Makapuku Forum

Makapuku Forum

Pata picha kwa miaka 17 Mama huyu Semeni Selemani hajaonana na Mtoto wake na amekua akimtafuta kila Kona bila mafanikio lakini leo amekutanishwa nae kupitia kipindi cha Redio cha LEO TENA Clouds FM

Semeni Selemani ambaye ni Mkazi wa Tabata DSM amesema alikua akiwatafuta Watoto wake wawili ambao walimpotezana kwa nyakati mbili tofauti ambapo wa kwanza ni huyu Mwita.

“Kutokana na ugumu wa maisha hatukuwa tunaishi pamoja na Baba yao, mimi nilikua naishi kwa Mama na yeye alikua anaishi kwa kaka yake, Baba yao alikuja na kusema anamuomba Mwita aende kupanda msalaba kwenye kaburi la Babu yake, baadae Baba yao akaja tena kumchukua Mtoto wa pili mimi sikuwepo nyumbani"

"Ikabidi niende Ilala alikokuwa anaishi Baba Mwita nilipofika wakaniambia Baba Mwita haishi tena hapa maisha ya mjini yamemshinda ameuza vyombo na kurudi Musoma, Watoto wote walitoroshwa kwangu na Baba yao wakiwa wadogo na sikuwaona toka hapo ndio juzi Mama yangu akaniambia huu ni mwaka wa mwisho lazima Watoto wangu niwaone twende CLOUDS kwenye kipindi cha LEO TENA ambacho huwakutanisha Wazazi na Watoto wao na leo ndio tumekutanishwa”

Mtoto wa pili wa Semeni aitwae Ngai ameshindwa kuja kuonana leo na Mama yake kutokana na mitihani aliyonayo shuleni ila Baba yao aitwae Adam pamoja na Mwita walifika CloudsFM leo na kukutana na Semeni baada ya miaka hiyo 17 ya kutoonana wala kuwasiliana.
Screenshot_20220615-160812_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga ameanzisha kampeni ya Kila Kijiji kuhakikisha inajenga zahanati kwa kutumia nguvu kazi ambapo ameipa jina la Jenga Zahanati na Kuku.

DC Mwanga amesema baada ya kutembelea Vijiji vingi vya Tarafa ya Magole amebaini kuwa na changamoto ya kukosa vituo vya kutolea Huduma za afya hivyo kamepeni hiyo itasaidia kupunguza changamoto hiyo.

Anasema Wananchi wanaoishi vijijini wengi hawana uwezo wa kiuchumi lakini wanafuga mifugo mingi ikiwemo kuku hivyo kila Mwananchi akitoa kuku mmoja au mayai 20 yataweza kufanikisha kukamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati.

DC Kilosa yupo katika ziara ya kikazi Tarafa ya Magole kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kwenye vijiji vyote ili kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Screenshot_20220615-161045_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom