Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini Kenya (EPRA) imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa Ksh. 9 (Tsh. 178.47) katika ukaguzi wake wa kila mwezi.

Kwa muda wa mwezi mmoja ujao lita moja ya petroli jijini Nairobi itagharimu Ksh.159.12 ( Tsh. 3,160.70), dizeli Ksh. 140 (Tsh 2,785.65) na mafuta ya taa Ksh. 127.94 (Tsh. 2,541.35).

EPRA imesema Serikali itatumia Hazina ya Maendeleo ya Petroli (PDL) kuwaepusha watumiaji kutokana na bei hizo za juu ambapo badala ya Watumiaji kulipia gharama yote husika, Serikali italipa sehemu ya ongezeko kupitia ruzuku.

Kwa sasa Madereva wa Nairobi wanalipa Ksh. 159.12 (Tsh 3,160.70) kwa lita moja ya petroli lakini walipaswa kulipa Ksh.184.68 (Tsh.3,668.41) na imepungua kutokana na Serikali kuwasaidia kulipa Ksh.25.76 (Tsh. 511.69) kupitia ruzuku, kwa upande wa diesel Serikali inalipia Ksh. 48.19 (Tsh. 957.23)
kwa lita kupitia ruzuku na mafuta ya taa ruzuku inayolipwa na Serikali ni Ksh. 42.43 (Tsh.957.23) kwa lita na kwamba bei hizi zinajumuisha kodi na zimerekebishwa ili ziendane na mfumuko wa bei.
Screenshot_20220615-161140_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema shirika la ndege la Uturuki litabadilisha jina lake na kuwa "Türkiye Hava Yolları" badala ya "Turkish Airlines" kama sehemu ya kushinikiza nchi yake ijulikane kimataifa kama "Türkiye" badala ya ‘Turkey’.

Mapema mwezi huu Nchi hii ilituma barua kwa Umoja wa Mataifa ikisajili rasmi jina la nchi hiyo kama ‘Türkiye’ ikisema jina hili jipya linawakilisha vyema utamaduni na maadili ya Kituruki huku baadhi ya Wachunguzi wa mambo wakisema hatua hii ni sehemu ya juhudi za kulitenganisha jina lake na jina la bata mzinga ambaye ni ‘Turkey’ kwa kiingereza.

"Turkiye haipo tena, sasa ni Türkiye” ambapo maneno ‘Türkiye Hava Yolları’ yataandikwa kwenye ndege zetu zote badala ya Turkish Airlines, "Hava Yolları" inamaanisha mashirika ya ndege kwa Kituruki.

Umoja wa Mataifa na NATO wameanza rasmi kutumia "Türkiye" badala ya "Uturuki." Baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa kigeni wanaotembelea Ankara pia wamebadilisha jina hilo.
Screenshot_20220615-161255_OGInsta%2B.jpg
 
Beki wa Liverpool na Timu ya Taifa ya Ufaransa Ibrahima Konaté amewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutalii.

Konaté anakuwa staa mwingine wa soka kuitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miezi miwili huku mwingine akiwa ni Ander Herrera wa PSG.
Screenshot_20220615-161355_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) kwa kila Mtanzania atayefikisha umri wa miaka kumi na nane kwani atatakiwa kuanza kulipa kodi katika umri huo.

Dr. Mwigulu ameyasema haya jana wakati akiwasilisha Bungeni Dodoma mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/2023 huku akinukuliwa akisema "Kila Mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi ambapo ili kutimiza amza hiyo Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi"

"Kwakuwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unamtaka kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 au zaidi kujisajili NIDA, napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi ambapo kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao"
Screenshot_20220615-161745_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jana tarehe 14/6/2022 imekamata marobota ya vitenge 507 yaliyoingizwa nchini kinyume cha sheria.

Taarifa ya TRA imesema Marobota hayo yameingizwa nchini na Mfanyabiashara Raia wa China kwa njia za magendo kupitia Kampuni yake inayoitwa Kapansky na kuhifadhi mzigo huo kwenye ghala la Kampuni ya Shinyanga Emporium lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam bila kuwa na nyaraka zozote za forodha.
Screenshot_20220615-161853_OGInsta%2B.jpg
 
"Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa
Heading 6704"

"Hatua hii inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali" ——— Dr. Mwigulu

hata mkiweka 100% tutanunua tu
Screenshot_20220615-162209_OGInsta%2B.jpg
 
Zaidi ya wananchi 290 katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wamejiandikisha kuhama katika makazi hayo na kwenda Kijiji cha Msomera mkoani Tanga.

Akizungumza na wafugaji hao, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema kaya 296 zimeshajiandikisha ili kuondoka katika eneo hilo
Screenshot_20220615-162830_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali ya Rwanda imesema bado haijakata tamaa licha ya Uingereza kusitisha safari ya ndege ya kwanza ya waomba hifadhi kutoka nchini humo.

Safari hiyo iliyokuwa imepangwa kufanyika baada ya Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya kusema mpango huo unaakisi athari zisizoweza kurekebishwa.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo amesema "Hatukatishwi tamaa na yaliojiri, Rwanda itaendelea kujitolea kikamilifu kufanya ushirikiano huu ufanye kazi.
Screenshot_20220615-163000_OGInsta%2B.jpg
 
Urusi imewapiga marufuku kuingia nchini humo raia 49 wa Uingereza wakiwemo maafisa wa ulinzi, waandishi wa habari mashuhuri na wahariri kutoka Shirika la Habari la BBC, The Financial Times na The Guardian.

Taarifa ya wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imedai waandishi wa habari wa Uingereza wamejihusisha kwa makusudi kusambaza taarifa za uwongo na za upande mmoja kuhusu Urusi, matukio ya Ukraine na Donbass.

Miongoni mwa waandishi wa habari waliopigwa marufuku ni pamoja na Shaun Walker wa The Guardian, Gideon Rachman wa The Financial Times na mwanaharakati Mark Galeotti.
Screenshot_20220615-163133_OGInsta%2B.jpg
 
Kampuni ya Microsoft leo Juni 15, 2022 inaachana rasmi na usimamizi wa wavuti ya Internet Explorer ambayo ilikuwa maarufu kipindi cha miaka ya nyuma.

Internet Explorer ilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1995 kama sehemu ya kifurushi cha nyongeza cha Windows 95.

Kuanzia 1995 hadi 2013, kampuni hiyo ilitoa matoleo 11 ya programu yake ya wavuti ambapo ilikuwa ni miongoni mwa wavuti za awali kutengenezwa duniani.

Toleo lake la mwisho lilikuwa Internet Explorer 11 iliyotolewa 2013 kabla ya kubadilishwa na Microsoft Edge
Screenshot_20220615-163231_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na msanii nguli wa filamu wa Nigeria, Jim Lyke.

Katika mazungumzo yao, waziri ameeleza kuwa Serikali imeshusha kodi ya zuio katika biashara ya filamu kutoka asilimia 15 hadi 10 ili kutoa unafuu kwa kampuni zinazofanya masuala ya filamu nchini.
Screenshot_20220615-163336_OGInsta%2B.jpg
 
Katika mkakati wa kubana matumizi, Serikali inatarajia kudhibiti mambo kadhaa ikiwemo ununuzi na matumizi ya magari.

Hayo amebainisha jana Jumanne Juni 14, 2022 bungeni mjini Dodoma wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.

Katika hotuba yake hiyo, Dk Mwigulu amesema watadhibiti matumizi hayo kwa kuzingatia waraka wa rais namba moja wa mwaka 1998 kuhusu hatua za kubana matumizi ya serikali na waraka wa mkuu wa utumishi wa umma namba mbili wa mwaka 2021 kuhusu utaratibu wa kutumia usafiri huo.

“Baadhi ya maeneo yenye gharama kubwa sana kwa serikali ni ununuzi wa magari, mafuta ya uendeshaji, vipuri na matengenezo,” amesema.
Screenshot_20220615-163440_OGInsta%2B.jpg
 
: VILABU BORA 20 AFRIKA

1. Al Ahly
2. Wydad AC
3. ES Tunis
4. Raja CA
5. RS Berkanè
6. Mamelodi Sundowns
7. TP Mazembe
8. Zamalek SC
9. Pyramids
10. Sahel Star
11. Orlando Pirates
12. Horoya AC
13. Petro Luanda
14. SIMBA SC
15. ES Sétif
16. CR Belouizdad
17. JS Kabylie
18. Kaizer Chiefs
19. Al Hilal
20. Al Masry
Screenshot_20220615-164748_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom