Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220819-052614_Opera%20Mini.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Mashabiki
.
Ni kweli mmiliki wa haki za matangazo anatoa pesa nyingi kuliko mshirika yeyote wa ligi kuu kwa sasa. Na anapaswa kuheshimiwa.

Ni kweli tunapaswa kuheshimu viwango vya pesa na kuwapa thamani inayostahili washirika walomwaga pesa. Na inapaswa kuwa hivyo.

Lakini ndio uweke Mechi ya Ligi, siku ya kazi halafu saa nane mchana..? Hata sisi machizi soka, wamachinga muda huo tunatafuta pesa.

Ratiba za mechi inazuia sana watu kwenda uwanjani, tunatumia nguvu kubwa kushusha mapenzi ya watu kwa mchezo na timu zingine ambazo sio kutoka kariakoo.

Mashabiki wanapungua kila siku kuingia viwanjani, Ratiba utaathiri pia mashabiki kutazama kwenye Televisheni na ubize ukiwa wa kutosha hata APPLICATION haifui Dafu.

Che Guevara
.
Screenshot_20220819-074407_OGInsta%2B.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Nidhamu.
.
Ili kufanikiwa lazima kutengenezwe nidhamu ya kweli katika dhana ya utendaji. Kama tutaachia vitendo vya hovyo basi tutaruhusu kuharibika kwa mchezo wenyewe na hatimaye biashara kuvurugika.
.
Kitendo cha Inonga sio cha kiungwana na kitendo cha Sure Boy sio cha kiungwana lakini Mamlaka za Usimamizi kunyamaza ni ashirio la kukosa uungwana zaidi kwa maslahi mapana ya Soka la Nchi hii.
.
Tuliwahi kuona namna Mukoko aliigharimu Yanga kwa Kutaka kulipiza Rafu kwa John Bocco baada ya Bocco kutoadhibiwa na Muamuzi katika mchezo ulopita. Hapo iliathirika klabu, kuna siku itaathirika "CARRIER" ya moja ya Vijana mahiri.
.
Tufanye maamuzi kwa maslahi mapana na sio muktadha wa kisiasa kwa Soka letu. Tuwanusuru vijana na kuiga mambo ya Hovyo.
.
Che Guevara
Screenshot_20220819-074536_OGInsta%2B.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Biashara ya Masihara.
.
Mimi nataka nini kwenye soka..? Mimi nataka kuacha alama ya mabadiliko, mwanzo kuna watu walikua wanachukia lakini sasa wengi wanafurahia na tunacheza midundo inayofanana. Leo kila kinachotokea kinatokea kwa namna ya kipekee kabisa, na kila kitu kinabadilika.
.
Wakati tunakilia pesa za wadhamini, Tunafanikiwa tunazipata tunawapa wadhamini wanachotakiwa kupewa lakini je, wadhamini nao wanajua wanachotakiwa kufanya baaada ya kutoa pesa zao..? Nimeamua kuuliza hivi sababu kuna mambo ambayo yanatokana na pande zote mbili au kukosa umakini wakuifanya biashara.
.
Msimu ulopita Yanga ilikua timu ya kwanza kubandika LOGO ya Mdhamini Mkuu, mwaka huu kaanza ligi bila kumbandika na timu nyingi zikifanya Dhulma hiyo ya kibiashara. Chanzo changu makini kabisa kinaniambia kosa sio vilabu tu bali wadhamini nao wanajidhulumu sababu kuna muda nao wanachelewesha vibandiko.
.
Ni wakati sasa wa kuamua aidha kufanya Biashara au kutokufanya kuliko kufanyafanya. Haya makosa madogo ambayo pia yapo kwenye kanuni yanapaswa kufutwa kabisa sababu inafukuza wadhamini wengine wanaofikiri ni Msimamizi wa Vilabu (Bodi Ya Ligi) ndiye anashindwa kufanya kazi kumbe kuna sehemu na nayetaka kufanyiwa kazi anakosea.
.
Huu ni wakati wa Hela, hiki ni kizazi cha Gharama.
.
CHE GUEVARA
.
NB:
Hivi ni dhambi ukiwa Rais wa TFF kisha ukawa mwanachama hai wa Coastal Union.?
Screenshot_20220819-074750_OGInsta%2B.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Wana wa Uzao Wetu
.
Angalia picha ya kikosi cha Simba, hiyo picha ilipigwa 1.06.2003 pale Cairo Misri, angalia tena na kisha mwishoni utamuona Bishoo aliyesuka, hana papara na wakati huo unaweza kudhani ni moja ya mastaa wa Kinaijeria na ndiye aliyeongoza mapambano ya kuwatoa Zamaleki, kama humjui huyo ndiye SELEMAN ABDALLAH MATOLA.
.
Miaka zaidi ya 20, ameishi akiujua utamaduni wa wanasimba, ametumika kama Mchezaji, Nahodha na sasa kocha msaidizi, anaujua utamaduni wa klabu na bila shaka yeye ndiye mlizi sahihi wa mifumo na Utamaduni wa klabu ya Simba Kuonesha hayupo hapo bahati mbaya angalia wachezaji wangapi wamepita ila yeye Yupo.
.
Tumeamua kuishi kwenye kasumba ya Roho mbaya, tumeamua kuishi kwenye dunia ya kutoheshimiana kisa tunajuana. Wanaosema Matola afukuzwe hawana Hoja, hoja yao kubwa ni kwa nini wengine wote waondoke yeye abaki..? Haya ni matokeo ya roho mbaya na kasumba yetu ya kupenda aidha wote tukose au nipate yeye akose.
.
Wakati sisi tunawaza namna ya kuwaomba msamaha kina Mkwasa kwa kushindwa kuwaheshimu kuna hawa Vinaja wa SOSHO MEDIA wanaanza Dhambi mpya ya kuwadharau kina Matola. Leo kesho natamani Said Maulid akae Benchi la Yanga, natamani pale Costal Guardiola Mweusi aheshimiwe. Halafu wewe unakuja unamsema hovyo MZAWA.? UNANIUDHI.
.
Simba inafungwa kutokana na mipango ya Uongozi na sio uwepo wa Matola, Matola ni Moyo wa Simba ni alama ya Uzao na kumbukumbu nzuri ya Wana wa Msimbazi. Kashinda kila kitu kama kocha na kama mchezaji, kabla hujaongea basi kuwa na Heshima, Binafsi nampa #HeshimaFullTank, Yeye ni Alama ya Utamaduni wa wanasimba.
.
VALUE THEM HOME BOYS
.
NB:
Tuishi Upendo, Tuishi Uzawa, Tujifunze kwa Wageni
Screenshot_20220819-074913_OGInsta%2B.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Ni Utambulisho.
.
Naona tumeondoka kwenye AGENDA za kujenga nchi na sekta ya michezo haswa soka. Tumeacha kujadili maendeleo na kufungiwa viwanja tumeenda kwenye mjadala mfu na masihara yasokua na maslahi kwetu. Tumeamua kujadili vitu visivyoshikika, Tumeamua Kuhamisha GOLI.
.
Kiswahili chetu hakijatufundisha MISAMIATI mingi na pengine toka umezaliwa hujawahi kuwa na neno mbadala la watu wanaotoka Bara la Ulaya au Amerika haswa wenye asili ya weupe. Sisi msamiati wetu ni mmoja tu, sisi tunaita MZUNGU na wala hatuoni ubaguzi. Kwetu huo ni UTAMBULISHO, kama Mchaga na Mfipa.
.
Hakuna namna nyingine tunatambuana kirahisi, kwa nini MZUNGU iwe ishu wakati kina Mayele tunawaita WACONGO na hakuna shida..? Kuna sehemu tunaipamba bila mantiki, leo hii eti Mzungu imegeuka Sifa tena na wala sio UTAMBULISHO. Tusitengeneze maana ya mtaani bali tuishi kwenye maana yetu ambayo tumekua tukiwaita WAZUNGU.
.
Jose Morinho amewahi kusema, ukitaka ushindi basi sajili straika wa KIAFRIKA au Babu Ferguson aliwahi kusema wachezaji wa KIBRAZIL wanaendekeza sana starehe, haikua ishu sababu ni utambulisho. Hakuna namna tutabaguana kwa utambulisho hadi kwa matendo yetu ya hovyo, kwa mfano kule ITALIA Wanavyowaita kina BALOTELI Kuwa MANYANI.
.
Kwangu MZUNGU Sio Sifa, kwangu Mzungu ni mgeni Mweupe kutoka Ng'ambo, sio Sifa eti mtu anayejali muda au mtu asiye na ROHO MBAYA. Alichokifanya AHMED ALLY ni utambulisho wala hakuna chembe ya Ubaguzi, hizi Dhihaka na Nyimbo ni sehemu ya Utani katika Soka letu. Tanzania yangu inawatambua watu wa Ng'ambo haswa ulaya kuwa ni WAZUNGU.
.
Tubaki kwenye UTAMBULISHO.
.
Che Guevara
.
NB:
JAJA ndiye alikua Mbrazil wa Mchongo, ila DARIO wa kweli.
Screenshot_20220819-075052_OGInsta%2B.jpg
 
