Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kamati ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na ukaguzi wa klabu za Ligi Kuu ya NBC na leo wamefanya ukaguzi katika Klabu ya Yanga.
Screenshot_20220819-042054_OGInsta%2B.jpg
 
Watu watano wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya basi la Tanzanite kupinduka katika kijiji cha Mbwasa wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumatano Agosti 17, 2022 ambapo basi hilo lilikuwa linatoka Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa amesema kuwa ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo lilipokuwa likishuka kwenye mlima Saranda na kusababisha vifo vya watu watano akiwamo Diwani wa Iramba Mwinjuka Mkumbo (40).
Screenshot_20220819-042149_OGInsta%2B.jpg
 
YANGA imeanza Ligi Kuu Bara kama ilipoishia msimu uliopita ikishinda ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania, lakini staa mmoja ameibua vita mpya iliyowahusisha viungo sita wa timu hiyo akiwamo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Gael Bigirimana.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alimuanzisha Aziz Ki kama winga katika mchezo dhidi ya Simba katika dakika 45 za kwanza, lakini kile cha pili alimrudisha kucheza kama namba 10 nyuma kidogo ya mshambuliaji wa mwisho na jamaa akaonyesha makali katika eneo hilo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nabi alisema alijaribu kumpeleka pembeni Aziz Ki, lakini ilishindikana na sasa anataka kuendelea kumuamini staa huyo wa zamani wa ASEC Mimosas kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho baada ya kuanza kuonyesha makali.

Screenshot_20220819-042311_OGInsta%2B.jpg
 
Aliyekuwa kiungo wa Simba, Taddeo Lwanga akiwa mazoezini na wachezaji wenzake katika Klabu yake mpya ya Arta Solar 7, ya Djibouti.
Kiungo huyo amejiunga na Arta ambayo wanachezea mastaa wa zamani wa Chelsea na Barcelona, Solomon Kalou na Alex Song.
Taddeo amejiunga na timu hiyo baada ya kuachana na Simba mwanzoni wa msimu huu wa 2022/23.

Screenshot_20220819-042422_OGInsta%2B.jpg
 
ADEBAYOR ALIYEYUKIA HAPA SIMBA!!
.
“Nia tulikuwa nayo lakini hiyo changamoto (Mshahara) ilitufanya kumkosa, Simba hatujafikia levo ya kumpa mchezaji Dola 25,000 (sh 58milioni) wachezaji wetu Dola 1,000 au 1,500 hatuwezi kumlipa mmoja hiyo pesa kubwa kiasi hicho wakati uwanjani wanacheza 11 inakuwa sio sawa ndio maana tulikubali kumkosa.
.
“Sio yeye tu wapo wengi ambao tulikuwa tukionyesha nia ya kuwataka basi timu nyingine zinamkimbilia hiyo inaonyesha ukubwa wetu ulivyo kwa sasa, sisi tuna mtandao mkubwa tukigusa tu wanaibuka,”

- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’.
Screenshot_20220819-042922_OGInsta%2B.jpg
 
ISHU YA DILUNGA IKO HIVI
.
“Dilunga aliumia akiwa katika majukumu yake ndani ya klabu, baada ya kumpeleka Afrika Kusini kutibiwa sasa hivi yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa Simba.
.
“Sisi tutaendelea naye mpaka dirisha dogo tuone hali yake, kama atakuwa amepona bado tunamhitaji sana. Naamini Mungu atamsaidia atarejea katika hali yake mchango wake tunauth
amini,”

- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’.
Screenshot_20220819-043027_OGInsta%2B.jpg
 
MMEMSIKIA KOCHA NABI KUHUSU AZIZI KI !?
.
“Nilitamani Azizi Ki angeweza kucheza pembeni ili tutengeneze nafasi pana ya wengine kuweza kupata nafasi ya kucheza, lakini tunaona jinsi alivyo na ufanisi akicheza pale nyuma ya mshambuliaji wa mwisho,”
.
“Tuna viungo sita ambao sasa tutalazimika kuwatumia katika maeneo ya kati pekee. Hili litaleta ushindani zaidi baina yao kuhakikisha wanakuwa katika ubora kuwania nafasi.
.
“Haitakuwa kazi rahisi kwetu kama makocha katika kuchagua nani anatakiwa kuanza viungo wetu wengi bora ambao kila mmoja anatamani kucheza, tutalazimika pia kuwa na mzunguko wa kuwapa nafasi.”
Screenshot_20220819-043546_OGInsta%2B.jpg
 
MOLINGA APIGWA CHINI NAMUNGO
.
Klabu ya Namungo imeachana rasmi na aliyekuwa Mshambuliaji wake, David Molinga Falcao baada ya nyota huyo kumaliza mkataba wake na kushindwa kuwaridhisha viongozi.
.
Taarifa za Kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo zilieleza kufikia makubaliano na staa huyo wa zamani wa Yanga huku sababu ikielezwa kushuka kiwango.

…………………….
Screenshot_20220819-043631_OGInsta%2B.jpg
 
OFFICIAL| KABWILI RAYON SPORTS
.
Aliyekuwa kipa wa Yanga, Ramadhan Kabwili amesaini mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya Rayon Sports inayoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda.
.
Haikuwa ngumu kwa Rayon kumpata kipa huyo aliyewika na Serengeti Boys iliyoshiriki Afcon ya vijana mwaka 2017 nchini Gabon kwani alipendekezwa na kocha wa makipa wa timu hiyo Mrundi Vladimir Niyonkuru aliyewahi kufanya kazi na Kabwili ndani ya Yanga miaka kadhaa nyuma.
.
Rayon inajipanga kurudisha Ufalme wake kwenye Ligi Kuu ya Rwanda baada ya msimu uliopita kumaliza katika nafasi ya nne.

……………..
Screenshot_20220819-043737_OGInsta%2B.jpg
 
MO SALAH ARUDISHA MKWANJA KWA JAMII
.
Supastaa Mohamed Salah amechangia Pauni 130,000 kusaidia ujenzi wa kanisa lilochomwa moto huko Misri na kusababisha vifo vya watu 41. Kanisa la Abu Seifein Church, lililopo katika mji wa Giza, lilichomwa moto Jumapili.
.
Na Salah ameamua kuonyesha utu wake kwa kuchangia kiwango hicho cha pesa, ambacho ni sawa na Sh 307 Milioni za Kitanzania.
.
Jambo hilo lilimfanya mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, anayekipiga Liverpool kupewa sifa nyingi kwenye mitandao ya kijamii.
Screenshot_20220819-043835_OGInsta%2B.jpg
 
Adriano moja kati ya vipaji halisi vya mpira, haikuwa rahisi kumpora mpira, ilikuwa ni burudani kumtazama akiwa uwanjani, dunia ilimatabiria makubwa sana ila akaondoka kwenye matarajio hayo ndani ya muda mfupi sana
Screenshot_20220819-043935_OGInsta%2B.jpg
 
| Manchester United wameanza mazungumzo na Real Madrid pamoja na kambi ya Casemiro juu ya uwezekano wa kuinasa saini yake

- Real Madrid na United wataendelea na mazungumzo hayo kesho huku Kocha Ancelotti akipewa nafasi ya kuamua hatma ya Mbrazil kama anamhitaji kikosini

- United wapo tayari kumpa Case mara mbili ya mshahara ambao analipwa Real Madrid
Screenshot_20220819-044019_OGInsta%2B.jpg
 
Picha zitakazoishi miaka mingi, picha ambazo zinaweza kukumbusha ujana wako ndani ya EPL, picha ambazo zinaweza kukumbusha kuhusu TVT miaka ile wanarusha EPL, picha ambazo zinaweza kukumbusha sauti ya Juma Nkamia

Those good old days when these two battled against each other
Screenshot_20220819-044355_OGInsta%2B.jpg
 
️ 2009: Inter Milan walimuuza Philpe Coutinho
2010: Inter wakashinda UEFA

️ 2018: Liverpool walimuuza Coutinho
2019: Liverpool wakabeba UEFA

️ 2022: Barcelona wamemuuza jumla Coutinho
2023:
Screenshot_20220819-044447_OGInsta%2B.jpg
 
Hapo kashawachafua sana watu, halafu wamemkanyaga, imebidi amfuate Colina atoe kadi ila Muitaliano alikuwa anameza tu filimbi

Football those days beauty beauty
Screenshot_20220819-044640_OGInsta%2B.jpg
 
Shaffih Dauda

Kwenye umri wa miaka 22 tayari George Best alikuwa staa za Ireland Kaskazini na Manchester United, huku akiwa ametwaa Ballon dor

Alipofikisha umri wa miaka 28 tayari alikuwa na makombe sita makubwa ikiwemo UEFA na mabao 181 kwenye jezi ya Manchester United, lakini alishindwa kumudu presha ya umaarufu na pesa

Pombe na wanawake zilikuwa starehe zake kubwa sana George Best, ilifika wakati alidiriki kusema alijaribu kuacha wanawake na pombe kwa dakika 20 tu lakini zilikuwa dakika ngumu zaidi kwenye historia ya maisha yake

Matumizi ya kupitiliza ya pombe yalimsababishia maradhi ya ini huku pia wanawake wakimfanya awe na afya duni pia, stori ilibadilika ghafla sana

Wakati anakimbizwa hospitalini baada ya hali kuwa mbaya zaidi 2005, aliwaambia watu wake wanunue kurasa kwenye gazeti fulani na akaweka tangazo “TAFADHALI MSIFE KAMA MIMI”

Ujumbe kwenu vijana, msife kama yeye

DIGALA
Screenshot_20220819-044833_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom