Makapuku Forum

Makapuku Forum

Farhan Jr

Kuna wakati ilionekana ngumu kusema upo timu gani kati ya miamba miwili, SIMBA na YANGA, binafsi sijawahi kuona ugumu kwakuwa huwezi kuchambua mpira bila kuwa Shabiki

Kama unapenda pepo usiogope kufa, huwezi kwenda Msikitini au Kanisani kusali kwa ajili ya kufika mbinguni, kama hautaki kufa

Sijawahi kupata tabu yoyote kwenye kazi yangu tangu nimeanza IRINGA as long as nasimama kwenye ukweli, Alhamdulillah nina Rafiki zangu wanacheza Yanga na Simba, nina Viongozi ambao ni Yanga ila ni watu wangu, haijawahi kuwa shida

Basi kwasasa kama FARHAN SHABIKI wa mpira, naitakia kheri timu yangu SIMBA, tushinde dhidi ya Yanga, tukose ubingwa sawa ila tuwalize leo, maana Ndugu zangu haswa Kaka na Dada zangu nyumbani wananitesa sana

Unaweza kujiuliza nawezaje kuchambua wakati chama limefungwa Guys huwa nakuwa na ganzi kama ya dakika 10 hivi ila baada ya hapo ni lazima kazi ziende kwa mujibu wa taaluma yangu

All the best Reds, lakini kheri kwenu pia Wananchi kwakuwa ni sehemu ya familia yangu pia

Screenshot_20220430-170951_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Hakuna aliyesafiri kwenda Morogoro au Unguja, hakuna mambo mengi ya kizamani bali kila timu imejiandaa vyema

Hakuna magumashi kutoka kwa Waamuzi wala wachezaji, kila mtu aliingia kufanya kazi yake kwa usahihi na ukamilifu mkubwa uwanjani

Makocha walisomana vyema, wakaingia uwanjani wakagawana vipindi na kila mtu alicheza kwa plan yake nzuri na mechi imekosa tu magoli ila mpira umeonekana

Mashabiki wameondoka uwanjani wakiwa wameridhishwa, wachezaji wote wakakumbatiana na kupata picha za pamoja kuonesha mpira ni uungwana

Kuna Inonga na Mayele wa dakika 90 kisha kuna Inonga na Mayele wa nje ya dakika 90! Wakasalimiana kiungwana, wakafurahi pamoja na kila Mtu akaenda zake, no hard feelings ni football

Taratibu uswahili unaondoka, taratibu usasa unaingia, taratibu taswira ya mpira inakua! Kubadilika kwa Kariakoo ndio kubadilika kwa nchi

Sasa Wananchi mnataka kuchukua bila kufungwa kweli??
Screenshot_20220430-193916_OGInsta%2B.jpg
 
tucheke tu dear yaani nikikumbuka maneno ya shombo ya juzi ya yule msemaji wao anavyoisema vibaya simba na msemaji wetu yaani leo sikutegemea hiki nilichokiona
Hahaha sio kwa mbwembwe zile aisee
Ooh sijui nini .. yako wapi sasa , natamani jtatu ifike upesi tusikilize uchambuzi kutoka kwa wachambuzi wa mchongo .
 
Imeandikwa na @swalehmawele

FT: Yanga SC 0-0 Simba SC.

Ilikuwa ni mechi nzuri katika sanaa ya uzuiaji na haikuvutia kwa sababu hazikuonekana zikitengenezwa nafasi nyingi za kufunga, lilikuwa ni swala la nani angeweza kufanya kosa kubwa ili aadhibiwe, timu zote mbili zilikosa funguo ya kuifungua safu ya ulinzi ya timu pinzani ( unlock defensive patterns ).

Mohammed Nabi aliuweka mtego wake katika kipindi cha kwanza kwenye turn overs ( Simba wanapoupoteza mpira ), aliitaka timu yake iwe direct wanapoupokonya mpira, pasi tatu mpaka nne wawe kwenye zone ya Simba na watengeneze nafasi, tatizo lilikuja kwao katika uharaka wa wachezaji wa Simba kwenye kuziba mianya ( coverage ).

Simba ilichagua kucheza taratibu hasa kwenye eneo la kiungo, unaweza kucheza na Yanga kwa zaidi ya siku mbili na wasikupe mianya, mikimbio inayofanyika mbele ya safu ya ulinzi, unategemea nini dhidi ya quality kama ile? ndicho kile kilichotokea, mikimbio mbele ya safu yao ya ulinzi.

Kipindi cha pili walimu wote wawili walibadili game approach, Mohammed Nabi akaweka presha wakati ambao timu ina mpira au haina mpira na Pablo Franco akaziwinda pasi za kuchonga kutoka kwa Rally Bwalya zinazovuka safu ya kiungo ya Yanga baada ya kushindwa kwenye penetration passes, sub ya Bwalya ilikuwa ni ya kimkakati zaidi, pia haikufanikiwa kwa sababu Yanga walicheza aerial duels nyingi zaidi.

Inakera kucheza dhidi ya Kibwana Shomary, alicheza vyema mbele ya Morrison, akaonyesha umwamba kwa Sakho na hakumuhofia Shomary Kapombe.
Zipo nyakati ambazo ulikosekana ukomavu na uthubutu, wachezaji wengi walifikiria kwanza kuzisaidia timu zao zisifungwe, pakubwa ilipunguza ufanisi wao katika forward movement.
Henock Inonga wow, anacheza kama hatacheza tena, mwanaume wa shoka mno, anacheza kwa ajili ya timu na mashabiki.
Aishi Manula na Djigui Diarra walikutana na mechi nyepesi kwa upande wao, hawakujaribiwa mara nyingi.
Screenshot_20220430-195159_OGInsta%2B.jpg
 
Wakala wa wachezaji, Mino Raiola amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 54 baada ya kupigania uhai wake kwa muda akiwa hospitalini.
Raiola alikuwa wakala wa wachezaji mashuhuri kama Zlatan Ibrahimović, Paul Pogba, Haaland na Henrikh Mkhitaryan.
Screenshot_20220430-200344_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Yalikuwa ni maji yale ambayo Nabii Musa alipaswa kuchapa fimbo ili Wanaisrael wavuke bahari ya Sham kuelekea nchi ya ahadi, ndipo hapo ikaja stori maarufu ya Fimbo ya Musa

Yalikuwa ni maji yale ndio yalizamisha meli maarufu ya TITANIC kwenye bahari ya Atlantic upande wa Kaskazini, ndio ilikuwa April 25, 1902 ni hapo tukapata movie nzuri ya Titanic na wale Rose na Jack

Nachokifahamu kwa uhakika ni kuwa Tanzania imepakana na Kongo, kinatutenganisha ni maji, yes ni maji ya ziwa Tanganyika! Wataalam wanasema ni ziwa lenye kina kirefu zaidi Afrika, ndipo huko nyumbani kwa huyo pichani

Basi nipeni maji kwanza ninawe kisha nisome kuhusu BALL POSSESION! La haula! Ndio hii Simba 51% kwa 49%?? Na vipi kuhusu shots on target?? Ni kweli Yanga hawana?? Hapana sina uhakila

Mpeni maji anawe, ni usafi kama waislamu na udhu, kama ndege na mwanae, kama jangwa na joto, kama Mburahati na singeli, kama udaku na Mwijaku, kama Morogoro na mpira basi kama HENOCK INONGA na FISTON MAYELE

Katikati ya mziki mkubwa wa Mayele basi Inonga aliondoka flash yake, katikati ya umeme wa Mayele basi Inonga alizima main switch, katikati ya biriani na Ijumaa basi Inonga alileta kisinia Jumatatu

Nipeni nami maji ninawe na mengine nimpelekee Kaka Mayele

If defense could have been the question then HENOCK INONGA could have been the answer!
Screenshot_20220430-202216_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom