Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220327-065538_Instagram%20Lite.jpg
 
Farhan jr

Katika transformation kubwa ambayo Simba wameifanya kwa misimu mitatu nyuma ni eneo la usajili na uhamisho wa wachezaji, eneo wamejifunza vingi

Afrika Mashariki hii timu nyingi zinafanya sajili za kujuana, za kishkaji na kwenda mbali zaidi zina mikono ya watu ndani ya system ya timu (SYSTEMIC REGISTRATION)

Sajili hizo mara nyingi haziendi kutibu shida ya timu bali kutibu matatizo kwenye mifuko ya watu, kupitia 10% ndio maana sajili nyingi za kimataifa zilikuwa zinafeli sana nchini, Simba ikiwemo

Hakuna njia iliyosalia ya kubadili upepo zaidi ya kukubali kujifunza, kupata EE BALANCE yaan Exposure na Experience, ndipo CEO alipopaswa kusafiri kufahamu wenzao wanafanyaje

Alifika Al Ahly pale Misri, TP Mazembe (alipata kuonana na Viongozi) pamoja na Mamelodi Sundowns, yote hii ni miamba Afrika ambayo imebobea kwenye biashara za wachezaji

Katika darasa kubwa alilopata CEO ni networking, kati ya Klabu na AGENCIES (Mawakala) ambao wapo kwenye mfumo wa Kampuni, yes ndio njia rahisi zaidi ya kupata wachezaji wazuri kwa gharama nzuri kisha kufanya biashara kubwa

Simba kupitia Agencies wakapata faida ya kuwa na Scouts zaidi ya 62 Afrika nzima, ni rahisi wao kumpata Sakho mwingine kutoka Bambali, Peter Banda mwingine kutoka Lilongwe au Kanoute mwingine kutoka Mali

Hii biashara ni WIN WIN, kwakuwa walichowin Simba ni kuwa na uwanja mzuri wa mazungumzo kabla ya biashara (PHATIC FUNCTION PER BUSINESS) ndio urahisi huu walimpata Peter Banda mbele ya Sherrif Tiraspol

Wamejifunza kitu, hata ukitazama sajili zao za kimataifa msimu huu, watoto wengi wana misimu zaidi ya nane mbele na biashara kubwa mbele, zoezi kubwa walilosalia nalo ni dirisha la ndani, kuna sehemu padogo pana shida, JE NI WAPI HAPO?

Lets end here, but tomorrow we shall continue tackling some more problems concerning this case ITAENDELEA

Screenshot_20220327-121929_Instagram.jpg
 
CLEAN SHEET NYINGI LIGI KUU YA NBC
.
10— Djigui Diarra (Yanga)
09— Aishi Manula (Simba)
08— Abuutwalib Mshery (Mtibwa/ Yanga)
06— Mussa Mbisa (Coastal Union)
05– Ahmed Salula (Azam FC)
.
Nani atachukua tuzo ya Kipa Bora msimu huu __!!
.

…………….
Screenshot_20220327-133035_Instagram.jpg
 
KIM AWARUHUSU MASTAA SIMBA
.
Simba itakuwa wenyeji wa USGN katika mechi ya mwisho ya Kundi D itakayoamua hatma ya kwenda robo fainali ama kuaga michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
.
Taarifa nzuri kwa mashabiki wa Simba, Kocha mkuu wa Stars, Kim Poulsen amelipokea ombi la kocha Pablo ambaye aliomba wachezaji waliopo Stars waruhusiwe kujiunga na kambi na kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo Kim amewaruhusu wachezaji hao ambao wote sasa wametakiwa kuungana na wenzao kuanzia leo kwa kambi ya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya USGN unaosubiriwa kwa hamu.

......……..
Screenshot_20220327-133210_Instagram.jpg
 
Hazard kama Bale Asema Haondoki Madrid
.
Eden Hazard ameripotiwa kugoma kuondoka Real Madrid na kudai atabaki hapo kugombea namba kwenye kikosi cha Carlo Ancelotti. Ripoti zinafichua kwamba Hazard anataka kubaki Bernabeu hadi mwisho wa mkataba wake ambapo ni 2024.
.
Los Blancos wanatajwa kuwa na mpango wa kumfungulia mlango wa kutokea Hazard kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini mkali huyo wa zamani wa Chelsea amedaiwa kuwa “Gareth Bale mwingine” kwa kugoma kuondoka.
.
Bale ni mchezaji mwingine aliyeigomea Real Madrid kuondoka na kubaki kwenye kikosi hicho hadi mwisho wa msimu huu ambapo mkataba wake utafika tamati huko Bernabeu.
.
………….
Screenshot_20220327-133328_Instagram.jpg
 
󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 ENGLAND WAFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE
.
️ 53 - Wayne Rooney
️ 49 - Harry Kane
️ 49 - Bobby Charlton
️ 48 - Gary Lineker
️ 44 - Jimmy Greaves
.
Kane anaelekea kuivunja rekodi ya Wazza.
Screenshot_20220327-133444_Instagram.jpg
 
“Ni lazima turekebishe makosa yetu ili tupate matokeo mazuri dhidi ya Chelsea, kwakuwa ni timu ngumu” Toni Kroos, kiungo wa Real Madrid
Screenshot_20220327-133704_Instagram.jpg
 
Miaka 19 tu imetosha kwa Pedri kuonesha ubora mkubwa sana, anacheza kama ana miaka 27

Ukomavu mkubwa akiwa na jezi ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania

Screenshot_20220327-133750_Instagram.jpg
 
Kauli ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba ya kutaka Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kuelekeza dola 1.3 bilioni za Asasi za Kiraia kwenda kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita, imekosolewa na wadau wa asasi hizo.

Akiandika katika ukurasa wake wa Twitter, Dk Mwigulu amesema walikuwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Emmanuel Tutuba katika mkutano na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Kate Somvongsiri.

Screenshot_20220327-140145_Instagram.jpg
 
Mwimbaji wa Bongofleva, Diamond Platnumz amesema hapendezwi kushindanishwa na wasanii nchini kutokana na kuwazidi katika maeneo makuu matatu; ambayo ni mauzo, shoo za kimataifa na maendeleo (mali) yatokanayo na muziki.

Je, kauli hiyo inasadifu muziki wa msanii huyo kwa kiasi gani? Makala hii inakwenda kuangazia hilo kwa kina, tena kwa mtindo wa namba ambazo kamwe hazidanganyi!

Diamond, aliyetoka kimuziki mwaka 2009 ameshinda tuzo za kimataifa kama Channel O, MTV, Soundcity, Headies, Afrima, Afrimma, Kora, AEA, EAUSA, the HiPipo Music Awards n.k na kumfanya kuwa msanii pekee Bongo kufikia mafanikio hayo kwa kipindi cha miaka 10.

Anashikilia rekodi ya kushinda tuzo saba za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 2014 kwa usiku mmoja, anakaribiwa na Alikiba aliyeshinda tuzo tano mwaka 2015, ikiwa ni sawa na asilimia 20 kwa mwaka 2011.

Ndiye msanii wa kwanza Bongo kuchaguliwa kuwania tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act, tayari amewania mara tatu (2014, 2016 na 2021) na kumfanya kuwa msanii pekee Bongo aliyewania mara nyingi.

Kwa kipindi cha miaka 12 katika muziki wa Bongofleva, Diamond ameweza kushinda na kutunukiwa tuzo zaidi ya 46 za ndani na za kimataifa, huku akimpiku Lady Jaydee mwenye tuzo zaidi ya 35.

Screenshot_20220327-140327_One%20UI%20Home.jpg
 
Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kwa msisitizo kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin "hatakiwi kubaki madarakani" kauli ambayo baadae Ikulu ya White House imesema haikuwa imeandikwa kwenye hotuba yake.

"Kwa ajili ya Mungu, Mtu huyu hawezi kubaki madarakani" alisema Biden wakati wa kuhitimisha ziara yake ya Ulaya akiwa kwenye Jumba la Kifalme huko Warsaw, Poland.

"Hoja ya Rais ilikuwa kwamba Putin hawezi kuruhusiwa kutumia mamlaka juu ya majirani zake au eneo, Rais Biden hakuwa akijadili uwezo wa Putin ndani ya Nchi yake ya Urusi au mabadiliko ya Serikali, mstari aliosema Putin hawezi kubaki madarakani haukuwepo kwenye hotuba yake iliyotayarishwa na kuandikwa" amesema Afisa mmoja wa Ikulu ya White House ambapo pia Maafisa wengine wa Marekani walisema hapo awali kwamba kumuondoa Putin madarakani halikuwa lengo lao.

"Kwetu sisi sio kuhusu mabadiliko ya Serikali, Watu wa Urusi wanapaswa kuamua ni nani wanataka awaongoze" alisema Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken.

Msemaji wa Serikali ya Urusi amesema kauli hii ya Biden sio sahihi kwani maamuzi ya Putin kubaki madarakani yanapaswa kufanywa na Watu wa Russia.
Screenshot_20220327-141501_Instagram.jpg
 
Moja ya story kubwa za wiki hii ni hiii ya Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un pamoja na Wanajeshi kuamua kutengeneza video fupi ikionesha tukio la jaribio la kombora.
Screenshot_20220327-141621_Instagram.jpg
 
Tanzania inaenda kuandika historia nyingine kwenye sekta ya uwekezaji wa viwanda kwa kuwa na kongani kubwa ya viwanda 200 katika eneo la Kwala, Kibaha mkoani Pwani.

Mradi huo ambao jana Mwekezaji kutoka China, Kampuni ya SINO TAN INDUSTRIAL PARK amekabidhiwa ardhi yenye ukubwa wa Ekari 2500 unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu.

Akizungumza baada ya kushuhudia makabidhiano rasmi ya ardhi kwa Mwekezaji wa mradi huo unaogharimu Dola za Marekani bilioni 3, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji anasema uwekezaji huo unaenda kusaidia serikali kupunguza matumizi ya fedha ya kigeni kuagiza bidhaa kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Prof. Godious Kahyarara mradi huo unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000.
Screenshot_20220327-141741_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom