Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kampuni ya Morning Sight Investment imeitambulisha rasmi hoteli yake mpya iliyoijenga Kigamboni Jijini Dar es salaam iitwayo AYA SOPHIA VILLA ikiwa ni moja ya uwekezaji mkubwa uliofanywa kwa mwaka 2022 ndani ya Jiji la Dar es salaam.

Uongozi wa Hoteli hii ya @ayasophiavilla ambayo imejengwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwenye eneo la Mbutu Beach umesema bei ya chini ya Villa moja kwa usiku mmoja ni dola za kimarekani 200 ( Tsh. 466,401) na vimepangika kama ifuatavyo.... VIP Villa ambayo ni dola 250 kwa usiku mmoja, Vip family ambayo ni dola 350 kwa usiku mmoja, Golden Villa ambayo kwa usiku mmoja ni dola 200 na mwisho ni Royal Villa ambayo kwa usiku mmoja ni dola 350.

Huu ni uwekezaji mwingine mkubwa kushuhudiwa kwa mwaka 2022 kwenye Jiji la Dar es salaam na hasa Kigamboni ambako kuna utulivu mkubwa na mara zote Watu hupendelea kwenda kupumzika iwe ni kwenye siku za wiki au mwishoni mwa wiki.

Hoteli hii ambayo pia ina Wanyama mbalimbali ambao Wageni wanaruhusiwa kupiga nao picha na kuwalisha, tayari imeanza kupokea Wageni na Uongozi umeahidi kufanya mahojiano maalum na AyoTV ya kuuonesha uwekezaji huu kwa undani zaidi ikiwemo kuonesha vyumba, swimming pool 7 ilizonazo, idadi ya ajira zilizozalishwa na mengine “Watupigie kwenye 0673377777 0672377777 au ayasophiahotel.co.tz”
Screenshot_20220819-040749_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220819-040808_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220819-040921_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema ujenzi wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT II), Awamu ya Pili kutoka Mbagala hadi Gerezani umefikia asilimia 66.6 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Februari, 2023.

Prof. Mbarawa amesema hayo jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo ambapo amefafanua kuwa kazi zinaenda vizuri huku ikitarajiwa kuwa mradi huo kukamilika kwa muda uliopangwa ili uweze kupunguza msongamano wa magari na kurahisisha usafiri.

“Nimefurahi kazi inaenda vizuri ila bado nitakuwa nikija hapa kukagua mradi huu mara kwa mara ili kuhakikisha mkandarasi anamaliza kwa wakati na viwango kwa sababu mradi huu ni muhimu sana katika kurahisisha usafiri na kupunguza msongamano”

Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anakamilisha upande wa pili wa barabara za juu (flyover) ya Chang’ombe na Kurasini ifikapo mwezi Oktoba ili kuruhusu magari kupita juu huku kazi nyingine zilizobakia zikiendelea.

Amemtaka pia kukamilisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 80 eneo la BP ifikapo mwezi Desemba 2022 na madaraja mengine kukamilishwa mwezi Januari, 2023 ili kupunguza changamoto ya msongamano wa magari katika maeneo hayo.
Screenshot_20220819-041049_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya Serikali ya Japan kukumbwa na kitu ilichokiita "tatizo lisilo la kawaida" ambalo ni Vijana wengi nchini humo kutokunywa pombe vya kutosha tangu janga la corona litikise dunia hivyo kusababisha mauzo na mapato ya ushuru kuporomoka Nchini humo, sasa imebuni shindano la kupata njia za kibunifu za kuhamasisha Vijana kunywa pombe.

Serikali ya Japan ikiongozwa na Wakala wa kutoza ushuru imeanzisha kampeni iitwayo “Sake Viva!" likiwa ni jina la kilevi maarufu nchini humo na kutaka Washiriki wa shindano la kutafuta njia mpya ya kuhamasisha Vijana kunywa pombe kuwasilisha maoni yao juu ya jinsi ya kuhamasisha unyaji pombe kwa vijana kwa njia za utangazaji, miundo na hata mbinu za uuzaji kwa kutumia AI au teknolojia endelevu.

Japani ilipokea yen trilioni 1.1 (dola bilioni 8.1) katika ushuru uliotoka kwenye uuzwaji wa pombe kwa mwaka 2021 sawa na asilimia moja 1.7% ya mapato ya jumla ya ushuru ikiwa ni tofauti na asilimia 3% waliyoipata mwaka 2011 au asilimia 5 waliyoipata mwaka 1980.

Shindano hili linajumuisha mawazo ya jinsi ya kutangaza aina mbalimbali za pombe za Kijapani huku nafasi ya kuwasilisha maombi ipo wazi mpaka Septemba 9 2022 ambapo Washiriki wataalikwa kwa mashauriano ya kitaalamu October 2022 kabla ya mchuano wa mwisho Novemba jijini Tokyo.

Hata hivyo Serikali hii imekosolewa vikali na baadhi ya Watu ambao wanaona ni uamuzi mbaya na unaoweka maisha ya Vijana hatarini.
Screenshot_20220819-041330_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameridhia tarehe 23 Agosti 2022 iwe siku ya mapumziko ili Watanzania wawepo majumbani na waweze kuwapokea Makarani wa sensa na kutoa maelezo sahihi.
Screenshot_20220819-041431_OGInsta%2B.jpg
 
Watu watatu wa familia moja Wakazi wa Kitongoji cha Idoselo, kijiji cha Kasesa jimbo la Busanda Wilayani Geita mkoani Geita wamefariki kwa kupigwa na radi huku mwenzao mmoja akijeruhiwa katika tukio hilo.

Akisimulia tukio hilo kwa Majonzi Baba wa Familia hiyo James Lubiyu amesema tukio hilo wakati linatokea Marehemu wote walikuwa ndani ya nyumba wamejikinga na mvua ambapo radi ilipotokea athari zilianza kuonekana kwenye miti.

Waliofariki ni Bibi wa familia Mageni Nkoma (75), Mama wa familia Maleciana Ludewa (57) na Mtoto Kelvin Shadrack mwenye umri wa mwaka mmoja.
Screenshot_20220819-041641_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra), imesema kuanzia Septemba 1, 2022, mabasi yanayofanya safari za mikoani na nchi za nje yasiyotumia tiketi za mtandao hayaturusiwa kufanya shughuli za usafirishaji wa abiria.

Kauli hiyo imetolewa leo Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maendeleo ya mchakato wa matumizi ya tiketi mtandao kwa mabasi yanayoendea katika mikoa mbalimbali na nchi za jirani.
Screenshot_20220819-041805_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi alipokua akitambulishwa kwa viongozi mbalimbali wa DRC alipowasili katika Ikulu ya Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja leo Alhamisi Agosti 18, 2022.
Screenshot_20220819-041913_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom