Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kiwanda cha kwanza barani Afrika cha kuzalisha na kusambaza chanjo za Corona kilichozinduliwa 2021, kiko hatarini kufungwa baada ya kutopokea hata oda moja ya chanjo, amesema Afisa Mkuu wa kampuni hiyo.

Kampuni ya Aspen Pharmacare (APNJ.J) ya Afrika Kusini ilijadili mkataba wa kutoa leseni Novemba 2021 ili kuuza chanjo ya Johnson & Johnson (JNJ.N) ya COVID-19 na kuisambaza kote Afrika.

Huku ikiwa ni 1 ya sita tu ya Watu wazima barani Afrika waliopokea dozi kamili ya chanjo ya Corona kulingana na takwimu za hivi punde za WHO, makubaliano ya Aspen ya kuuza chanjo ya Aspen ya COVID-19, Aspenovax, barani Afrika yalionekana kuwa na ‘soko’ la uhakika lakini sasa imekua ndivyo sivyo.

"Hatujapokea oda ya chanjo za Aspenovax, kwa sababu hatujapata oda yoyote ya chanjo basi ni wazi kutakuwa na sababu ndogo sana za kubakiza njia ambazo tunatumia kwa uzalishaji” Mkurugenzi Mkuu wa Aspen Stavros Nicolaou ameliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu.

Lengo la Umoja wa Afrika ni kuzalisha asilimia 60 ya chanjo zote zinazotolewa barani Afŕika ifikapo mwaka 2040 kutoka asilimia 1 ya sasa, na mitambo kadhaa ya aina hiyo inaanzishwa.
Screenshot_20220503-042939_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov amesema Urusi haitegemei kukamilisha operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine May 9, katika maadhimisho ya sherehe zake tangu kutangazwa kwa taifa huru mnamo Mei 9, 1991.

Lavrov amesema Urusi haitaharakisha kukamilisha kile kinachojulikana kama Operesheni Maalum ya kijeshi nchini Ukraine wakati wa maadhimisho ya uhuru wa Urusi.

“Jeshi letu halitasitisha shughuli zake kwa tarehe yoyote ile, hata katika siku yetu ya maadhimisho ya Uhuru wa Urusi, zaidi tutasherehekea kwa dhati Mei 9 kama tunavyofanya kila wakati kukumbuka wale wote walijitoa kwa ajili ya ukombozi wa Urusi na Jamuhuri nyingine za USSR ya zamani kwa ukombozi wa Ulaya"
Screenshot_20220503-043103_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema imeona mjadala wa malalamiko kutoka kwa Wadau Mtandaoni kuhusu watoa huduma kubadili bei za vifurushi kimyakimya ambapo TCRA imesema endapo kuna Mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane na Mamlaka hiyo.

"TCRA imeona mjadala wa malalamiko kutoka kwa Wadau Mtandaoni kuhusu watoa huduma kubadili bei za vifurushi kimyakimya, Mamlaka ingependa kuwajulisha kuwa endapo kuna mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane nasi kupitia 0800008272"

"Pia unaweza kuwasiliana na Mamlaka kupitia baruapepe dawatilahuduma@tcra.go.tz, Mamlaka inafuatilia suala hili kwa watoa huduma ili kuweza kubaini ukweli"
Screenshot_20220503-043156_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220503-043209_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa kutoka Chama tawala cha Conservative nchini Uingereza Neil Parish amejiuzulu Ubunge wake baada ya kukiri kuwa alitazama video za ngono kwenye simu yake ya mkononi akiwa Bungeni kwa nyakati mbili tofauti.

Mbunge huyo ambaye amewakilisha majimbo ya Tiverton na Honiton huko Devon tangu 2010, amesema mara ya kwanza ilikuwa bahati mbaya baada ya kuangalia tovuti ya trekta kisha akakutana na video za ngono lakini mara ya pili katika Baraza la Common ilikuwa ya makusudi na anajutia ambapo tayari amesimamishwa kazi na Chama cha Conservative wiki iliyopita kutokana na madai hayo.

Wabunge wenzake wawili wa kike walidai kuwa walimwona akiangalia video za ngono ya kwenye simu yake akiwa karibu nao “nitaishi na hili maisha yangu yote, nilifanya kosa kubwa sana na niko hapa kuuambia ulimwengu, najutia"
Screenshot_20220503-043316_OGInsta%2B.jpg
 
Muhubiri maarufu kutoka Kisongo Arusha Dr. GeorDavie amesema Yesu Kristo alimtokea chumbani mwaka 2003 saa kumi na moja asubuhi ikiwa ni saa chache kabla hajaelekea kwenye mkutano wa injili alikotakiwa kuhubiri neno la Mungu ambapo alimkabidhi funguo ili azitumie kuwafungua Watu mbalimbali wenye matatizo.

"Yesu Kristo alinitokea mwenyewe kabisa, alinikabidhi funguo akaniambia hizi funguo size mbalimbali kawafungue Watu wangu na kesho yake nilikua nina mkutano, alinitokea kama saa kumi na moja asubuhi kwenye eneo hilo hapo juu (Kisongo) akaniambia nimekutuma kama Prophet (Nabii), nenda kawafungue Watu wangu" ———
Screenshot_20220503-043642_OGInsta%2B.jpg
 
Muhubiri maarufu Dr. GeorDavie ambaye Kanisa lake lipo Kisongo Arusha amesema ni kweli alitokewa na Yesu Kristo chumbani mwaka 2003 na alifanikiwa kumuona sura saa chache kabla ya kwenda kuhubiri kwenye mkutano wake wa kwanza wa Injili toka aanze huduma.

"Ile saa kumi na moja asubuhi nimeamka tu kwenye ukuta nikaona Mtu amesimama, nuru yake iliangaza chumba kizima.... sikuweza kumuona chini ila nilimuona kuanzia juu mpaka kiunoni ameshika kitita cha funguo anatikisa, akaniita jina langu"

Interview nzima ya Dr. GeorDavie ipo kwenye youtube ya millardayo au unaweza kubonyeza link yangu hapa instagram ikupeleke kumtazama moja kwa moja.
Screenshot_20220503-043758_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji ya mwalimu wa Sekondari Bwiru, Ambrose Mapembegashi.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, Kamanda wa Polisi Ramadhani Ng'anzi amesema katika tukio hilo lililotokea Aprili 29, 2022 watuhumiwa walivamia nyumbani kwa marehemu na kumjeruhi na kitu chenye ncha kali katika kichwa na shingo kisha kuiba baadhi ya mali zake ikiwemo TV aina ya Itel, Redio aina ya Sapeano na Pasi aina ya Africab.
Screenshot_20220503-044140_OGInsta%2B.jpg
 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia Shule Kuu ya Madini na Jiosayansi kimefanya tafiti na kubaini matumizi ya gesi kwenye magari yanapunguza asilimia 60 ya gharama.

Mhadhiri msaidizi wa chuo hicho, Athuman Mkilindi alisema kubadili mfumo wa magari kutoka kutumia mafuta ya petroli na kutumia gesi asilia kuna unafuu mkubwa na imekuwa na faida kubwa kupitia tafiti yao.

"Tulifanya utafiti kwenye gari yenye injini ndogo (Cc) ya 1,500 kwa gesi kilometa moja utatumia Sh77.5 ukiwa unaendesha na umewasha kila kitu kwenye gari mfano kiyoyozi na petroli kwenye kilometa moja unatumia Sh211 hapo utaona unaokoa Sh134," alisema Mkilindi
Screenshot_20220503-044627_OGInsta%2B.jpg
 
Idara ya Uhamiaji mkoani Mwanza inawashikilia raia 68 wa Ethiopia kwa makosa ya kuingia nchini kinyume na utaratibu.

Akitoa taarifa leo Meib2,2022 kwa waandishi wa habari, Kamishna wa Uhamiaji mkoa wa Mwanza, Peter Mbaku amesema wahamiaji hao walikamatwa Aprili 29 mwaka huu katika kijiji cha Sanjo kata ya Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Mbaku alisema wahamiaji hao walikamatiwa ndani ya nyumba ya mkazi wa kijiji hicho huku wakisaidiwa kupita nchini kuelekea nchini Afrika Kusini na mwanamke.
Screenshot_20220503-044730_OGInsta%2B.jpg
 
Maafisa wa afya nchini Kenya wameanza kuchukua hatua katika mipaka ya nchi hiyo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Mwanasayansi mbobezi wa utafiti na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Virusi katika Taasisi ya Utafiti wa Matibabu nchini Kenya (KEMRI), Dk Samoel Khamadi amesema hatua zote zimechukuliwa kwa ajili ya kugundua na kupambana na ugonjwa huo kwani maafisa wa wizara ya afya wanafuatilia kwa karibu watu wanaovuka mipakani hasa wale wanaotoka karibu na Kongo.

“Maafisa wetu wa afya katika sehemu zote za kuingilia wamepatiwa mafunzo ya namna ya kubaini watu wanaoweza kuwa na ugonjwa wa ebola, endapo kutakuwepo na mtu anayehisiwa atawekwa karantini na ikibidi sampuli zitachukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika maabara zetu,” amesema Dk Khamadi.

Kuibuka tena kwa virusi hivyo katika mji wa Mbandaka, kaskazini magharibi mwa DRC, kumesababisha vifo vya watu wawili tangu Aprili 21, 2022

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa hadi kufikia Aprili 27, 2022 takribani watu 267 walikuwa wamegundulika kuwa na ugonjwa huo nchini Kongo
Screenshot_20220503-045001_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Simba imetozwa faini Sh1 milioni kwa kosa la mashabiki wake kumrushia mwamuzi wa mechi dhidi ya Coastal Union chupa baada ya Meddie Kagere kufunga bao. Mechi hiyo ilichezwa Aprili 7 na matokeo yaliisha 2-1
Screenshot_20220503-045158_OGInsta%2B.jpg
 
Yanga SC imetozwa faini ya Sh2 milioni na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa kosa la kupitia mlango usio rasmi katika mechi dhidi ya Azam FC iliyopigwa Aprili 6 na matokeo Yanga ilishinda 2-1.

