Makapuku Forum

Makapuku Forum

Unafahamu nini kuhusu tiba ya upandikizaji wa uboho? wamesema ni mpya sana kwenye Taifa la Tanzania ambapo sasa imeanza kutolewa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo sasa inaingia kwenye orodha ya Hospitali chache za Afrika zenye uwezo wa kutoa matibabu haya.
Screenshot_20220322-160531_Instagram.jpg
 
Mahakama nchini Afrika Kusini imesimamisha ujenzi wa Makao Makuu ya Amazon Africa, kwenye ardhi takatifu, Jaji Patricia Goliath amesema Liesbeek Leisure Properties Trust (LLPT), Mmilii wa eneo la ekari 37 huko Cape Town, Afrika Kusini lazima asimamishe ujenzi mara moja akisubiri mashauriano sahihi na ya maana na Watu wa asili wa kabila la Khoi na San.

Watu wa kabila ya Khoi na San wameishi Afrika Kusini kwa maelfu ya miaka, maendeleo ya makazi na biashara yanajengwa kwenye makutano ya mito miwili, karibu na maeneo ya malisho ambayo yalikuwa na sherehe na ambapo watu wa asili walipigana na Wavamizi, uamuzi umesema.

Africa Kusini inakumbwa na tatizo kubwa la ajira, mradi huu ungetoa ajira nyingi kwa Watu wa eneo hilo; ila bado Watu wa asili la eneo hilo lazima wahusishwe.
Screenshot_20220322-160632_Instagram.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema upatikanaji wa maji katika eneo la Chalinze haukuwa rahisi kwa sababu kulikuwa na mvutano mkali baina ya viongozi ambao uliolenga kujenga.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 22, 2022 mara baada ya kuzindua mradi wa maji Mlandizi Chalinze – Mboga ulioanza Julai 2019 na kukamilika Novemba 2021.

“Nakumbuka wakati wa kampeni tulipokuwa tunapita kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza Serikali kupitia CCM, nilijionea mwenyewe changamoto za maji nchi nzima ikiwemo mkoani Pwani, hasa hapa Chalinze baada ya kampeni nilikuja kwa tukio jingine.

“Ndiyo hiyo siku nilimuona mwanangu Ridhiwan akifoka moto mdomoni unatoka akimfokea Injinia Luhemeja kwamba usipoleta maji hapa nakushtaki kwa wananchi lakini leo nimeshuhudia kila mmoja kamuomba radhi mwenzake kwa matamshi makali lakini maji yamepatikana Chalinze leo tunavyofurahia safari ilikuwa ndefu na ngumu,” amesema Rais Samia.

Amesema Serikali imeipa upekee mkubwa mkoa wa Pwani na maeneo mengine kwa kuwa ina dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani.
Screenshot_20220322-160924_Instagram.jpg
 
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amemtaka Rais wa Russia, Vladimir Putin wazungumze moja kwa moja, akieleza kuwa ana mpango wa kumhakikishia kuwa hatajiunga tena na Nato.
Screenshot_20220322-161104_Instagram.jpg
 
• Wakati sakata la kumtaka msanii Steven Mengele maarufu Steve Nyerere, kujiuzulu nafasi ya usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), mwenyewe amesema hatojiuzulu hadi aandikiwe barua na waliomteua.
Screenshot_20220322-161251_Instagram.jpg
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amesema ndege aina ya Embraer 190 (5H-FJH) iliyozuiwa nchini haiwezi kutumika kulipa madeni ya waliokuwa wafanyakazi wa Fastjet Tanzania kwa sababu haikuwa mali ya shirika hilo.

Johari aliyasema hayo baada ya waliokuwa wafanyakazi 105 wa Fastjet Tanzania, kuingiwa hofu iwapo Sh5 bilioni wanazodai shirika hilo zitalipwa, baada ya kile walichodai kuwa ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa kama dhamana, imebadilishwa usajili na kuruhisiwa kuondoka.
Screenshot_20220322-161356_Instagram.jpg
 
Mpiganaji wa Mau Mau, Michael Kirungia amefungua kesi Mahakama Kuu ya Kenya jijini Nairobi akitaka kuondolewa ofisini kwa Naibu wa Rais wa Kenya, Dk William Ruto.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa kwa hati ya dharura na Michael Ki
Kirungia anadai kuwa Dk Ruto ameacha kazi zake za kikatiba kama msaidizi mkuu wa rais na kufanya kazi ambazo anajipangia mwenyewe.
Inaripoti Daily Nation
Screenshot_20220322-161525_Instagram.jpg
 
Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis inayowakabili maofisa saba wa polisi mkoani Mtwara, imeahirishwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Washitakiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara leo Jumanne Machi 22, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lugano Kasebele na kutumia dakika 2 tu mahakamani hapo kabla ya kuahirisha hadi Aprili 5, 2022
"Haya tuonane tarehe 5 Aprili upelelezi haujakamilika" Amesema Hakimu Kasebele
Screenshot_20220322-161628_Instagram.jpg
 
Golkipa wa klabu ya Zamalek na timu ya taifa Misri, Mohamed Abou Gabal akiwa na kipa wa Simba, Aishi Manula wa kocha wa makipa Tyron Damons walipokwenda kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Berkane nchini Morocco.
Screenshot_20220322-161748_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom