Imeandikwa na @swalehmawele
FT: Simba SC 3-0 Geita Gold

Bila shaka ni ushindi muhimu sana kwa Simba ili kujenga saikolojia ya ushindi katika akili za wachezaji, leo substitution moja ya kocha Zoran Maki ilikuja kubadilisha taswira ya uchezaji kwa Simba katika eneo la mwisho na kuanzia hapo mambo yakaanza kuwa mazuri upande wao, kivipi?.

Simba ilitengeneza shape ya 4-1-3-2 wakati ambao wanatengeneza mashambulizi, kocha alianza na Jonas Mkude kama kiungo wa kati mshambuliaji mbele ya Sadio Kanoute, Mkude alisogea katika mstari wa viungo watatu katikati ya Pape Sakho na Peter Banda na kuifanya timu iwe na 3-2 katika eneo ambalo Geita Gold wanazuia zaidi.

Hapa lengo lilikuwa ni kuifanya timu iwe na wachezaji wengi ambao wana akili ya kushambulia zaidi ( creating overloads with offensive minded players ), ni kama walitaka kuizunguka safu ya ulinzi ya Geita Gold kwa kuwa na wachezaji wawili nyuma yao ( Chama & Phiri ) na kuwa na wachezaji watatu mbele yao ( Mkude, Banda & Sakho ).

Wapi Simba ilifeli? ni katika usahihi wa Jonas Mkude katika kupiga pasi, pasi nyingi za Mkude zilikuwa ni square, hakuwa na ujasiri wa kupiga pasi ambazo zingeifunga difense line ya Geita Gold kutokea chini ( penetration passes ) na pia hakukuwa na mikimbio sahihi ambayo ingeitanua safu ya ulinzi ya Geita Gold ambayo ilikaba katika low block.

Geita Gold wamepoteza mechi ambayo walionyesha ujasiri na usahihi katika transitions zao, katika system ya 4-4-2, waliuharakisha mpira kupita kwenye eneo la kiungo ( midfield zone ) ili kuzikwepa pressing na 1 v 1 kwa wachezaji wa Simba, walifanikiwa lakini tatizo likawa katika ujasiri wa kuifunga back line ya Simba chini ya kamanda Mohammed Ouattara.

Nikivaa viatu vya Dejan naiona presha kubwa, kuna kitu anataka kitokee lakini mara nyingi hapokei pasi sahihi, eneo la ushambuliaji utaulizwa kuhusu magoli.

Kuna maswali magumu kama Zoran ataendelea kutumia double ten ya Chama na Okrah, Chama anatuliza timu na Okrah anaifanya ikimbie, kuna aina mbili hapo za kutengeneza mashambulizi.

Yule Yusuph Kagoma mtu, Yahya Mbegu kama juzi kama jana.

Nafikiri Geita Gold hawakucheza vibaya sana, kilichokuja kuamua ni quality.