Makapuku Forum

Makapuku Forum

WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujaribu kukwamisha Sensa ya Watu na Makazi mjini Musoma.

Mratibu wa Sensa wa Manispaa ya Musoma, Joseph Ochora amemtaja karani wa sensa, Thomas Ndyetabura kwamba anashikiliwa na polisi tangu juzi kwa kuhesabu kaya moja tu kutwa nzima, baadaye kukutwa akiwa amelewa.

Kwa mujibu wa Ochora, karani huyo alitakiwa kuhesabu kaya 20 hadi 30 kwenye Kata ya Kwangwa, lakini baada ya matendo hayo nafasi yake ikatolewa kwa karani mwingine na kazi inaendelea.

“Changamoto nyingine imetokea Kata ya Kitaji, Barabara ya Shaban Nyumba Namba 28, ambapo kaya moja ilikataa kuhesabiwa, tumewakabidhi polisi,” amesema Ochora.

Amesema kaya hiyo ina binti aliyemtaja kwa jina moja la Leila na mama yake mzazi (hakumtaja majina), kwamba licha ya kugoma kuhesabiwa, waliwatolea maneno ya kashfa karani wa sensa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu amethibitisha uwepo wa matukio hayo.

Screenshot_20220825-212708_OGInsta%2B.jpg
 
Zodwa
Ghaiiiiiiii

Utatuua wewe mtoto...

Baki hapo hapo...
Hilo jina nalipenda kutokana na yule Dada wa Zimbabwe..
Hahahaha basi mama yangu kwa heshima yako sibadilishi tena

Yule rafiki yake zari yeah mimi baadhi ya majina ya wasouth africa nayaelewa

Mnivumilie jamani simu yangu eti keyboard yake hainipei emojis huku jf
 
WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujaribu kukwamisha Sensa ya Watu na Makazi mjini Musoma.

Mratibu wa Sensa wa Manispaa ya Musoma, Joseph Ochora amemtaja karani wa sensa, Thomas Ndyetabura kwamba anashikiliwa na polisi tangu juzi kwa kuhesabu kaya moja tu kutwa nzima, baadaye kukutwa akiwa amelewa.

Kwa mujibu wa Ochora, karani huyo alitakiwa kuhesabu kaya 20 hadi 30 kwenye Kata ya Kwangwa, lakini baada ya matendo hayo nafasi yake ikatolewa kwa karani mwingine na kazi inaendelea.

“Changamoto nyingine imetokea Kata ya Kitaji, Barabara ya Shaban Nyumba Namba 28, ambapo kaya moja ilikataa kuhesabiwa, tumewakabidhi polisi,” amesema Ochora.

Amesema kaya hiyo ina binti aliyemtaja kwa jina moja la Leila na mama yake mzazi (hakumtaja majina), kwamba licha ya kugoma kuhesabiwa, waliwatolea maneno ya kashfa karani wa sensa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu amethibitisha uwepo wa matukio hayo.

View attachment 2334855


Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Hahahaha basi mama yangu kwa heshima yako sibadilishi tena

Yule rafiki yake zari yeah mimi baadhi ya majina ya wasouth africa nayaelewa

Mnivumilie jamani simu yangu eti keyboard yake hainipei emojis huku jf
Kama simu yangu tu..
Na copy na kupaste emoj za watsap.
Muda wote nacheka Kwa style moja.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Hahahaha basi mama yangu kwa heshima yako sibadilishi tena

Yule rafiki yake zari yeah mimi baadhi ya majina ya wasouth africa nayaelewa

Mnivumilie jamani simu yangu eti keyboard yake hainipei emojis huku jf
Eeeeh....Huyo huyo
Usibadili tena kwa kweli...Hili limekaa poa sana...

Kwa nini haikupei emoji? Hata zile za kwenye simu zinagoma?
 
Habibu Anga

Wiki iliyopita kulikuwa na habari kubwa sana. Mamlaka ya kupambana na ufisadi mkubwa nchini Nigeria EFCC walitangaza kwamba wanamsaka mtu anayeitwa Ismaila Mustapha ama jina maarufu ‘Mompha’ ambaye mpaka sasa hajulikani yuko nchi gani japo mara kwa mara anapost picha mitandaoni akiwa anafurahia maisha kwa anasa.

Hii ilikuwa habari kubwa sana kiasi kwamba watu wengi waliuliza huyu mtu ni nani hasa, sababu hata wale ambao wanamuona Mompha mitandaoni bado hawamjui uhalisia wake.

Ukitaka kumfahamu Mompha, wapaswa kuijua walau hata kidogo historia ya Hushpuppi sababu huyu Mompha ndiye ambaye amemfundisha Hushpuppi kuwa tapeli wa kimataifa kwa kutumia mbinu adhimu na za akili kubwa na kuvuna mabilioni ya fedha.

Nieleze kidogo..

Binafsi nimejitahidi sana kutafiti ili kumuelewa Hushpuppi.. kuelewa hasa saikolojia yake. Nini hasa ilikuwa ni chanzo… ‘trigger’… mpaka kumsababisha kufuata mkondo wa aina ya maisha aliyokuwa anaishi.

Nini hasa kilisababisha awe na ‘drive’ aliyonayo mpaka kufikia viwango ambavyo alifikia. Ni nini hasa kilimpa “hasira” ya maisha mpaka kuwa mtafutaji mpambanaji japo si kwa halali.

Yawezekana swali hili kwa wengine lisiwe na umuhimu sana, lakini binafsi limenitesa mno na kunifanya nitafiti mno kuhusu maisha ya Ramon Abbas ‘Hushpuppi’ ili kufahamu ‘chanzo’ kilicho chochea kumfanya awe aina ya mtu aliyekuja kuwa na tukamfahamu.

Sasa,

Mwaka 2018 kuna mwanasiasa pale Nigeria alianzisha kampeni ya kuitaka serikali ichunguze chanzo cha utajiri wa kufuru wa Ramon ‘Hushpuppi’.
Kitendo hiki kilimuudhi mno Ramon ‘Hushpuppi’ kiasi kwamba akamjibu kwa maneno makali yule mwanasiasa.
Kwenye hayo majibu yake Hushpuppi alirekodi video na kuweka kwenye mtandao wa Snapchat.

Katika hii video Hushpuppi alilalamika mno ubovu wa siasa za Nigeria. Akalalamika kuhusu rushwa na namna gani ambavyo wanasiasa wamewatelekeza vijana bila ajira alafu wanamuandama kijana kama yeye ambaye ameenda nje ya nchi kutafuta maisha na amefanikiwa na amekuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengi wa Nigeria…….

Inaendelea Post inayofuata.
Screenshot_20220826-194451_OGInsta%2B.jpg
 
Habibu Anga (2)

Akiwa anaendelea kuongea kwa hasira kwenye hiyo video, Ramon ‘Hushpuppi’ eidha kwa bahati mbaya au kutokana na hasira, aliongea jambo ambalo wengi tulikuwa tunalitamani kulijua kwa muda mrefu sana.. ‘trigger’ ambayo ilitokea kwenye maisha yake na kumfanya awe namna alivyo.

Ramon aliongea kwamba, mama yake anatokea eneo la Niger Delta, eneo ambalo ndilo lenye rasilimali ya mafuta pale Nigeria.

Ramon akaeleza kwamba licha ya mama yake kutokea eneo hilo lenye utajiri mkubwa lakini wananchi karibia wote wa eneo hilo wanaishi kwenye umasikini uliokithiri.

Ramon akatoa mfano hai wa mama yake, ambaye ambaye ana umri wa zaidi ya miaka sitini lakini maisha yake yote hajawahi kunufaika hata kwa kupata dola moja kutokana na jimbo lao kuwa na rasilimali ya mafuta.

Ramon akaeleza kwamba licha ya jimbo lao kuwa na utajiri mkubwa huo wa mafuta, lakini wakiwa wadogo mama yao aliwalelea kwa kuchuuza mikate barabarani na waliishi kwenye umasikini mkubwa.

Ramon akaenda mbali zaidi na kueleza kwamba akiwa mdogo alishuhudia dada yake akipoteza maisha kwa kuugua typhoid kutokana na familia yao kukosa fedha za matibabu.

Ramon akabainisha kwamba matukio hayo yote yalimuathiri sana kisaikolojia akiwa mtoto na hata sasa bado yangali yakimuumiza hasa kifo cha dada yake.

Marafiki wa utotoni wa Ramon wanabainisha kwamba, kifo cha dada yake kwa kuugua typhoid pengine ndio ilikuwa ‘trigger’ ya kumfanya Ramon “Hushpuppi’ kuwa namna alivyo leo hii.
Marafiki zake wanadai kwamba baada ya kifo cha dada yake, Ramon alibadilika kabisa.

Watu wanaomfahamu wanamueleza Ramon alikuwa ni kijana mpole mno na ambaye hakuwa na matukio yoyote ya ajabu mtaani.

Enzi hizo mtaani kwao Hushpuppi watu walikuwa wamembatiza jina wanamuita “Ramoni” kutokana na kupenda sana mitindo ya mavazi.

Sasa, kwenye kipindi hiki, yaani mwanzoni mwa miaka ya 2000’s ndipo pia kulikuwa kumeibuka wimbi la “internent cafes” Africa nzima.

Upepo huu pia ulipitia kwenye mitaa ya Oworo jijini Lagos ambako Hushpuppi na wazazi wake walikuwa wakiishi……
Screenshot_20220826-194900_OGInsta%2B.jpg
 
Habibu Anga (3)

Hiki ndicho kipindi ambacho vijana wa Nigeria walikuja na ile aina ya utapeli wa kujifanya “Prince” ambaye amefiwa na baba yake tajiri.

Utapeli ambao ulikuwa ukifanyika kwa kutuma barua pepe kwa watu wanaotaka kuwatapeli. Kipindi kile karibia kila mtu alikuwa akitumia barua pepe ya mtandao wa “Yahoo” na ndipo hapo likatokea jina la “Yahoo Boys” waliloitwa vijana wanaotafuta hela kwa kutapeli watu mitandaoni.

Hushpuppi naye alijiunga kwenye makundi haya ya vijana “Yahoo boys” waliokuwa wanashinda kwenye internet cafés kutuma barua pepe za utapeli.

Baada ya kupata fedha kidogo toka kwenye shughuli hiyo, Ramon alianzisha biashara ya kuuza nguo za mitumba mtaani kwao.
Hapa kwetu tanzania tunaita “kulenga”. Yaani anaingia sehemu kama Ilala, kisha ‘analenga’ nguo kadhaa nzuri kisha anaenda kuziuza mtaani kwa faida kubwa kutokana na ubora.
Biashara yake hii ilienda vyema kiasi kwamba akaanza kuchukua nguo za asili ya Nigeria na kusafirisha kuzileta Kenya na Uganda ambako soko la mavazi ya Kinaijeria lilikuwa limekolea kipindi kile.

Marafiki zake Ramon wanaeleza kwamba, enzi hizo Ramon ndoto yake kubwa ilikuwa ni kumiliki pikipiki ya kutembelea pamoja na ‘Danfo’. Hii Danfo pale Nigeria ni magari ya usafiri wa umma kama hapa kwetu tunavyoita ‘Dala Dala’.

Kwa hiyo Ramon aliendelea kwa bidii kufanya michoro yake ya mtandaoni lakini pia wakati huo huo akiendelea na biashara ya mitumba.

Ule utaratibu wake wa kupeleka nguo Kenya na Uganda haukufanikiwa sana.. lakini japo safari zake za Afrika Mashariki hazikufanikiwa sana kibiashara lakini zilimpa kitu kingine muhimu sana.
Katika hizi safari zake, Ramon akafahamiana na mtu anaitwa Eddy Kyeyune ( hapo juu pichani ya huyu Eddy Kyeyune).

Jambo moja nataka ukumbuke ni kwamba hii ilikuwa ni miaka ya 2012 kwenda 2013. Kipindi hicho Hushpuppi alikuwa ni ‘kumbikumbi’. Alikuwa na hela ya ugoro tu, hawezi hata kulala Hoteli ya nyota tano. Alikuwa bado kwenye mapambano ya kutafuta mwanya wa maisha afike anapopataka………….
Screenshot_20220826-195258_OGInsta%2B.jpg
 
Habibu Anga (4)

Lakini huyu somo ninayesema kwamba alifahamiana naye, Eddy Kyeyune huyu kipindi hicho pale nchini Uganda tayari alikuwa ni ‘big fish’.

Huyu Eddy Kyeyune jina lake laweza kuwa geni masikioni mwako lakini kuna uwezekano kabisa ukawa unamfahamu.
Kama miaka mitatu/minne iliyopita kulikuwa na watu maarufu sana hapa Afrika Mashariki walikuwa na kikundi chao cha ‘kula bata’ wanajiita “Rich Gang”.

Wanachama wake walikuwa wanafahamika mno kwa kuonyesha maisha ya ufahari na anasa kwenye mitandao ya kijamii hasa mtandao wa Instagram.

Kwenye hii Rich Gang mwanachama maarufu zaidi watu waliyekuwa wanamfahamu alikuwa “Ivan Don”. Huyu alikuwa maarufu kuzidi wenzake kutokana na kumuoa mwanadada Zarina Hassan (Zari).

Lakini lile kundi lao lilikuwa na wanachama karibia saba na viongozi wa kundi hili walikuwa ni Ivan Semwanga (Ivan Don mume wa Zari) na huyu ninayemzungumzia, Eddy Kyeyune.

Ramon ‘Hushpuppi’ na Eddy walikuwa na vitu kadhaa vya kufanana lakini pia walikuwa na tofauti kubwa ambayo iliwafanya urafiki wao usiwe mkubwa sana.

Wote wawili walikuwa wanapenda maisha ya anasa. Lakini walikuwa na aina tofauti kabisa ya utafutaji. Ramon alikuwa “Yahoo Boy” anatapeli mtandaoni. Lakini Eddy na Ivan walikuwa na utapeli wa ‘usangoma’.

Wawili hao walikuwa wanaweka kambi nchini Afrika Kusini kama Sangoma ambao wanatibu matajiri kuwaepusha na mikosi na kuwasaidia kupata ukwasi zaidi.

Wanatoa tiba kwa matajiri na kulipwa hela nyingi sana alafu wanarejea Uganda ‘kuweka heshima mtaani’ kwa matumizi makubwa na anasa mpaka wakawa ‘celebrities’ pale Kampala.

Aina yao hii ya utafutaji ilikuwa tofauti kabisa na Ramon. Na ndio sababu urafiki wao haukuwahi kuwa mkubwa na Ramon hakuwahi kuwa mwanachama wa ‘Rich Gang’.

Lakini japo urafiki wao haukupata nafasi ya kukua sana, lakini Ramon kupitia kufahamiana kwake na Eddy Kyeyune alivuna kitu muhimu zaidi ambacho kilibadilisha kabisa maisha yake.

Eddy Kyeyune alimtambulisha Ramon kwa somo anayeitwa ‘Mompha’ (Ismail Mustapha)………
Screenshot_20220826-195456_OGInsta%2B.jpg
 
Habibu Anga (5)

Mompha kwa kipindi hicho tayari alikuwa ni ‘Big Boy’. Milionea anayeishi maisha ya anasa lakini haijulikani anafanya biashara gani. Kipindi hicho Mompha alikuwa anaishi jijini Kuala Lumpur nchini Malaysia.

Eddy Kyeyune alipomtambulisha Ramon kwa Mompha.. Mompha alivutiwa mno na Ramon “Hushpuppi’ sio tu sababu alikuwa ni Mnaijeria mwenzake lakini alivutiwa zaidi na akili nyingi za Ramon, ubunifu na ‘njaa’ ya maendeleo ambayo Ramon alikuwa nayo.

Kwa hivyo Mompha akamchukua Ramon kutoka Uganda na kwenda naye kwake Kuala Lumpur kwa lengo la ‘ku-mentor’… kumfunda namna gani ambavyo hela zilikuwa zinapatikana.

Sasa,

Huyu Mompha ni moja ya ‘pioneer’… moja ya waanzilishi wa awali kabisa wa aina ya utapeli kitaalamu unaitwa BEC (Business Email Compromise). Ni moja ya watu wa kwanza kabisa kufanya utapeli wa aina hii katika ‘large scale’ mpaka kuwa milionea.

Huyu Mompha chimbuko lake alikuwa ni ‘Yahoo Boy’ kama vijana wengine wengi pale Lagos. Lakini baadae akajiongeza akili na kujiingiza kwenye aina ‘sophisticated’ zaidi ya utapeli kama vile aina hii ya BEC ninayoisema.

Utapeli wa BEC (Business Email Compromise) wenyewe unajikita zaidi katika stadi ya ‘uhandisi jamii’ (social engineering), pamoja na kitu kinaitwa kitaalamu ‘phising’.

Utapeli wa aina hii huwa unalenga kutapeli viwango vikubwa vya fedha na hivyo huwa mara nyingi walengwa huwa ni makampuni makubwa.

Kuna makala niliandika mwaka jana inaitwa “MATUKIO MATATU, MAFUNZO MATATU, BILIONI 900 ZA KITANZANIA”.
Nilieleza matukio matatu, na moja ya tukio muhimu, nilieleza kuhusu wizi wa dola Bilioni moja toka katika benki kuu ya Bangladesh, wizi ambao ulifanywa kwa njia ya mtandao………..
Screenshot_20220826-195944_OGInsta%2B.jpg
 
Habibu Anga (6)

Sasa ufanyikaji wa tukio lile ni mfano mzuri wa matumizi ya stadi ya ‘phising’ na ‘uhandisi jamii’ katika utapeli. Nitaeleza..

Utapeli wa dizaini hii ni adhimu mno na watu wachache sana ambao wana weledi wa kutosha kuweza kuutekeleza kutokana na ugumu wake na kuhitaji kiwango kikubwa cha maarifa na akili.

Lakini ukifanikiwa kuutekeleza basi utavuna mabilioni ya mapesa. Ndio maana waona watu kama akina Mompha na Hushpuppi walikuwa wanaishi maisha ya anasa kama Wafalme.

Utapeli huu huwa una hatua tano katika utekelezaji wake. Hatua ya kwanza ni Identification (kutambua target), hatua ya pili ni ‘Grooming’, hatua ya tatu ‘Observation’, hatua ya nne ‘Exchange of information’ na hatua ya tano ni ‘funds transfer’.

Sitaki kufundisha vijana wetu utapeli lakini nifafanue kwa mifano halisi utapeli huu adhimu wa BEC namna gani ambavyo akina Hushpuppi na Mompha walikuwa wanafanya na kuvuna mabilioni ya fedha.

Makala hii inapatikana yote kwa ukamilifu kwa members wa Group langu la WhatsApp.

Kuwa mwanachama wa Group unalipia shilingi elfu tano tu kwa mwezi na utapata Makala hii pamoja na Makala nyingine nyingi kwa muda wa mwezi mzima.

Fanya malipo ya shilingi elfu tano kwenda MPESA 0759181457 HABIBU ANGA kisha nijulishe nikuunge na uanze kupokea simulizi.

Unaweza pia kubofya link kwenye bio yangu ambayo itakuleta moja kwa moja inbox whatsapp.
Screenshot_20220826-200100_OGInsta%2B.jpg
 
WATOTO wanne wamefariki dunia kwa kuungua moto uliowashwa na mganga wa kienyeji kwa lengo la kuondoa mikosi kwenye familia.

Watoto hao waliungua moto wakati wakigombania kutoka nje ya kibanda baada ya moto huo uliokuwa umezunguka kibanda hicho kuzidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa tayari mganga anayetuhumiwa kuhusika katika tukio hilo amekamatwa na upelelezi wake unaendelea.

"Ni kweli tuna taarifa ya tukio hilo na upelelezi wa tukio zima tunaendelea nao," amesema Kamanda Ambwao.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kigwa, Bakari Kabata, amesema watoto waliofariki hawazidi umri wa miaka kumi na tano ambao ni wa familia moja.

Akielezea tukio hilo, Diwani huyo amesema mwenyeji mwenye mji huo, alimuita mganga kwa mambo ya kimila, akimtaka kumuondolea mikosi kwenye nyumba yake na mganga huyo kusababisha maafa hayo.

Ameeleza kuwa mama wa familia ni miongoni mwa majeruhi saba ambao wamelezwa Hospitali ya Omulinga na ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete.

Katika tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jana Alhamisi, amesema kuwa wanafamilia wapatao ishirini walikuwa kwenye kibanda kilichowashwa moto na mganga huyo aliyewapa sharti la kutoka mmoja mmoja baada ya moto kuwashwa.

Hata hivyo moto ulipokuwa mkali, ulisababisha wanafamilia kugombea kutoka nje wakisukumana na watoto hao kuwa waathirika wakubwa na kufariki dunia.
Screenshot_20220826-202318_OGInsta%2B.jpg
 
Makarani wawili wa Sensa ya Watu na Makazi katika Kata ya Lamadi, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, wanachunguzwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa vishikwambi vya Sensa.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Gabriel Zakaria ameviambia vyombo vya habari kuwa makarani hao Saphina Francis na Yona Mwalongo kwa pamoja wameibiwa vishikwambi hivyo majira ya saa tisa usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu, wakiwa wamelala ndani ya nyumba moja.

"Baada ya kuhojiwa na polisi, makarani hao wanadai walifunga mlango na geti lakini hakuna sehemu yoyote ya nyumba waliyokuwa wamelala imevunjwa, na hivyo kuagiza polisi kuwahoji na kuwachunguza kwa uzembe uliosababisha upotevu wa mali ya umma," amesema Gabriel.
Screenshot_20220826-202559_OGInsta%2B.jpg
 
Msimamizi wa Maudhui katika Sensa ya Watu na Makazi Kata ya Rau, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, ameibiwa kishikwambi baada ya kuacha begi dukani kwa mtu.

Mratibu wa Sensa Mkoa wa Kilimanjaro, Albert Kulwa ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa Agosti 26, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, ambapo amesema tukio hilo ni la kizembe na limetokea Agosti 25.

Kwa mujibu wa Kulwa, msimamizi huyo alipomaliza majukumu yake jioni alikwenda katika duka lililopo jirani na kuomba ahifadhiwe begi lakini ghafla begi hilo likapotea kwenye mazingira ya kutatanisha.
Screenshot_20220826-202732_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu kodi ya pango ikisema kawa sio mpya bali wigo umengezwa kwa wapangishaji wa nyumba binafsi kama ilivyokuwa kwa wenye nyumba za biashara ambapo nao wamejumuishaa kwenye wigo wa kodi kuanzia July Mosi 2022.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya huduma na Elimu kwa Mlipakodi imesema
“Tunapenda kuwafahamisha Wananchi kuwa kodi hiyo sio mpya bali wigo umeongezwa ili Wapanganishaji wa nyumba binafsi kama ilivyokuwa kwa wenye nyumba za biashara nao wamejumuishaa kwenye wigo wa kodi kuanzia July Mosi 2022”

“Mwenye nyumba atapata cheti cha kodi ya zuio kama ushahidi wa malipo ya kodi iliyolipwa kutokana na zuio la asilimia 10.

Akiwa katika mafunzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022 wilayani Bariadi jana Ofisa huduma na elimu mkuu kutoka TRA, Eugenia Mkumbo aliwasisitiza wapangaji kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.
Screenshot_20220826-202848_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom