Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wakati tunapambana na mfumuko wa bei (inflation) unaondelea kwa kasi kubwa bila juhudi zozote za serkali kuingilia kati japo kuondoa baadhi ya kodi na vikwazo. Sasa wafanyabiashara nao wamekuja na mbinu nzuri kabisa ya kibiashara, mfinyo au mbinyiko (sio lile basi la kwenda Dodoma Kimbinyiko nadhani).

Hii mbinu kwa kiinglishi wanaiita shrinkflation (from word shrink- decrease in bulk or volume), mbinyiko huu wengi huwa hatuuoni sana kwa sababu hatuna kawaida ya kuangalia ukubwa/ujazo wa baadhi ya bidhaa tunazonunua. Mathalani, kwa kiwango cha kawaida kabisa, nyama (natoka jamii ya wafugaji) unanunua kilo moja ila unajaziwa mifupa na mafuta ya kutosha na unauziwa kwa bei ile ile. Unaponunua bidhaa angalia mfuko (packaging inasomaje, utaona)

Kwa sisi tunaotumia breakfast ya kitaifa, chai chapati mbili, mara zote tunadhani chapati zina ukubwa na uzito sawa !!! ( this does not make me stingy-mind you, got tumboz tu feed). Maharage pia, bakuli ambalo mhudumu alipakua upawa full wa maharage leo unaweza kuhesabu punje ngapi za maharage zinazoelea kwenye mchuzi mwingi 🙂. Makampuni ya simu na bundle zao ni mfano mzuri, bundle linapunguzwa kwa bei ile ile.

Sawa, mbinyiko huu unauhisano mkubwa sana na mfumuko wa bei na mlaji anakuwa makini (price sensitive) na pesa yake na vivyo hivyo muuzaji (na mzalishaji) anakuwa makini na kuhakikisha anapata faida kwa hiyo anabinya bidhaa huku akikuuzia kwa bei ile ile maana mbinyo (mfinyo) unamlazimisha achague yafuatayo;
Mosi, aongeze bei (wateja watakimbia maana kipato chao hakijabadilika), pili, apunguze ujazo kidogo kwa bei ile ile au tau, atafute malighafi za kiwango duni akuuzie kwa bei ile ile.

Tunakwenda wapi, hatuwezi kusema tunakwenda wapi kama tulipo hatujui ni wapi, kauli ya mama ni sahihi (bei zitapanda-fact) lakini baadhi ya wafanyabiashara waliona ni wigo sasa wa kupandisha bei na sasa kuna taharuki, mgeni akikutembelea saa sita na saa nane hajala huyo ongeza chungu.
Leo hakuna magazeti na kwa kuwa Shunie mfumuko wa bei la bundle umemzidia na Lee alikuwa kwenye bia za promosheni jana simu yake ametunziwa na Ashura.

Nimeona nikupe kitu rahisi cha kusoma na kutafakari.

AshamedJoyousCranefly-max-1mb.gif

MALCOM LUMUMBA
 
Hahahhaha nitaweka binamu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom