Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Ninachowaomba mashabiki wote wa Real Madrid wampe muda Luka Modric, ni mchezaji mzuri sana na naamini watampenda sana”

- Jose Mourinho alisema haya 2012 wakati huo ni Kocha wa Real Madrid
Screenshot_20220819-050115_OGInsta%2B.jpg
 
Aliikataa Bayern Munich, aliikata Real Madrid, aliikataa Juventus na bado akaikataa Barcelona

Anaitwa Marco Reus, nahodha wa kweli na mchezaji mwandamizi wa Borrusia Dortmund
Screenshot_20220819-050556_OGInsta%2B.jpg
 
| VICTOR AKPAN UPDATES

- Ukweli ni kuwa Kocha wa Simba na bench zima la ufundi halijaridhishwa na ubora wa Kiungo Victor Akpan na wanaamini kuwa hawezi kuipa timu kitu cha ziada tangu acheze Misri kwenye pre season

- Kocha anasema anahitaji typical holding Midfielder na sio box to box kama Victor Akpan, kwenye role hiyo wanaamini Sadio Kanoute anatosha sana kuliko yeye

- Taarifa za kuaminika ni kuwa Kocha hakuridhishwa pia na uwezo wa Moses Phiri akisema wazi kuwa hafit kwenye kile ambacho yeye anakifikiria kwenye falsafa yake

- Agency ya Akpan tayari imejulishwa kuhusu jambo hilo na wameambiwa waanze kutafuta timu ya mchezaji wao eidha kwa mkopo au kuuzwa jumla, Simba hawana tatizo kwenye hilo

- Simba wameagizwa na Kocha kurudi tena sokoni na kusaka Kiungo mkabaji ambaye atakidhi vigezo vya Mwalimu na matakwa ya kimfumo.

- Kilichosalia ni agency kuchakata jambo hilo huku Simba ikisemekana kwa taarifa zisizo rasmi wametua Nigeria kusaka saini ya Kiungo mkabaji

Screenshot_20220819-051117_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Ile ngoma ya SUKARI binafsi naamini ni Pepo ya Zuchu na ni Jehanamu ya Zuchu, ni ngoma iliyompandisha kwenye chart nchini na ni lazima ipatikane SUKARI nyingine kuendelea kwenda juu

Nandy alivaa crown kutokana na hit juu ya hit yani ikitoka hii inakuja hit nyingine, bado naona Zuchu hajatoa ngoma nyingine ya kuifikia Sukari, bado sukari inamdai sana, kipaji chake ni kikubwa sana ila imezidiwa nguvu na SUKARI ile

Sijajua kama mikono ya Producer Trone pale Pluto inafikiria kama ninavyofikiria Mimi? Ila naamini Trone anafahamu kuwa kwa Zuchu bado hajampa mdundo mwingine kama ule wa sukari, anahisi vidole vinamsaliti huenda

Sijajua Zuchu anafikiria kama Mimi ila naamini nae atakubaliana na mimi kuwa mikono yake bado haijaandika sukari nyingine, ulimi wake na lips zake bado haujatupa sukari nyingine, labda kalamu yake imepotea, itafute tena

Zuchu wale Dada zako kuanzia wakina Lady Jay Dee, Nandy, Ruby wakina Mwasiti walitupa hits after hits, unahitaji sukari nyingine kama tatu kwenye stoo yako kama sio nne, fanya hivyo

Bi Mkubwa wako Bi. Khadija Kopa, tangu Cultural Music Club pale Unguja mpaka TOT, mpaka kushea majukwaa na Mafundi kama Leila Khatib, Mwanamtama Amir na wakina Abdul Misambano, ilikuwa ngoma after ngoma, fuata nyayo

Bado hujatupa SUKARI nyingine, kila nikisikiliza nyimbo zako nikiweka sukari nitairudia mara nne mpaka tano, pambana utupe Sukari nyingine, una uwezo leta sukari! Upo top three ya Wasanii bora wa kike nchini, leta sukari tena

Kila la kheri Bint wa Malkia Kopa, mitaa bado inakudai SUKARI

Screenshot_20220819-051233_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Nimeamka leo asubuhi na mapema sana, napokea simu kutoka Bibi zangu huko nyumbani Morogoro, wanasema usiku wa jana hawajalala wanasikia vishindo kutoka milima ya Uluguru, vishindo tena vikubwa

Wananiambia Machifu wameumia, Machifu wanaumizwa na kitukuu chao Tepsie Evance, Mababu na Mababu wanasema hapati kile anachostahili, licha ya kuufanya mpira uwe mchezo rahisi sana ila bado hapewi heshima

Napokea simu kutoka kwa Wazee wa mila kutoka Mto Kilombero na Ruaha wanasema jana usiku maji yalikauka yote mtoni, haiwezekani Tepsie amefunga na kuassist na kwenye kiwango bora sana ila Farhan hujaandika kitu, wamechukizwa

Sauti kutoka mto Kilombero zinasema “Mwambieni Farhan aandike kuhusu Tepsie, aandike ili Mdogo wake asijisikie mnyonge, mwambieni aandike kwakuwa sisi ndio tunampa huo utashi” Naam! @tepsie_59 asubuhi hii nakuandikia Fundi

Nitaandika sana bila kuchoka ila Mambuyi wa Wapogoro kule Epanko, Mbangayao na kilele cha mlima Ndororo wasichukie, nitaandika kuhusu Mchawi huyu wa soka kutoka Morogoro, nitaandika bila kuchoka

Ghafla napokea simu kutoka safu za milima ya Udzungwa naambiwa maporomoko ya Sanje jana yalikauka, naambiwa chura wa Kihansi pale Mlimba walipotea, ni adhabu tumepigwa kwakuwa sijaandika kuhusu Tepsie

Nawaahidi Mababu zangu na Bibi zangu hapo Morogoro kuanzia Mbuga, Ulanga mpaka Kinole Morogoro! Nitaandika na sitoacha, Tepsie atarudi nyumbani kama Legend siku moja na mimi nitarudi nyumbani kama Ngugi siku moja ni ahadi

Babu na Bibi zangu msishushe laana kwenye kizazi hiki, tuendelee kuwapa pongezi @morokidsacademy @mtibwaofficial @moroathleticsacademy na Kilombero Soccernet, baraka na neema ziendelee

Fundi sana anaitwa TEPSIE EXCELLENCE oooh sorry! TEPSIE EVANCE All the best Homeboy @tepsie_59

Screenshot_20220819-051352_OGInsta%2B.jpg
 
Juma Ayo

MAONI HURU:

Nimeona taarifa za kocha wa simba kupendekeza baadhi ya wachezaji waondolewe kwa mkopo ,sidhani kama ni tatizo kiufundi kwasababu kocha ndiye anaona na kutathmini performance ya wachezaji katika mazoezi,.

Lakini katika management ya simba hii haiko sawa ,inaonesha klabu haina watu wa ufundi ambao walifanya recommendations na scouting ya wachezaji wazuri wanaoendana na ukubwa wa simba..haiwezekani kocha aanze kuwakata wachezaji mapema hata ligi haijafikia raundi ya pili na wengine hawajacheza kabisa ,maan yake viongozi walisajili wachezaji ambao average na inawezekana kocha kawaona watamfukuzisha kazi mapema inabidi awatoe kwa mkopo.

Kwa mtazamo wangu viongozi wabadilike na Kuna haja ya klabu kuwa n mkurugenzi wa ufundi na pia kwa ukubwa na uwekezaji wa simba ni muhimu kuwa na scouts au agencies mbalimbali kuwasaidia kuwatafutia wachezaji wazuri..kocha amewaprove wrong viongozi mpaka hapo ,ni makosa makubwa pia na kuwadhalilisha wachezaji, maana hata psychologia yao walishajua wanakwenda kuchezea simba ,mara kesho wanaambiwa waondoke wanaenda timu fulani kwa mkopo...

Leo tunasikia Dilunga anarudi wakati mwanzo Kuna kauli za viongoz vilisikika kuachana nae je kama ni kocha kasema maana yake no breakdown ya communication kutoka benchi la ufundi kwenda kwa management.

NB: KUNA WACHAMBUZI WALIONESHA DOUBT TANGU AWALI NA WACHEZAJI HAO HAO AMBAO LEO KOCHA ANAWAPENDEKEZA WATOLEWE KWA MKOPO NA MIMI NIKIWEMO.
Screenshot_20220819-051625_OGInsta%2B.jpg
 
Nassor Kapama hayupo kwenye mipango ya kocha aomba atolewe kwa mkopo
Geita wapo tayari kumchukua kwa mkopo

Bongo mambo ni mengi muda mchache

Ihefu na Singida Big star wametuma ofa kwa Bocco
Screenshot_20220819-051741_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom