kuzitoa na kuzinunulia nyumba ya ndoto zake huku nyingine akizigawanya kwenda kwenye akaunti za ndugu zake wapatao sita.
Manivel alitumia dola laki 9 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh. bilioni 2 kununulia nyumba hiyo ya ndoto zake ikiwa na vyumba vitano ambapo baada ya hiyo miezi saba Kampuni hiyo iligundua makosa hayo na kuanza taratibu za kisheria mwezi February na kumfungulia Manivel mashitaka ya kutaka alipe pesa zote pamoja na riba.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Victoria nchini Australia James Elliott, licha ya kuamuru kulipwa kwa fedha hizo alishangazwa na Walalamikaji kwa kutotambua makosa hayo ya malipo kwa muda wa miezi saba ambapo hata hivyo aliagiza Manivel kulipa fedha zote ikijumuisha asilimia 10 ya riba na ada za kisheria.
Akili ya auntie yangu
Espy Atoto 
View attachment 2341243