Makapuku Forum

Makapuku Forum

"Katika mazungumzo yetu niliwataka wenzangu pamoja na mambo mengine kujiimarisha kiuchumi, tulipe kodi na tulipe tozo ili tuisaidie Serikali yetu katika kujitegemea zaidi na sisi kama Nchi kujitegemea zaidi na nikaeleza kwanini sisi Wabunge tulipitisha jambo hili la tozo na nikasema endapo wenzetu mnatuona Wabunge tulifanya jambo baya kupitisha jambo hili basi mtatuhukumu huko mbele, Wabunge sikumaanisha Taasisi nyingine yoyote"

Juzi tarehe 26 nilikuwa kwenye shughuli nikazungumza baadhi ya mambo baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya Watu wakakata baadhi ya mambo wakawasilisha ujumbe nusu ambao umesababisha mjadala mkubwa katika Nchi yetu mjadala ule umesababisha usumbufu wa hapa na pale nimeona tukutane pamoja na mambo mengine niweke sawa jambo hilo lilivyokuwa" ——— asema Spika Job Ndugai
Screenshot_20220103-120811_Instagram.jpg
 
"Binafsi yangu popote pale ambapo nilihisiwa labda kwa namna moja ama nyingine nimetoa neno la kumvunja moyo Rais wetu na akavunjika moyo nitumie fursa hii kumuomba radhi Mheshimiwa Rais na Watanzania wote, haliwezi kutokea halitotokea na sio rahisi jambo hilo kutokea, Rais ndio Kiongozi Mkuu, tumuheshimu pekee yake hatoweza tumsaidie kwasababu pamoja tunaweza kwenda mbali zaidi"

"Wabunge mtawasikia wapo na Rais, na sisi wote tunatekeleza sera na Ilani za CCM hatugombani hata siku moja lakini wapo Watu ambao wangependa kupita katikati na kutusambaratisha, Watu hao washindwe na walegee” ——— asema Spika Job Ndugai
Screenshot_20220103-122811_Instagram.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || BRANDING.
.
Sura ya nje ya Taasisi ni ishara ya namna Taasisi zinafanya kazi kutoka ndani. Namna Taasisi inavyozungumzwa ndivyo kwa asilimia kubwa inaathiri namna yake ya utendaji. Hivyo katika moja idara muhimu ni idara ya Mahusiano na Mawasiliano, mtu anayeteuliwa kuisemea Taasisi ni lazima awe mtu anayeenda mbele kuiheshimisha Taasisi.
.
Kuna kauli mbaya sana huwa naiongea, sio kama nawadharau watu hapana ila naongelea matokeo ya wao kuwa kwenye nafasi fulani. Football ya Tanzania imejaa MASELA katika kila Idara, uongozi, makocha na hata wanaozisemea klabu nyingi ni watu wa Hovyo na wanaongea hovyo hovyo wakifikiri ndio namna nzuri ya kuzisemea klabu zao.
.
Niliwahi kusema kua klabu ya Simba inapambana sana kuondoa picha ya USELA kwenye namna ya kuiongoza klabu yao. Simba imeamua kutengeneza Taasisi inayoheshimika na sio Taasisi inayosemeka sana, CREDIBILITY ndio kitu ambacho Simba imeamua kutengeneza na kiukweli inawasaidia sana kuifanya Simba ya kibiashara.
.
Hongera Simba kwa Kumpata Ahmed Ally na Hongera Ahmed unakwenda kufanya kazi na Taasisi ambayo inafanya TRANSFORMATION ya uendeshaji, wameona unafaa kuisemea Klabu yao na kuimbia DUNIA mazuri ya Simba.
.
NB:
Naamini sitosikia ahadi za kutembea UCHI mitaa ya Dar Es salaam.
.
Screenshot_20220103-111501_Instagram.jpg
 
"Tuko vizuri tunaenda vizuri sana , tuko mikono salama kabisa ya Mama yetu (Rais Samia Suluhu) na hakuna mgogoro hakuna migongano mahali, wewe utaona migogoro iliyopo ni ya kwenye mitandao tu haipo kama kuna shida mahali tuambieni, Nchi imetulia kabisa, Nchi iko vizuri kabisa, hivi vitu ni vitu vya kutengeneza tu, Dunia ya sasa ndio hiyo Watu wanaweza kutengeneza vitu vikamshughulisha kila Mtu lakini ni ufundi wa kutengeneza maneno ya hapa na pale"

"Walioguswa visivyo wote nawaomba sana radhi kwa mara nyingine lakini niwahakikishie Mimi ni yuleyule uimara wangu uko palepale na Mungu atakuwa nasi tutafika salama kabisa" ——— asema Spika Ndugai, tazama yote aliyosema kupitia youtube ya millardayo.
Screenshot_20220103-124550_Instagram.jpg
 
"Nimefurahi sana kujiunga na Simba, ni ndoto ya kila Mtu kufanya kazi na Taasisi kubwa kama Simba, ni furaha kujiunga na Taasisi yenye mafanikio makubwa"

"Nitafanya kazi hii kwa kujituma, nitafanya kazi kwa weledi, niwaambie Wanachama na Wanasimba wote kwamba hapa mmepata Mtu"

"Wanasimba msiwe na wasiwasi, Timu yetu ipo vizuri, kufika kileleni jambo la muda na tukifika hatutoki hadi tunachukua ubingwa" ——— Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally
Screenshot_20220103-200103_Instagram.jpg
 
"Wanasimba karibuni Zanzibar kwenye Mapinduzi Cup, tukutane Amaani Stadium siku ya Jumatano kwenye mchezo wa kwanza"

"Kwasasa tuna jukumu kubwa la kuchangia ujenzi wa uwanja wetu, ni jukumu letu Wanasimba wote, wapo Watu wanataka kutukatisha tamaa lazima sisi hatutakata tamaa, Rais wa heshima na Mwekezaji, Mo DEWji ameshaahidi kutoa Bilioni 2 na sisi tuunge mkono"

"Nimekuja na jambo kubwa huku Zanzibar, jambo hilo ni uzinduzi wa jezi mpya ambazo tutazitumia kwenye michuano ya Kombe la FA na Kombe la Mapinduzi" ——— Afisa Habari wa Simba SC , Ahmed Ally
Screenshot_20220103-210920_Instagram%20Lite.jpg
 
Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete imethibitisha kutokea kwa kifo cha Katibu wa Rais Mstaafu, Adam Issara kilichotokea jana jioni Jijini Dar es Salaam.

Adam Issara alifariki akiwa katika Hospitali ya Dr. Mvungi jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ambapo taratibu za msiba na mazishi zitatolewa punde.

"Wakati wa uhai wake, Ndugu Adam Issara alikuwa Mtu mwaminifu, muadilifu, mchapa kazi hodari na nguzo muhimu ya Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kabla ya kujiunga na Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu mwaka 2017, Adam Issara alifanya kazi katika iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa Afisa Dawati katika Idara ya Asia na Australasia, na baadae kuwa Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kati ya mwaka 2007 na 2017"

"Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na familia yake wanaungana na mjane wa Marehemu, Bi. Happy Godfrey, familia ya Marehemu Adam Issara katika kipindi hiki cha simanzi na maombolezo, Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema, peponi" Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne
Screenshot_20220104-120640_Instagram.jpg
 
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza matengenezo ya dharura ya umeme katika maeneo ya Ubungo-Makumbusho.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema matengenezo hayo yanafaanyika ili kubadilisha waya wenye hitilafu ili kuepusha madhara kwenye mfumo wa umeme huku likitaja maeneo yatakayoadhirika kuwa ni Masaki, Msasani, Mikocheni, Sinza, Kawe, Lugalo, Mwenge, Kijitonyama, Regent, Makumbusho, Victoria, Mwananyamala, na maeneo ya viwanda mikocheni.

“Tafadhali usishike nyaya wala kukanyaga waya uliokatika, Toa taarifa Ofisi ya Tanesco iliyo karibu nawe au piga simu samba 0748550000,” imesema tariff hiyo.
Screenshot_20220104-120804_Instagram.jpg
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimesema kitendo cha Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kujitokeza hadharani na kukiri mapungufu na kutoa ufafanuzi kuhusu kauli yake juu ya suala la mikopo ya nchi na kuleta taharuki, sio kujidhalilisha bali kujiimarisha.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha leo Jumanne Januari 4, 2021 Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo, Ramadhani Meneno amesema kitendo hicho cha Spika Ndugai kijitokeza hadharani chama kinaamini ni cha kijasiri na kiungwana.
Screenshot_20220104-120914_Instagram.jpg
 
Shirika la Kutetea Haki za Wahamiaji limesema zaidi ya wahamiaji 4,000 wamepoteza maisha au kutoweka walipokuwa wakijaribu kufika nchini Hispania wakisafiri kwa nija ya majini kwa mwaka 2021.

Miili ya idadi kubwa ya wahamiaji, asilimia 94, haikupatikana kwa hivyo inahesabiwa kuwa haipo.

Wahamiaji wanaowasili katika Visiwa vya Kanari vya Hispania katika Atlantiki wameongezeka tangu mwishoni mwa mwaka 2019 baada ya kuongezeka kwa doria kwenye pwani ya kusini mwa Uropa kupunguza kwa kiasi kikubwa vivuko vya bara hilo kupitia Bahari ya Mediterania.
Screenshot_20220104-121008_Instagram.jpg
 
Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi na mkewe Isaura wamekutwa na maambukizi ya virusi vya Uviko-19.

Tarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais huyo jana Jumatatu Januari 3, 2021 inasema kuwa Rais Nyusi na mkewe wamejitenga baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo.
Screenshot_20220104-121748_Instagram.jpg
 
Wizara ya Ujenzi imesema kuchelewa kukamilika kwa barabara ya njia nane (Kimara - Kibaha) kumetokana na maboresho yaliyoongezwa kwenye mradi huo.

Mboresho hayo ni pamoja na ujenzi wa madaraja ya juu kwa waenda kwa miguu Mbezi kwa Yusuf na flyover kwenye makutano ya barabara ya Goba na Mbezi.

Serikali imeongeza TZS bilioni 56 kwa ajili ya maboresho kwenye mradi huo wenye urefu wa 19.2km.
Screenshot_20220104-123045_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom