Makapuku Forum

Makapuku Forum

Soko la Mbagala rangi tatu lililopo Wilayani Temeke Dar es salaam limeungua kwa moto usiku wa kuamkia leo, tayari DC wa Temeke Jokate Mwegelo na RC wa Dar es salaam Amoss Makalla wapo eneo la tukio.
Screenshot_20220213-140121_Instagram.jpg
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema Serikali ya awamu ya sita tayari imepeleka Bilioni 30 kwenye Mikoa 10 ambapo kila Mkoa umepokea sh. Bilioni 3 kwa ajili ya kujenga Shule maalum za sayansi kwa ajili ya Wanafunzi wa kike.

Waziri Bashungwa ameeleza hayo katika mdahalo maalum wa kujadili mafaniko katika Sekta ya elimu kwa mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Waziri Bashungwa amesema kupitia mradi wa SEQUIP Serikali imepeleka Bilioni 110 kwenye kata 235 ambazo bado hazina Shule za Sekondari na ujenzi umeshaanza na wengine wapo hatua ya ukamilishaji wa Shule hizo 235.

Bashungwa amesema ndani ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan tayari ameshatoa kibali cha kuajiri Walimu 6949 ambapo Walimu 3000 walikuwa Walimu wa Sayansi kwa Shule za Sekondari.
Screenshot_20220213-140257_Instagram.jpg
 
Mwanamke mmoja aitwaye Nancy Amani amefikishwa Mahakamani nchini Kenya kwa tuhuma za kumuibia Sylvester Mwangi ambaye alimkaribisha nyumbani kwake Jijini Nairobi kama Rafiki wa kawaida, Nancy anasema hakuiba bali alipewa vitu na Mwangi kwakuwa ni Wapenzi.

Nancy anadaiwa kuiba TV, Sub-Woofer, mtungi wa gesi, viatu, nguo n.k "Nancy alimpigia Mwangi na kumuambia anasafiri kutoka Nyahururu kwenda Nairobi na kumuomba ampe hifadhi nyumbani hana pa kufikia na alidai gari lake alilokuwa anatumia limeazimwa na Rafiki yake"

"Mwanaume alimkaribisha nyumbani, aliondoka asubuhi akamuacha pale kwake, akiwa kazini akapigiwa na Majirani wakimuuliza kama anahama nyumba alipouliza kwanini akaambiwa Wanawake wawili wamebaba vitu kutoka ndani kwako na wameondoka na pikipiki"

Nancy amekana kuhusika na wizi na kusema Mwangi ni Mpenzi wake na alimpa vitu hivyo kwa mapenzi yake, ameachiwa kwa dhamana na kesi itaendelea tena February 24,2022.
Screenshot_20220213-140401_Instagram.jpg
 
Polisi Mkoani Njombe wamemkamata Daniel Mwilango kwa tuhuma za mauaji ya Nickson Myamba (48) aliyekuwa Katibu wa Baraza la Walei Kanisa la Roman Katoliki Kigango cha Parokia ya Makambako yaliyotokea February 08, 2022, Mwilango amekamatwa Wilayani Mvomero, Morogoro.

RPC wa Njombe, Hamis Issa amesema Mtuhumiwa amekamatwa akiwa na vitu mbalimbali vya Marehemu "Simu ya Marehemu alikuwa anayo yeye pamoja na funguo ikiwemo ile ya chumba ambacho tukio lilitokea, Mtuhumiwa huyo amekiri na kuonesha vitu alivyotumia katika mauaji ikiwemo panga aliliokuwa amelitupa chooni, chuma alichotumia kumpiga Marehemu, ndoo na vitambaa vilivyotumika kwa ajili ya usafi wa damu kwenye chumba yalipotendekea mauaji"

"Mauaji yalitokea kwenye duka la vitabu lililopo katika eneo la Kanisa hilo ambapo Mtuhumiwa alijiandaa na kutumia chuma kizito kumpiga mwenzake kisogoni, alipopoteza fahamu alimuongezea chuma kingine na hili pigo la pili lilimsababishia Nickson Kufariki, alichokifanya Daniel alitumia panga kuutenganisha mwili, kiwiliwili, kichwa na kifua vilikuwa sehemu yake halafu na kiuno na miguu vilikuwa sehemu yake”

"Tunamshikilia pia Mlinzi wa Kanisa hilo anayeitwa Nickson Valentine kwa kushiriki katika tukio hilo, upelelezi unaendelea na hadi sasa tumebaini chanzo ni chuki za Mtuhumiwa dhidi ya Marehemu, ukimuuliza anasema 'Marehemu ni tishio la maisha yangu kwasababu amepewa kazi zangu' na anamuhisi Marehemu ndiye aliyesababisha yeye akaondolewa kwenye sehemu ya duka na miradi mingine wakati yeye aliondolewa kwasababu ya ubadhilifu na sio vinginevyo”
Screenshot_20220213-140651_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

“When words become unclear, I shall focus with photographs. When images become inadequate, I shall be content with silence.”

Kama maneno ya Mtu wa Morogoro pekee hayatoshi, basi tutazame vyema hii picha, Ni Peter Banda na Mwamuzi wa akiba wakifurahia bao

Vipaji wa Vijana wadogo kama hawa huwa vinapotea mapema sana wakipigwa presha kubwa, Waholanzi na hata Wajerumani wanafanikiwa sana kwakuwa hawa wapatie wakosee wanaona bado wapo kwenye trial and error! Give them time, dont burry them alive
Screenshot_20220214-034314_Instagram.jpg
 
Just from football point of view, kama mtahitaji kuendelea kuwatumia ni nyinyi tu! Kama mtaamua kuendelea kusikiliza kelele basi ni nyie tu
Screenshot_20220214-034443_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Jana nilitoa mtazamo wangu muda kama huu kuwa PETER BANDA na PAPE OUSMANE SAKHO wanapaswa kuanza leo hii, bahati mbaya kuna baadhi hatukuelewana

Nilisema kwa nature ya michuano ya Afrika kuwapa nafasi vijana, basi fahamu yupo tayari umtume bure kwakuwa anajua nini maana ya hii michuano

Nazungumza sana na Cherrif Mwandishi mmoja yupo Paris, anajua kiu ya POS kwenye michuano hii ni mtu wake karibu sana! Huwa nazungumza sana na PB11 Najua pia njaa yake kwenye michuano hii

Whatever happens ila naamini ni wakati wao wa kuendelea kuaminiwa! Leo wote wameanza

Ni kawaida sana kutoelewana
Screenshot_20220214-034559_Instagram.jpg
 
“SAKHO.. What A Goal.. Kwa vimo vya mabeki wa ASEC inahitaji ubongo wa haraka kupiga hesabu za nini anatakiwa afanye wakati mpira ukiwa hewani..
.
“Ikiendelea hivi, sio kulalamika tu, Wataandamana kabisa ” - Ali Kamwe.
Screenshot_20220214-035557_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom