Makapuku Forum

Makapuku Forum

Baada ya Rais wa Shirikisho la soka nchini Morocco kutangaza kuwa Hakim Ziyech atajumuishwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya taifa, winga huyo amechapisha ujumbe kwenye Instagram kukanusha

Ziyech anasema tayari alishastaafu timu ya taifa na anaendelea kukazia kuwa hatorejea tena kuvaa jezi ya timu kutokana na mambo mengi yanayoendelea ikiwemo ya uzushi juu yake
Screenshot_20220315-140648_Instagram.jpg
 
Karim Benzema amekuwa mwanasoka aliyefunga mabao mengi katika historia ya watikisa nyavu nchini Ufaransa baada ya mabao yake mawili ya jana (Jumatatu) kuipa Real Madrid ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mallorca, matokeo yanayowafanya waendelee kuongoza La Liga kwa tofauti ya pointi kumi.

●Karim Benzema-412
●Thierry Henry-411
Screenshot_20220315-140951_Instagram.jpg
 
KOCHA wa timu ya Taifa Tanzania, Kim Poulsen amewaacha wachezaji wakongwe John Bocco na Erasto Nyoni katika kikosi chake kinachoingia kambini Jumapili kwa ajili ya mechi za kufuzu Chan na AFCON.

Kim amesema amewaacha nyota hao lakini bado wana nafasi ya kumshawishi kwenye mechi zao zijazo ili aweze kuwarejesha kikosini.

“Erasto na Bocco hawatokuwepo lakini bado wana nafasi ya kurejea wakati tukiwa kambini na bado kuna muda kabla ya kucheza mashindano yetu,” amesema Kim.

Screenshot_20220315-141055_Instagram.jpg
 
Baada ya kutoa sare na Crystal Palace usiku wa jana klabu ya Manchester City imeendelea kupunguza pointi kati yake na Liverpool na kutoa mwanya wa pointi nne huku Liver akiwa na mchezo mmoja mkononi.

1. Manchester City- Mechi 29 na Pointi-70
2. Liverpool-Mechi 28 na Pointi-66
3. Chelsea-Mechi 28 na Pointi-59
4. Arsenal-Mechi 26 na Pointi-51
5. Manchester United-Mechi 29 na Pointi-50.

Screenshot_20220315-141311_Instagram.jpg
 
Uongozi wa klabu ya Yanga, umesema kitu muhimu ni taratibu za kununuliwa kwa mchezaji husika zizingatiwe, ila ukweli milango yao ipo wazi kwa yeyote kwani wataleta majembe mengine ya maana ya kuifanya Yanga iendelee kuwa imara na tishio zaidi.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuenea tetesi kwamba straika Fiston Mayele anatakiwa na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, japo mtendaji mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa alishakanusha kuwa hakuna ofa yoyote kwao kutoka Sauzi na kwingineno.

Akizungumza na Mwanaspoti, mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hersi Said alisema hakuna mchezaji atakayezibiwa riziki kama atatakiwa na timu ya nje au klabu nyingine ya ndani ilimradi taratibu zifuatwe.
Screenshot_20220315-141426_Instagram.jpg
 
Karim Benzema amekuwa mwanasoka aliyefunga mabao mengi katika historia ya watikisa nyavu nchini Ufaransa baada ya mabao yake mawili ya jana (Jumatatu) kuipa Real Madrid ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mallorca, matokeo yanayowafanya waendelee kuongoza La Liga kwa tofauti ya pointi kumi.

Lakini Mfaransa huyo alilazimika kutoka uwanjani akichechemea katika kile kinachoonekana kuwa ni jeraha upande wa chini wa mguu wake wa kushoto, jambo linaloiweka Real Madrid katika sintofahamu wakati ikijiandaa kuikabili Barcelona katika mechi ya wababe wa Hispania, maarufu kama El Clasico.

Vinicius Junior, ambaye alifunga bao la kwanza, na Rodrygo pia walipata matatizo katika kipindi cha pili.
Screenshot_20220315-141625_Instagram.jpg
 
Mtoto wa bilionea Juan Carlos Escotet Rodriguez mwenye umri wa miaka 31 amepoteza maisha wakati akijaribu kumuokoa mchumba wake wakati wa mashindano ya uvuvi mwishoni mwa wiki katika jimbo la Florida.

Kwa mujibu wa Magazine Espanol, mtoto huyo wa bilionea anayeitwa Juan Carlos Escotet Alviarez, ambaye ni mkurugenzi wa Banesco, alikuwa amepanga kumuoa mchumba wake, Andrea Montero mwezi Novemba.

Jarida la Miami Herald limeripoti kuwa mtoto huyo alifariki wakati akijaribu kumuokoa Montero aliyekuwa ameanguka kutoka kwenye boti yao ya urefu wa futi 60 wakati wawili hao wakishiriki shindano ya kuvua samaki lililoandaliwa na klabu ya Ocean Reef.

Herald limeandika kuwa baada ya kuingia majini, kijana huyo alipigwa na upanga wa boti hiyo na akafariki kutokana na majeraha aliyopata.

Gazeti hilo linamkariri mwandishi wa habari, Angela Oraa wa Venezuela akisema Montero aliweza kutoka majini bila ya matatizo.

Screenshot_20220315-141742_Instagram.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imepanga Mei 6, 2022 kutoa hukumu ya rufaa iliyokatwa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wanaopinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Leo Machi 15, 2021 rufaa hiyo ya jinai namba 129/2021 ilipangwa kwa ajili ya kutajwa ambapo Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Ruth Massam amesema hukumu hiyo itatolewa Mei 6, 2022.

Mbali na Sabaya waomba rufaa wengine ni Sylvester Nyegu na Daniel Mbura ambapo rufaa hiyo ilikuwa inasikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Sedekia Kisanya.
Screenshot_20220315-142033_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom