Sitaki Ndoa!- (A Short Story ) - 3
"Sasa kwa nini hutaki ndoa", aliuliza tena Padre.
"Padre si ukweli unamweka mtu huru?", ilikuwa zamu ya Jane kuuliza sasa.
"Mkitaka niseme ukweli, nitausema", alisema Jane
"Hatuko kituo cha Polisi wala hatuko mahakamani mwanangu Jane", alisema Padre na kuongezea, "Ninyi mmekuwa pamoja muda mrefu, kwa sasa mnachotaka kufanya ni kuyakabidhi maisha yenu mikono mwa BWANA kwa ndoa Takatifu."
"Naelewa Padre, lakini siko tayari" alilisitiza Jane.
Wakati wote huu Moses alikuwa kimya.
"Tatizo ni nini Jane, nimewahi kukupiga, mmewahi kula njaa, nimewahi kushindwa kukupa matumizi", aliuliza Moses.
"Hapana Moses, wewe ni mwanaume na nusu zaidi wewe ni mtu mwema sana na siku zote umekuwa baba mzuri kwa mtoto wetu", alisema Jane
"Tatizo ni nini sasa", aliuliza tena Moses.
"Tatizo ni kwamba sishibi", Jane alidakia.
Padre alishtuka kidogo na kumgeukia Moses, "Moses umekuwa muamini mzuri sana, unashiriki jumuiya, michango yote unatoa, lakini hununui chakula nyumbani kwako"
"Chakula Padre, nenda kwangu friji limejaa vyakula, stoo kuna mchele na mahindi ya kutosha hata miezi 6", Moses alijieleza na kukumbuka maneno kwamba mapenzi yakifika mwisho, hata panya akidondosha glasi unaambiwa ni wewe. Kumbe Jane alikuwa na chakula chake.
"Father, ngoja niseme, nieleweke vizuri. Kwa kweli tangu nianze mahusiano na Moses hajawahi kuniridhisha. Hajawahi kunifikisha kileleni." wakati huu Jane alikuwa ameangalia pembeni.
"Mimi napenda sana kufanya mapenzi, lakini mwenzangu ndio hivyo amekuwa hanifikishi popote. Najuta kwamba katika kipindi chote hicho nimekuwa nikilala na wanaume wengine ili kukata kiu yangu. Hiyo ndio sababu sitaki Ndoa. Sitaki kuzini nikiwa kwenye ndoa. Niko tayari tuishi hivi hivi mpaka tuzikane lakini sio kufunga ndoa." alimaliza na kisha akamgeukia Moses ambaye wakati huu alikuwa ameegea meza.
"Nakupenda Moses, lakini ndoa na wewe sitaki"
Padre alimuita Moses, Moses hakuitika, akampiga piga begani, Moses hakushtuka, Padre akapiga kelele kuomba msaada kisha kumkimbiza hospital ya misioni iliyokuwa mita chache kutoka hapo parokiani.
"Mgonjwa wenu ameishafariki, poleni sana" daktari alisema.