Pia imetozwa faini Sh1 milioni kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa kwa mwamuzi wa mechi hiyo.
Screenshot_20220503-045249_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya kumalizana na Yanga kikosi cha Simba kimetua mkoani Mtwara kwa na kisha kuelekea mkoani Lindi kwa gari ambapo kesho Mei 3 watakuwa wageni wa Namungo FC katika uwanja wa Ilulu, Lindi mechi ya Ligi Kuu.

Screenshot_20220503-045402_OGInsta%2B.jpg
 
Tanzania kuna vipaji vingi vya soka lakini changamoto kubwa imekuwa ni kushindwa kutengeneza majukwaa ya kuweza kuvifanya vipaji hivi vionekane na hatimaye viwe uti wa mgongo wa taifa.Kimsingi vyama vya soka vya kitaifa,mkoa na wilaya vimeshindwa kutengeneza miradi bunifu(creative projects) kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya soka la vijana.

Viongozi wengi kwenye FA za mkoa na wilaya hawana maono(vision) kuhusu mchezo wa mpira wapo kwasababu za kisiasa,matakwa binafsi, na kadhalika.Aina hii ya viongozi tulionao wameshindwa kubuni miradi ya muda mfupi na muda mrefu(short t & long term projects) inayohusu maendeleo ya soka la vijana.

Shafih Dauda kupitia project yake ya Ndondo Cup ametoa somo kwa vyama vingi vya soka namna gani vijana wanaweza kutengenezewa mazingira mazuri ya kuonesha vipaji vyao na hatimaye kupata nafasi ya kucheza ligi kuu na timu ya taifa.Ukiangalia project ya Ndondo Cup imefanikiwa kuwasaidia vijana wengi kupata fursa za kucheza kwenye vilabu vya ligi kuu na hata timu ya taifa,Iddy Nado,Anual Jabiri,Kelvin Sabato na wengineo ni mfano wa matunda mazuri ya ndondo cup.

Vyama na wadau muhimu wa mpira wa miguu wanapaswa kuichukua project ya Ndondo Cup kama darasa huru,wanapaswa kumeza dawa chungu na kukubali ukweli kwamba wanaendesha soka kihisia sana kuliko kisayansi.

The Young Digala is here.

@omarrkombo
Screenshot_20220503-051117_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Natamani kuwaelewa mnaposema Clatous Chama sio Mchezaji wa mechi kubwa ila swaumu yangu itaonekana si kitu kama nikikubaliana na hilo

Nakubali vipi Mchezaji aliyewalaza Nkana Red Devils, akawaonjesha mpira AS Vita, akacheza kama hatocheza tena dhidi ya JS Saoura kisha miamba ya Afrika Al Ahly, nakubalije juu ya Mchezaji wa Chipolopolo

Natamani tena kuwaelewa kuwa Chama sio mchezaji wa mechi kubwa lakini aliondokaje huyu kwenda Berkane bila kuperform kwenye mechi kubwa za michuano ya Afrika?? Natamani kuwaelewa ila hapana

Natamani kuwaelewa kuwa Chama mnasema sio yule tena, lakini hapana! RS Berkane wakati Chama yupo fit kucheza walienjoy mpira wake mkubwa na kiwango chake kikubwa haikuwa rahisi kumruhusu aondoke

Nafahamu namna Berkane walisumbua, nafahamu namna gani Berkane walipambana ili Chama asalie kwenye timu, nafahamu kwanini Simba walikubali arejee licha ya kutocheza Shirikisho, ilikuwa mapambano ya zaidi ya miezi mitatu

Kuna wakati tusihukumu watu kisa derby! Maana tutahukumu wangapi? Tutakubaliana tukisema Feisal ni wa kawaida!? Kwakuwa hajashine kwenye derby!?? Tutasema Mayele ni wa kawaida kwakuwa derby mbili goaless?

Natamani sana kuwaelewa mnaposema Chama sio mzuri wakati timu inashambuliwa, lakini hapana! Niambieni kama kuna Mchezaji wa aina ya Chama (Ballers) ambao ni wazuri timu ikiwa haina mpira, jibu ni HAPANA

Natamani sana kukubaliana nanyi kuhusu Chama ila hapana, naomba niseme FORM IS TEMPORARY BUT CLASS IS PERMANENT

Nakubali kutokubaliana ni sahihi tu kutokubaliana, tukubali kutokubaliana
Screenshot_20220503-052042_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom