Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wabunge nchini Ghana wametuma mualiko maalum kwa Nahodha wa Black Stars, Andre Ayew afike bungeni kutoa maelezo kwanini Ghana imefanya vibaya AFCON
Screenshot_20220215-084457_Instagram.jpg
 
Uongozi wa Simba umetangaza kumsamehe mchezaji Bernard Morrison ambaye alisimamishwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu na kutakiwa kuomba radhi na wamethibitisha amefanya hivyo, sasa amerejeshwa kwenye kikosi hicho kujiandaaa na mechi zinazokuja.
Screenshot_20220215-084621_Instagram.jpg
 
FA ya Misri imeruhusu mashabiki 50,000 kuingia uwanjani kwenye mchezo wao wa kufuzu kombe la dunia dhidi ya Senegal

Kama Misri itafuzu itakuwa mara yao ya nne, 1934, 1990 na 2018
Screenshot_20220215-164510_Instagram.jpg
 
“Wakati mechi yetu na Ireland tayari imekuwa ngumu, Cristiano Ronaldo alikuja kunywa maji dakika ya 87 na akatuambia kwenye bench kuwa msijali, Ureno tunashinda hii mechi, sote tulishangaa ila akaenda kufunga dakika ya 89 na 96, tukaibuka na ushindi” Danilo, juu ya Ronaldo
Screenshot_20220215-164749_Instagram.jpg
 
“Leo hii Steven Gerrard amekataa kuja kucheza Chelsea labda kwakuwa Liverpool ndio mabingwa wa Ulaya ila baada ya miaka 15 ijayo tutafananisha kati ya wao na sisi, Chelsea itakuwa na makombe mengi zaidi” Jose Mourinho (2005)
Screenshot_20220215-164848_Instagram.jpg
 
| Nasreddine Nabi: “Tutaingia kwa tahadhari kubwa, Biashara United ni timu nzuri ambayo kama tutafanya uzembe tunaweza kupoteza, sitaki hili litokee,”.
.
“Itakuwa mechi ngumu lakini hilo halitaondoa uhalisia wa sisi kupata matokeo mazuri kutokana na namna tulivyojiandaa,”
Screenshot_20220215-165116_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Kutoka Manungu mpaka Jangwani, ameenda kutrain na Kipa wa timu ya taifa ya Mali, Djigui Diarra ambaye amecheza mpira kwenye level kubwa zaidi yake

Anaenda kupangua mashuti ya Fiston Mayele moja wapo ya Mastraika wakali kutoka Kongo, atacheza penati za Farid Mussa moja ya vipaji halisi kwenye Ligi yetu

Atapanga ukuta wa Yannick Bangala kutoka Kongo, Captain Bakari Nondo au Dickson Job! Akiwaambia wapi wakae na nini wafanye pale kwenye uwanja wa mazoezi au mechi

Atapokea maelekezo kutoka kwa Prof Nabi, atapata matibabu mazuri kutoka kwa Madaktari wakubwa na atapokea recovery session imara kutoka kwa Physios wa viwango vya juu

Guys ndio maana hata Kabwili alikuwa anaitwa timu ya taifa na Kocha Kim Poulsen, sio kwa bahati mbaya bali unatrain na nani, unacheza wapi na unaishi vipi!

Guys ndio maana hata Jasper Cillesen alikuwa namba mbili Barca ila Uholanzi alikuwa panga pangua, ndio maana Sergio Romero alikuwa namba mbili United ila Argentina ni panga pangua

Kwenye mpira wa miguu kuanza mechi ni kitu kidogo kuliko miezi 10 ambayo mnashinda wote kambini na kutrain wote experience + exposure

Sitoshangaa Msheri akiitwa National team hivi sasa, unaweza kujiuliza kwanini hakuitwa wakati yupo Manungu! Lakini majibu yapo hapo juu tayari
Screenshot_20220215-165449_Instagram.jpg
 
Baada ya kusambaa kwa maneno yanayosomeka ‘Amka umeze P2” ikiwa ni saa chache baada ya Valentine’s day kupita, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amejitokeza na kuandika yafuatayo.

“Inaweza kuonekana ni utani lakini huu ndio ukweli hasa kwa baadhi ya Watoto wetu wa kike walio shuleni, P2 ni dawa ya kuzuia mimba zisizotarajiwa mathalani kutokana na kubakwa, kondom kupasuka na kwa waliokosea hesabu za siku zao za hedhi na hivyo kujikuta wamefanya yao na ili kuepuka kutoa mimba (abortion) au kuzaa Watoto wasiowatarajia wanaweza kutumia dawa hii”

"Hivyo kama Serikali tusingependa kuziwekea vikwazo dawa hizi, tunatamani upatikanaji wake usiwe na changamoto yaani ziwe zinapatikana haraka na kwa kila mwenye uhitaji aliepata dharura, hata hivyo tunatambua kwamba kuna mis-use ya hizi dawa hasa kwa Watoto wa Shule ambao kwa sasa inaonekana wanaogopa zaidi mimba kuliko UKIMWI!, matumizi holela ya P2 yanaweza kuzalisha matatizo mengine makubwa ya kiafya kwa wasichana/wanawake"

"Wataalam wetu wamenihakikishia kuwa matumizi holela na ya mara kwa mara ya P2 yanaweza kusababisha ugumba na saratani, tunaendelea kuliangalia suala hili kwa mapana yake, wakati tunaendelea kulijadili ndani ya Serikali na wadau, hatua ya haraka tutakazo kuchukua ni kuongeza kasi ya utoaji elimi ya juu ya madhara ya matumizi holela ya dawa hizi (P2)”

"Nimeshawaelekeza timu yangu kulitekeleza hili haraka, nasi Wazazi/Walezi tusione aibu kuwaeleza mabint zetu madhara ya ngono za mapema na kuepuka ngono zisizo salama, kama Binti/Msichana unaona hupo tayari kuzaa basi unashauriwa kutumia njia za uzazi wa mpango na siyo P2" ——— Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Screenshot_20220215-170428_Instagram.jpg
Screenshot_20220215-170450_Instagram.jpg
 
Daktari Bingwa wa mishipa ya fahamu na utindio wa Ubongo Dr. Yusuf Jamnagerwalla amesema ulaji wa nyama ya nguruwe maarufu ‘kitimoto’ husababisha kifafa iwapo hakijapikwa vizuri.

"Ugonjwa wa kifafa unatibika, ukimwona Mtu ana dalili za kifafa asifikirie kwamba amelogwa au ana mashetani/mapepo hapo ndio kila kitu kinaharibika, ukiona dalili hizo nenda kituo cha afya na kuwaachia Wataalamu wafanye kazi yao na mgonjwa atapatiwa matibabu na madawa yapo"

"Kila Jumatatu ya pili ya Februari ni siku ya kifafa na kuna Watu zaidi ya milioni 95 wanaishi na ugonjwa wa kifafa ambapo kato yao 60% hadi 70% wako kwenye nchi masikini na Nchi zinazoendelea, changamoto kubwa ni upatikanaji wa dawa"

"Kuna uhusiano kati ya ugonjwa wa akili na kifafa lakini sio wote wenye ugonjwa wa akili wana kifafa ila dalili za ugonjwa wa akili zinafanana na za ugonjwa wa kifafa" ——— Dr. Yusuph Nyamnagerwalla. via Clouds360.
Screenshot_20220215-170944_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom