Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mchezaji wa Simba SC John Bocco ameongezwa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” kuelekea mchezo wa marudiano kufuzu CHAN dhidi ya Uganda utakaochezwa Septemba 3, 2022 Kampala, Uganda
Screenshot_20220901-094554_OGInsta%2B.jpg
 
Mechi ya mwisho LA LIGA alifunga mbele ya FC Barcelona na mechi yake ya kwanza EPL anafunga mbele ya Liverpool, anaitwa Aleksander Isak.
Screenshot_20220901-094715_OGInsta%2B.jpg
 
Kwenye mechi tano tu za EPL, tayari Erling Halaand ana idadi sawa za hatrick na;

•Eden Hazard
•Sadio Mane
•Heung Min Son
Screenshot_20220901-095127_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati Liverpool wanakamilisha uhamisho wa Fabio Carvalho kutoka Fulham wengi waliamini Kijana huyo atahitaji muda kucheza Anfield ila stori imekuwa tofauti kwa Mreno ameonesha ukomavu na leo amefunga bao la muhimu sana kwa Kops.
Screenshot_20220901-095250_OGInsta%2B.jpg
 
Shaffih Dauda

Mfano tu winga ya kushoto akae Bernard Morrison kisha winga ya kulia akae Tuisila Kisinda, nyuma yao ni Feisal Salum na Khalid Aucho kisha mbele yao ni Fiston Mayele na Stephan Aziz Funguo.

Sijamtaja Yannick wala Dickson Job, sijamtaja Djuma Shabaan wala Kibwana Shomari, sahau kuhusu Djigui Diarra, sahau kuhusu waliyopo bench na ambao watakuwepo jukwaani.

Ifungwe Kaunta ifungwe Bar, si hatulali Jama
Screenshot_20220901-095340_OGInsta%2B.jpg
 
Nyota Erling Halaand kupitia Insta story yake akiwa na mpira ameweka caption inayosomeka;.

“Hawakutuamini” kisha kuna maandishi kwa juu yanasomeka “Mungu ametuamini”

Kazi ipo na mwamba huyu hapa
Screenshot_20220901-095446_OGInsta%2B.jpg
 
Kupitia Instastory yake Kinda Wesley Fofana amepost picha akiwa na jezi ya Chelsea akiwa bado kijana mdogo sana, inasemekana ni Shabiki wa muda mrefu wa Chelsea.
Screenshot_20220901-095617_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi kuhusu huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo amesema “Pamoja na uwepo wa ongezeko kubwa la magonjwa yasiyo ya kuambukiza, sababu nyingine inayohatarisha uhai na uendelevu wa mfuko huu ni vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya Watoa huduma na Wanachama wa mfuko, vitendo hivi vinalenga kujipatia manufaa kinyume na utaratibu”

“Mathalani katika mwaka wa fedha 2021/22 jumla ya Wataalamu 65 wamefikishwa katika Mabaraza yao kutokana na kukiuka taratibu na miongozo ya taaluma za afya, nimeieleza NHIF kuimarisha mikakati yake ya kupambana na vitendo vya udanganyifu pamoja na kuimarisha matumizi ya Mifumo ya TEHAMA”

“Vilevile, changamoto nyingine iliyopo ni uwepo wa kundi kubwa la Wananchi wanaojiunga na NHIF kwa hiari ambao, takribani asilimia 99 ni Wagonkwa,hatua hii imetokana na kutokuwepo kwa Sheria ya ulazima kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya”

“Kama mnavyokumbuka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ulianzishwa mwaka 2001 ukiwa umelenga kuwahudumia watumishi wa umma pekee lakini kutokana na uhitaji wa huduma hizi kwa wananchi wote, marekebisho ya Sheria yamekuwa yakifanyika mara kwa mara na kuruhusu makundi mbalimbali kuhudumiwa na mfuko”
Screenshot_20220901-182302_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu @ummymwalimu leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi kuhusu huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo amesema “Niwatoe wasiwasi Wadau wa NHIF wakiwemo Wanachama, Watoa huduma pamoja na Watanzania wote kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua stahiki kuhakikisha kuwa mfuko huu unakuwa imara, endelevu na stahimilivu kwani kwa sasa, ni moja kati ya mfuko unaotumika katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa nchini”

“Mfuko huu ndio umekuwa tegemeo la watanzania wengi hususani wa kipato cha chini na mfuko huu pia ndio umekuwa tegemeo la vituo vya kutoa huduma za afya nchini, pamoja na kuwa na wanachama asilimia nane tu ya Watanzania wote, vituo vingi vya kutolea huduma vinategemea mapato kutoka katika Mfuko kwa zaidi ya asilimia 70”

“Katika kuhakikisha kuwa maamuzi yote yahusuyo Mfuko huu yanazingatia taratibu na miongozo ya kuendesha chombo hiki, tumefanya tathmini ya uhai na uendelevu wa mfuko kwa mujibu wa sheria na, hivyo tunatambua ni yapi yanapaswa kufanyika ili kuhakikisha mfuko wetu unakuwa endelevu na imara zaidi, matokeo ya awali yanaonesha uendelevu wa mfuko huu unategemea sana ongezeko la wanachama watakaoandikishwa katika Mfuko huu”

“Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ambayo itaweka mazingira kwa kila Mtanzania kuwa na Bima ya Afya ili kuwezesha dhana ya kuchangiana gharama za matibabu na hivyo kuwaepusha Wananchi katika hatari ya janga la umaskini pindi wakiwa Wagonjwa au wanapougua”
Screenshot_20220901-182406_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi ishu ambayo imekua gumzo nchini kuhusu masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki ambapo amesema “Mimi nasema tu atakayetaka kutukana atukane tu, hata kama nitakosa Rafiki hata mmoja sawa tu lakini lazima niseme ukweli hata Mtu ana ng’ombe Elfu 12 mnataka Bwawa lake lijengwe kwa kodi ya Nesi au Mwalimu”

“Kuna Watu walitakiwa walipe kodi hawalipi halafu tunaenda kwa mazoea, Rais Samia anataka kuona zile kodi za chini Watu walipe kiuhalisia, binafsi kama Binadamu na Mimi nachukia kutoza toza Watu, nachukia kumtoza Mtu fedha yake kabisakabisa, niwaombe Mtu ambaye ana maoni tuendelee kuboresha, hatuna sababu ya kugombana Nchi hii ni yetu, fedha ni zetu na sisi wala hatupingani, Mimi na wenzangu tumepewa dhamana tu na Serikali lakini haitufanyi tuwe Watanzania kuliko Watanzania wengine”

“Nchi haijengwi na Mtu mmoja tumsaidie Rais Samia, sasa wengine akishaona tozo zimemuudhi anaweka picha anasema ‘Huyu ndio chaguo la Mungu’ anatengeneza mzozo tu hatuna hata uchaguzi, wengine zimekuja tozo tu wanasema ‘Waziri huyu ameagiza Mabasi 60 kwenye Kampuni yake’ Mimi sina hata Kampuni ya Bajaji hivi unaweza ukawa na bweni la Wavulana na Wasichana halafu ukawa na Kampuni ya biashara, sina hata Kampuni ya Bajaji”

“Kisa tozo?, tuongeeni tu hii ni dhamana tu hatuna haja ya kuchafuana, hatuna haja ya kugombana au kuona kuna Mtu mmoja ana nia mbaya na Watu, tumepokea maoni yenu msinung’unike tena yamefika Serikalini na siku sio nyingi tutakuja na majibu”
Screenshot_20220901-182513_OGInsta%2B.jpg
 
Kampuni maarufu ya AZANIA inayouza unga wa ngano na unga wa sembe nchini Tanzania na Nchi jirani kama Burundi na Rwanda, leo imemtangaza Bondia wa Tanzania Dulla Mbabe @official_dullahmbabe kuwa Balozi wake mpya wa unga wake wa SUPER SEMBE.

Unga huu wa mahindi ulianza kuzalishwa na @azaniagroup mwishoni mwa mwaka 2019 kukiwa na lengo la kuwapatia Watanzania unga wa sembe wenye viwango bora na virutubisho vya kutosha ukipatikana katika Mkoa wa Dar es salaam, ukanda wa Pwani na maeneo mengine.
Screenshot_20220901-182645_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi ishu ambayo imekua gumzo nchini kuhusu masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki ambapo amesema “Tumesikia maoni ya Wananchi wengine walisema tupo kimya, tulikuwa kimya tukisikiliza maoni ya Wananchi, tumekutana na Watalaamu wa Kodi tumepata maoni yao maoni yamelenga maeneo mbalimbali ila kubwa ni tozo za miamala ukituma na ukitumiwa na kwenye inatozwa, tumepokea na tunayafanyia kazi na tutatoa majibu ya utekelezaji wake siku sio nyingi”

“Kuweni watulivu wakati tunashughulikia hoja hiyo, tumeona wengine wakizungusha risiti zenye viwango vya tozo wakionesha pesa iliyokusanywa kwenye Benki, tutakutana na Taasisi za Fedha tuone kuhusu hilo, Nchi hii ni yetu wala Mtu usihofie kutoa maoni, hatuna sababu ya kugombana kwenye hoja zenye mantiki”

“Nimesikia malalamiko kuhusu kodi ya upangishaji wa majengo, hii sio sheria mpya ila utekelezaji wake umeanza mwaka huu, wengine wanasema kwanini Mpangaji apewe kazi ya TRA ya kukusanya apeleke fedha TRA, hii sio kodi ya Mpangaji, anayepaswa kulipa kodi ya kupangisha ni Mwenye nyumba na kuhusu Mpangaji anageukaje kuwa mkusanya kodi tumeipokea na tunaifanyia kazi, ni kweli inaweza kumgombanisha na Mwenye nyumba wake na kumpotezea muda”

“Sisi wote ni Watanzania hakuna aliye Mtanzania na nusu, twendeni kwenye misingi ya haki, hivi kama Mtu mwenye kima cha chini anatozwa kodi halafu kuna anayemiliki majengo anapangisha pesa karibu Tsh. Mil 60 halafu tusimtoze kodi kisa mazoea tu, wengine wanasema ‘Huyu Waziri huyu kasoma wapi huyu!?, Phd gani huyu anatoza tozo kwenye majengo ya kupangisha!?’, mnaona ni sawa tumtoze Mtu wa kima cha chini cha Milioni tatu kwa mwaka halafu anayepata Mil 60 tusimtoze?, nyie mnaona ni sawa?”
Screenshot_20220901-182801_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa leo Dodoma amezielezea faida ya tozo kwenye sekta ya afya, elimu na miundombinu katika nukuu zifuatazo “Tozo zimeboresha miundombinu, kwa kipindi ambacho Rais Samia amekuwa madarakani katika Tarafa 570 tayari tumeshajenga vituo vya afya kwenye Tarafa 207 ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani”

“Pia kuna maeneo ambayo ni magumu kufikika tuliyabainisha na kwa kipindi ambacho Serikali ya awamu ya sita imekuwa madarakani kupitia tozo za miamala ya simu tumejenga vituo vya afya 234 kwa Bilioni 117 kwenye tarafa nilizozitaja na maeneo magumu kufikika na kila kituo cha afya kimetugharimu Tsh. Bilioni 500, tangu Uhuru na awamu zote za Serikali ambazo zimekuwepo kujenga vituo vya afya 234 sio jambo la kawaida, tunamshukuru sana Rais”

“Vituo vya afya hivi lazima tuvipeleke vifaa vya kisasa Serikali ilituwezesha TAMISEMI Bilioni 149.5 tumeshakamilisha hatua za manunuzi ili tupeleke vifaa tiba kwenye vituo vya afya “

“Watanzania hapa hoja sio nanufaika vipi na tozo ishu ipo kwenye maeneo ambayo Waziri Mwigulu ameyasema, tusingeweza kujenga vituo vya afya 234 ndani ya mwaka mmoja kama sio hizi tozo, tozo hizi zina faida”
Screenshot_20220901-182923_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi ishu ambayo imekua gumzo nchini kuhusu masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki ambapo alitolea mfano huu na kuwajibu wanaohoji mbona zamani hakukuwa na tozo lakini Nchi ilikua inaenda?.

"Wengine wanasema mbona zamani Nchi ilikua inaenda tu ? ni kweli kabisa Ndugu zangu zamani Nchi ilikua inaenda tu wakati wa Mwalimu Nyerere wanaosoma Shuleni walikuwa wanapewa na mayai kabisa lakini sasa jiulizeni huko Chuoni walikua wangapi ? walikua 12, walikua 7, tuulizeni wengine tuliozaliwa familia ya Watoto 11 hatukujua kama kuku ana robo, hata kipapatio kinakatwa mara tatu wote lazima muenee"

Full video ya Dr. Nchemba akiongea ipo kwenye youtube ya millardayo.
Screenshot_20220901-183107_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi ishu ambayo imekua gumzo nchini kuhusu masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki ambapo hizi ni baadhi ya nukuu ya alichokisema.

“Kwanini mwaka huu tozo ziliendelea tena?, tumeendelea tena kwasababu tumeshafanya kwenye madarasa na vituo vya afya lakini kuna mambo ya msingi ambayo yana umuhimu wa kuchukuliwa hatua kwa haraka sana”

“Tunahitaji kuweka nguvu kubwa sana kwenye shughuli za uzalishaji, tatizo la ajira kwa Vijana ni kubwa mno, Watu wasio na kipato nchini ni wengi sana, kila wanapomaliza darasa la saba kuna Watoto laki mbili hawaendelei na kidato cha kwanza na kila wanapomaliza kidato cha nne kuna Watoto karibu laki tatu hawaendelei kidato cha tano, tumewahi kujiuliza wanaenda wapi na ‘future’ yao ipoje?”

“Tumeshajiuliza wale wanaohitimu na hawaingii Ofisini wanaenda wapi!?, hakuna Kijiji hata kimoja ambacho hakina Mhitimu ambaye hana kazi ndio maana Rais anasema tuweke nguvu kubwa kwenye shughuli za uzalishaji, ndio maana tumeweka pesa nyingi kwenye kilimo ili Vijana wengi watengeneze kipato…. hawa ambao hawana ajira”

“Mnyororo wa umasikini mkiubariki inakuwa unabaki hivyohivyo haundoki kwahiyo zaidi ya Trilioni 1 zimeenda kwenye kuongeza nguvu kwenye uzalishaji upande wa kilimo, uvuvi, Wamachinga” ——— amesema Waziri Nchemba, nukuu zaidi zinafuata lakini pia unaweza kutazama video yake nzima akiongea kwenye Youtube ya millardayo.
Screenshot_20220901-183214_OGInsta%2B.jpg
 
Ziwa Tanganyika halipo Kigoma peke yake bali hadi Congo DR limewafikia pia, leo tumekutanishwa na habari za upande huo na jinsi Ziwa hilo limekuwa tishio kubwa kwa Wananchi wa Mji wa Uvira ambao upo mashariki mwa Congo ambao baadhi wamelazimika kuhama na kwenda kuishi mbali kutokana na ongezeko la kina cha maji yanayozifunika nyumba zao.
Screenshot_20220901-183307_OGInsta%2B.jpg
 
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dr. Albina Chuwa amesema bajeti ya Sensa ya Watu na Makazi na Sensa ya Majengo inayoendeshwa Nchi nzima, iliyoidhinishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha 2022/23 ni Tsh. Bilioni 400 sawa na wastani wa Tsh. 6265 au USD 2.7 kwa Mtu mmoja.

“Tathmini iliyofanywa na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika (UNECA) ilionesha kuwa kwa Nchi za Afrika katika mizunguko ya miaka ya 2020 ni kati ya USD 2.0 hadi 5.0, Nchini Kenya ambayo ilifanya Sensa ya mwaka 2019 gharama iliyotumika kwa Mtu mmoja ilikuwa sawa na Tsh. 8150 au USD 3.52”
Screenshot_20220901-183358_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya soka ya Chelsea imekamilisha uhamisho wa nyota Pierre Aubemayang kutokea Barcelona kwa ada ya Euro Million 14 + Marcos Alonso.

Auba atasaini kandarasi ya miaka miwili na nyongeza ya mwaka mmoja kwa wababe hao wa West London.
Screenshot_20220901-183456_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom