UEFA CHAMPIONS LEAGUE
.
Man United inaingia kwenye mchezo huu ikijiamini kwa sababu ilishapata sare kwenye mechi ya kwanza ugenini, lakini pia imetoka kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Spurs kwenye mchezo uliopita.
.
Mbali ya yote, inaingia ikiwa na muuaji wa Atletico Madrid, Cristiano Ronaldo ambaye ana rekodi ya kuifunga timu hiyo mabao mengi zaidi alipokuwa Real Madrid na Juventus.
KIIZA: MABEKI WANAKAMIA SANA
.
Baada ya kuitungua Simba na kufanikiwa kuipa pointi tatu timu yake mshambuliaji wa Kagera Sugar, Hamis Kiiza amelia na kukamiwa na mabeki wa timu pinzani katika Ligi Kuu Bara, huku akikiri kuwa ligi msimu huu ni ngumu.
.
“Tangu niwafunge Simba wapinzani wananikamia, lakini wanasahau Uwepo wangu kwenye kikosi sio kigezo cha kufanya kila kitu, nisipofunga kuna mwingine atafunga hivyo kikubwa mchango wangu uonekane na sio kukamilisha tu idadi ya namba ya wachezaji.”
Uwanja wa Deva unaotumiwa na klabu ya Chester FC ni uwanja pekee wa klabu Duniani ambao unapatikana katika nchi mbili tofauti, uwanja huu una uwezo wa kuingiza watazamaji 6000 na upo mpakani mwa nchi ya England na nchi ya Wales, eneo la kuchezea na majukwaa yapo Wales wakati ofisi za klabu zipo nchini England.
Mpira wa Afrika una mambo mengi sana, ndio maana kwasasa timu nyingi zimeacha kulalamika bali kucheza mpira na kuwekeza kwenye mpira
Simba wanafanyiwa mengi sana ugenini ila wao wamechagua kuacha kulalamika na kuwekeza kwenye mpira, wakipageuza kwa Mkapa sehemu ngumu mtu kucheza
Kwa Madiba wale Mamelodi Sundowns walizuia mpaka Bus la Al Ahly lisipite, wanajua sio sahihi ila ndio fitna za soka la Afrika, kushinda mchezo haiwi tu ndani ya uwanja
Kabla ya kulalama na kuisema vibaya Simba ambayo haihusiki na maamuzi ya Marefa, jaribu kuvuta picha nao huwa wanafanyiwa mangapi nje ya nchi? Ni vile tu wameacha kulalama na kuamua kucheza mpira
Msemaji wa ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, ametoa taarifa ya kusikitishwa na kitendo cha Mashabiki wa Chelsea kuliimba jina la Roman Abramovich na kuonesha wapo sambamba nae
Mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakiipinga serikali waziwazi, huku wakitaja jina la Roman kwenye mechi ya pili mfululizo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.