Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Shirikisho la soka Cameroon, Samuel Eto’o anatarajiwa kushiriki mkutano wa soka utakaofanyika Juni 24-25 huko visiwani Zanzibar.

Eto’o ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika mara nne, amewahi kuchezea vilabu vikubwa vya soka kama Barcelona, Mallorca, Inter Milan, Chelsea na vinginevyo.

Mkutano huo ulioandaliwa na AfriSoccer unatarajiwa kuhudhuriwa na watu maarufu wa soka kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Screenshot_20220615-173855_OGInsta%2B.jpg
 
WAKATI Yanga kwenye suala la usajili ni bandika bandua kutokana na namna wanavyofanya usajili wao kuelekea msimu wa 2022/23, lakini kama unadhani Simba wamepoa unajidanganya.
Unataka kufahamu kwa upande wa mabingwa watetezi mpango wao upoje? Iko hivi, Simba ambao wanapambana kusaka kocha mpya kwa ajili ya kuziba pengo la Pablo Franco wanafanya usajili wao kimyakimya na tayari straika wa mabao wa Geita Gold, George Mpole amemwaga wino Msimbazi.

“Mpole alipokuwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ mara baada ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Algeria ambao Tanzania ilikubali kichapo cha mabao 2-0 mchezaji huyo alibebwa moja kwa moja na kupelekwa moja ya hotel iliyopo katikati ya mji (Dar) ili kufanya naye mazungumzo,” kilisema chanzo hicho.

“Mchezaji huyo kakaa kwenye hoteli siku tatu malipo yakiwa chini ya Simba kwa ajili ya mazungumzo hadi anaondoka kuuwahi mchezo na Dodoma Jiji leo (jana) huku mazungumzo yakiwa ni asilimia 80 mchezaji huyo kamalizana na timu hiyo.” kiilisema chanzo cha kuaminika.
Screenshot_20220615-180704_OGInsta%2B.jpg
 
TETESI UPDATE.

Panga la Mo dewji linakuja baada ya dirisha kufunguliwa
Wachezaji wanaotajwa kufyekwa ni pamoja Peter Banda.
Wengine ambao pengine wakakumbwa na fagio ni
-John Bocco
-Erasto Nyoni
-Mugalu na Mkude

Inaelezwa wengine wanatumika na wengine viwango vimeshuka
Usajili wa chini chini unaendelea msimbazi
Screenshot_20220615-180918_OGInsta%2B.jpg
 
YANGA imekamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Asec Mimosas, Stephano Ki Aziz wakati huo huo taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza imekamilisha usajili wa Benard Morrison kutoka Simba.

Morrison atachelewa kutambulishwa kutokana na mkataba wake na Simba kumalizika Agosti 30, mwaka huu, siku chache kabla ya msimu ujao kuanza wakati huo hadi mechi ya Ngao ya Hisani itakuwa imechezwa.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza Morrison ametuma maombi kwa njia mbalimbali, ujumbe mfupi wa maneno wa simu, barua pepe, kupiga simu na kuzungumza na viongozi wa juu ili wampe barua inayoonyesha yupo huru.

Morrison amewaomba mabosi wake ambao hivi karibuni walimtakia kila la heri kwenda kutatua matatizo ya kifamilia kumpatia barua hiyo akieleza kwamba kuna timu kutoka nchi mbalimbali zinamtaka.
Screenshot_20220615-191919_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Warren Mwinuka (20) Mkazi wa Mtaa wa Makondeko jijini Mbeya kwa tuhuma za kujifanya ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Juma Homera ) na kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la Mkuu huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema Mtuhumiwa huo alikamatwa Juni 7 majira ya saa nane mchana katika maeneo ya Mama John jijini Mbeya alipokuwa akiendelea kuwatapeli Watu.

Mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwahadaa Watu kwa kujifanya ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu yake ili Wananchi waweze kutoa na kumfikishia kero au shida mbalimbali na alitumia fursa hiyo kutapeli.

Kwa upande wake Mtuhumiwa amejitetea kuwa sababu ambayo ilimpelekea hadi kufanya hivyo ni kwakuwa anampenda sana Mkuu wa Mkoa huyo lakini Polisi wamesema upelelezi wa shauri hilo unaendelea na ukikamilika Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.
Screenshot_20220615-193538_OGInsta%2B.jpg
 
Mtoto wa miaka miwili(2) Nkiya Thomas, Mkazi wa Kijiji cha Nyamigogwa Kata ya Shabaka Wilaya ya Nyang'hwale, Mkoa wa Geita, amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa na Watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kwenye shamba ambalo lipo mkabala na nyumba yao.

Jamhuri David ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuagiza uchunguzi wa tukio hili ufanyike haraka "Hatuwezi kukubali Wilaya yetu kuwa na matukio ya namna hii , kwa upande wangu nimesikitishwa sana na tukio hili niombe tushirikiane kutokomeza haya matukio"

Kwa upande wake Mama Mzazi wa Mtoto aitwaye Mperwa Sahani amesema "Taarifa ya kifo cha Mtoto wangu nilipewa na Mtoto wa Shemeji yangu kuwa Nkiya amefariki wamemuona shambani amechinjwa nilipofika kweli nilikuta Mtoto wangu amechinjwa"
Screenshot_20220615-193723_OGInsta%2B.jpg
 
Basi la Zuberi lililokuwa limebea abiria likifanya safari yake kati ya Mwanza na Kahama limepata ajali leo June 15 kwenye eneo la Mwigumbi mkoani Shinyanga na inahofiwa kuna Watu waliopoteza maisha.

Mashuhuda kwenye eneo la tukio wamesema ajali hiyo imetokea leo saa tisa alasiri baada ya basi hilo kuacha njia eneo ambalo kuna daraja na kupinduka, @AyoTV_ inaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa ufafanuzi zaidi.
Screenshot_20220615-193844_OGInsta%2B.jpg
 
Leo tarehe 15/6/2022 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewafikisha Watuhumiwa wawili Raia wa China Zhu Wei na Tao Pan katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa makosa ya kukutwa na bidhaa ambazo hazijafuata taratibu za forodha, kukwepa kodi na uhujumu uchumi.

Mashtaka hayo yamesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Rita Tarimo ambaye ameiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 29/6/2022.
Screenshot_20220615-193943_OGInsta%2B.jpg
 
Mtoto wa miaka miwili(2) Nkiya Thomas, Mkazi wa Kijiji cha Nyamigogwa Kata ya Shabaka Wilaya ya Nyang'hwale, Mkoa wa Geita, amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa na Watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kwenye shamba ambalo lipo mkabala na nyumba yao.

Jamhuri David ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuagiza uchunguzi wa tukio hili ufanyike haraka "Hatuwezi kukubali Wilaya yetu kuwa na matukio ya namna hii , kwa upande wangu nimesikitishwa sana na tukio hili niombe tushirikiane kutokomeza haya matukio"

Kwa upande wake Mama Mzazi wa Mtoto aitwaye Mperwa Sahani amesema "Taarifa ya kifo cha Mtoto wangu nilipewa na Mtoto wa Shemeji yangu kuwa Nkiya amefariki wamemuona shambani amechinjwa nilipofika kweli nilikuta Mtoto wangu amechinjwa"View attachment 2261986
Huu ukanda unahitaji maombi maalumu.
 
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Warren Mwinuka (20) Mkazi wa Mtaa wa Makondeko jijini Mbeya kwa tuhuma za kujifanya ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Juma Homera ) na kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la Mkuu huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema Mtuhumiwa huo alikamatwa Juni 7 majira ya saa nane mchana katika maeneo ya Mama John jijini Mbeya alipokuwa akiendelea kuwatapeli Watu.

Mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwahadaa Watu kwa kujifanya ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu yake ili Wananchi waweze kutoa na kumfikishia kero au shida mbalimbali na alitumia fursa hiyo kutapeli.

Kwa upande wake Mtuhumiwa amejitetea kuwa sababu ambayo ilimpelekea hadi kufanya hivyo ni kwakuwa anampenda sana Mkuu wa Mkoa huyo lakini Polisi wamesema upelelezi wa shauri hilo unaendelea na ukikamilika Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani. View attachment 2261984

Hii nchi kila mtu mpigaji, ni vile akina Shunie hawajapata nafasi ya kupiga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom