Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220430-060124_Opera%20Mini.jpg
 
DUUH! CHICO KUIKOSA DERBY
.
Kwa mujibu wa Kocha msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze winga tereza raia wa Congo, Chico Ushindi atakosekana kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Simba kutoka na kuugua ghafla jana ambapo ililalazimika kupelekwa Hospitali.
Screenshot_20220430-061128_OGInsta%2B.jpg
 
Nimeshacheza derby nyingi za Simba na Yanga lakini mechi ambayo sitaisahau ni ile mimi nikiwa Yanga, kwa bahati mbaya nilifungwa goli la kona na Kichuya. Kwa upande wangu nilipata mtihani mkubwa sana japo nilishacheza mechi nyingi.

Nishawahi kufungwa pia na Emanuel Okwi lakini presha haikuwa kubwa kama ambavyo ilitokea kwa goli la Kichuya.

- Ally Mustapha ‘Barthez’, Golikipa wa zamani Simba, Yanga.
Screenshot_20220430-061418_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo April 29 amefanya kikao cha pamoja baina yake, Viongozi wa Masoko na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa lengo la kutoa elimu ya udhibiti wa majanga ya moto kwenye masoko ya Mkoa wa Dar es salaam.

Uamuzi wa RC Makalla kuitisha kikao hicho ni Kufuatia kuungua kwa baadhi ya masoko ndani ya muda mfupi ambapo ripoti za Kamati zinazoundwa kuchunguza zinaonyesha kuwa chanzo ni uzembe wa Watu kujiunganishia umeme kiholela na kina Mama kuweka maharage kwenye majiko usiku ili asubuhi wakute yameiva.

Kutokana na changamoto hiyo RC Makalla ameelekeza kila soko kuwa na vifaa vya kudhibiti moto na fundi wa umeme anaetambuliwa na TANESCO.

RC Makalla ameelekeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuandaa ratiba ya kupita kila soko la Mkoa huo na kutoa elimu ya kujikinga na majanga ya moto.
Screenshot_20220430-061622_OGInsta%2B.jpg
 
DC wa Temeke ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ametoa siku saba kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wilayani humo kuhakikisha wanaunda vikundi vya ulinzi shirikishi ambapo amesema mitaa ambayo haina ulinzi shirikishi ndio inayoripotiwa kuwa na matukio mengi ya uhalifu.

DC Jokate ametoa agizo hilo leo Aprili 29,2022 alipokuwa akizungumza na Wenyeviti hao "Ninatoa siku 7 muhakikishe kule ambapo hakuna vikundi vya ulinzi shirikishi mnaanzisha vikundi hivyo na kule ambapo vilikuwepo ila vinalegalega mviimarishe"

"Leo tunapozungumzia kuifungua Tanzania kama afanyavyo Rais Samia, ni kwamba Watu wanaitazama Tanzania na hususan Mkoa wa Dar es Salaam kama ni eneo salama, naahidi Temeke hatutakuwa Watu wa kuibadilisha taswira hiyo, kwenye mitaa au maeneo ambayo ulinzi shirikishi unasuasua au umegubikwa na siasa wajitathimini"

Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Kamanda Muliro pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ikiongozwa na OCD Temeke, wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na baadhi ya vikundi vya ulinzi shirikishi kilikuwa na lengo la kuweka mikakati ya jinsi ya kukabiliana na wimbi la vitendo vya uhalifu ambavyo vimeanza kujitokeza kwa siku hizi za karibuni.
Screenshot_20220430-061819_OGInsta%2B.jpg
 
Beki wa Simba SC Shomary Kapombe ametoa maoni yake kuelekea derby ya Kariakoo dhidi ya watani zao wa jadi Yanga ambapo mchezo utachezwa kesho Jumamosi ya April 30 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tunajua kuwa tumetolewa katika mashindano ya kimataifa wiki iliyopita, sisi kama wachezaji kutolewa katika mashindano kama yale imetuweka katika hali ngumu"

“Baada ya kutolewa katika mashindano kama yale sisi kama wachezaji tulikaa tukajipanga na tukaongea sababu mchezo unaokuja ni mchezo mkubwa zaidi na wenye hisia kubwa kwa mashabiki wetu”Kapombe
Screenshot_20220430-061923_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom