"Hadi kufikia Februari, 2022, Tanzania inakadiriwa kuwa na Watu 1,700,000 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) ambapo, WAVIU Milioni 1,491,147 sawa na 88% ya WAVIU wote walikuwa wanatambua hali zao za VVU ikilinganishwa 83% mwezi Machi 2020"
"Vilevile kati ya WAVIU Milioni 1,471,450 sawa na 99% ikilinganishwa na WAVIU 98.6% Machi 2021 wako katika tiba endelevu ya ARV na 95.8% walikuwa wamefubaza VVU ikilinganishwa na
94.8%, Machi 2022"
"Kati ya Wenye Virusi vya UKIMWI (WAVIU) Milioni 1,471,450 sawa na 99% ikilinganishwa na WAVIU 98.6% Machi 2021 wako katika tiba endelevu ya ARVs na 95.8% walikuwa wamefubaza VVU ikilinganishwa na 94.8% Machi 2022"
"Hii imetokana na kwamba Tanzania imeendelea kujipima kwa malengo ya 95-95-95, ambapo 95% ya WAVIU wanatakiwa kujua hali zao za maambukizi, 95% ya wanaojua hali zao wawe wameanza dawa za kufubaza VVU na 95% ya walio kwenye dawa wawe wamefubaza VVU chini ya kopi 1000 ifikapo 2025" ——— Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akitoa taarifa ya mafanikio ya Wizara kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Samia