Kampuni ya Morning Sight Investment imeitambulisha rasmi hoteli yake mpya iliyoijenga Kigamboni Jijini Dar es salaam iitwayo AYA SOPHIA VILLA ikiwa ni moja ya uwekezaji mkubwa uliofanywa kwa mwaka 2022 ndani ya Jiji la Dar es salaam.

Uongozi wa Hoteli hii ya @ayasophiavilla ambayo imejengwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwenye eneo la Mbutu Beach umesema bei ya chini ya Villa moja kwa usiku mmoja ni dola za kimarekani 200 ( Tsh. 466,401) na vimepangika kama ifuatavyo.... VIP Villa ambayo ni dola 250 kwa usiku mmoja, Vip family ambayo ni dola 350 kwa usiku mmoja, Golden Villa ambayo kwa usiku mmoja ni dola 200 na mwisho ni Royal Villa ambayo kwa usiku mmoja ni dola 350.

Huu ni uwekezaji mwingine mkubwa kushuhudiwa kwa mwaka 2022 kwenye Jiji la Dar es salaam na hasa Kigamboni ambako kuna utulivu mkubwa na mara zote Watu hupendelea kwenda kupumzika iwe ni kwenye siku za wiki au mwishoni mwa wiki.

Hoteli hii ambayo pia ina Wanyama mbalimbali ambao Wageni wanaruhusiwa kupiga nao picha na kuwalisha, tayari imeanza kupokea Wageni na Uongozi umeahidi kufanya mahojiano maalum na AyoTV ya kuuonesha uwekezaji huu kwa undani zaidi ikiwemo kuonesha vyumba, swimming pool 7 ilizonazo, idadi ya ajira zilizozalishwa na mengine “Watupigie kwenye 0673377777 0672377777 au ayasophiahotel.co.tz” View attachment 2327886View attachment 2327888View attachment 2327889
pazuri sana kufanyia matusi na mtoto wa mtu na kupumzika, acha nisake $200
 
On Lobi Manzoki.

• Yanga officials were in Uganda to negotiate with Vipers over a possible transfer for Manzoki.

• Both teams reached an agreement, I can confirm that 100%.

• Lobi refused to play for Yanga and he said, he’s a man of his words as he already said he will play for Simba SC.

• He’s informed my team and me that he don’t want to disappointed Simba SC since he already agreed and he love Simba.

• He said for now, he’s focused on Simba and will only think about a move to a different country but in Tanzania he will play only for Simba. This is what he said himself to us.

• Still no agreement between Vipers and Simba for Manzoki.

• Manzoki said, he’s going to wait for Simba.

• All in the hands of Simba now.

• That’s all for now.

Screenshot_20220819-090042_OGInsta%2B.jpg
 
| NOSIRU AFEEZ SIMBA SC
.
Simba inaendelea na mikakati ya chinichini ya kumalizana na mido mpya kutoka Nigeria NosiruAfeez Babatunde (@nosiru_afeez) anayekipiga katika klabu ya Kwara United.
.
Afeez anayetumia mguu wa kulia anasifika kwa kukaba, ufundi wa pasi na kupiga mashuti ya kuua makipa Nosiru anapewa nafasi kubwa ya kusajiliwa kuchukua namba ya Victor Akpan anayetolewa kwa Mkopo.
.
Kuna Jambo leo weka notification On
Screenshot_20220819-090328_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom