Makapuku Forum

Makapuku Forum

"Ni imani yangu kwamba hadi kufikia January 15,2022 madarasa yatakamilika kama Waziri Ummy alivyosema na January 17,2022 Watoto wetu waingie madarasani, na naamini madarasa yatakabidhiwa bila kuwa na harufu ya rangi ili wasije kupaliwa tukazalisha matatizo mengine"

"Niwashukuru Viongozi wote kwa usimamizi mzuri uliofanyika kwenye mradi huu, na nawashukuru Wenyeviti wa CCM kwa kusimama na kutetea Mkopo ulioleta maendeleo, walipotokea wa kuhoji mlisimama mkajibu mkijua kwamba kinachofanyika ni utekelezaji wa Ilani, Ilani ile wenyewe ni nyinyi na sasa mna mambo ya kwenda kifua mbele kwa Wananchi kuwaambia Chama kimefanya hiki"

"Niwashukuru wote wengine waliokuwa wanajibu kwenye mitandao n.k, Gavana wa Benki Kuu na Timu yake wakakaa kwenye TV na kufanya ufafanuzi mzuri sana kuhusu mikopo, uwezo wa kukopa, deni tulilonalo na uwezo wa kulipa" ———Rais Samia, Ikulu Dar es salaam leo
Screenshot_20220104-184209_Instagram.jpg
 
• "Hakuna siku Mtanzania mmojammoja atagongewa hodi mlangoni kwamba tunakudai Shillingi hizi kwasababu Nchi yako ilikopa haipo Nchi hiyo, hivi ni vitu vya Kitaasisi na vinaangaliwa kutoka kwenye mapato ya Kiserikali

"Hakuna siku Mtanzania atafuatwa aambiwe wewe una ng'ombe wengi sana toa mmoja tulipie deni la Taifa haipo siku hiyo, inalipiwa kwenye mapato ya Serikali" ——— Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba leo Ikulu.
Screenshot_20220104-184344_Instagram.jpg
 
"Mbali na fedha za Uviko kuna fedha ya tozo ambayo na yenyewe ilipoanza ilipigiwa kelele tukasema tupunguze baada ya kupunguza kelele zimeshuka, lakini Wapigaji kelele hawa wa sasa hivi waliuliza kuna fedha ya tozo kwanini tumekwenda kukopa, takwimu zilizotolewa na Mawaziri hapa zinaeleza kwamba pamoja ya kwamba tuna tozo mahitaji ya madarasa Shule ya msingi ni Elfu 10 na Watoto tunazidi kuwaleta tumeweza madarasa 500 kwa fedha za tozo, ni lazima tukope"

"Inashangaza kuona Mtu mwenye uelewa anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa kwanini? au kwanini tunaendelea na tozo wakati kuna mkopo, Mawaziri msione uvivu kutupa takwimu toeni elimu mliyoisema hapa, Watu wajue inawezekana kweli hawajui" ——— Rais Samia Ikulu Dar es salaam leo
Screenshot_20220104-184443_Instagram.jpg
 
• "Nimeweka Watu ninaowaamini mtanisaidia kazi, huu ni Mwezi wangu wa nane, nilisema nilikuwa nawasoma na nyinyi mnamisoma na siku niliyofanya mageuzi kidogo nikasema hapa nimeweka comma, kazi inaendelea"

"Nataka niwaambie nitatoa list mpya hivi karibuni, wale wote ninaohisi wanaweza kwenda na Mimi kwenye kazi ya maemdeleo ya Watanzania nitakwenda nao lakini wale wote ninaohisi ndoto zao ni kule na wanafanya kazi kwa ajili ya kule nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje kwasababu nikiwatuma ndani itawasumbua, kwahiyo bora niwape nafasi wakae nje tukutane uko mbele ya safari" ——— Rais Samia Suluhu Hassan leo IKULU.
Screenshot_20220104-184608_Instagram.jpg
 
"Kelele za wanaopiga kelele hazinishughulishi, mmerudia hapa Mama usivunjike moyo, moyo wangu Mimi sio wa glass ni moyo wa nyama ulioumbwa na Mungu kwahiyo nishikeni mkono twende na Watanzania"

"Nawaambia nitajitahidi nitakavyoweza kila fursa itakayoletwa kutoka Duniani ambayo naweza kuitumia kuleta maendeleo Tanzania nitaitumia na nafanya hivi kwasababu niliapa kwa Mungu nitaitumikia Tanzania na wala sifanyi kwa ajili ya mwaka 2025" ——— Rais Samia Suluhu Hassan leo IKULU.
Screenshot_20220104-184900_Instagram.jpg
 
"Kwa upande wa tozo Bilioni 7 tumezielekeza kwenye Sekta ya Elimu Msingi, na hapa tumejenga madarasa 560 na kwenye hili napenda kufafanua kwasababu kuna sintofahamu kwamba fedha za tozo zinaenda kufanya nini na fedha za mkopo zinaenda kufanya nini!?, fedha za tozo tulizopokea Bilioni 7 tumekwenda kukamilisha ujenzi wa maboma ya madarasa 560 ili kuwaunga mkono katika maeneo mbalimbali ambao wametumia nguvu kazi yao kujenga maboma ya madarasa, maboma haya yapo zaidi ya Elfu 10 kwahiyo hata hii fedha ambayo tumepeleka ni ndogo"

"Takwimu zinaonesha mwakani ndio tutakuwa na Wanafunzi wa kwanza ambao wataanza Sekondari kufuatia sera ya Elimu bila malipo, mwakani wakifaulu kwa kiwango cha 82% tutakuwa na ongezeko la Wanafunzi wa Kidato cha kwanza zaidi ya Laki 7, Rais usije ukakatishwa tamaa katika kutafuta fedha kwa ajili ya kutatua kero za Watanzania kwasababu mahitaji ni makubwa sana"

"Mh. Rais sambamba na fedha nyingi ambazo unatupatia kutoka kwenye vyanzo mbalimbali tutasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri, katika mwaka wa fedha wa 2021/22 Mamlaka za Serikali za Mitaa zilipanga kukusanya Tsh.Bilioni 863.85 na hadi November 30,2021 zimekusanywa Bilioni 356.72 kati ya lengo la kukusanya lengo ambalo tulijiwekea"

"Ujumbe wetu kwako Rais pamoja na Watanzania ni kwamba hatutokuangusha, nakushukuru Rais kwa jinsi unavyoguswa kwa kutatua haraka changamoto za Watanzania, nawashukuru pia Viongozi wengine na Watanzania wote" ——— Waziri Ummy mbele ya Rais Samia Ikulu Dar es salaam leo
Screenshot_20220104-185047_Instagram.jpg
 
"Ni jambo ambalo sio la kiungwana kukaa kusema Rais amekaa miezi tisa amekopa, Marais hawakopi ni Serikali ndio inakopa, hili sio jambo la Familia ni jambo la Nchi ndio maana yeye katika miezi tisa yake aliyokaa kila Mwezi analipa zaidi ya Bilioni 800 kwa ajili ya madeni, madeni mengine ya Awamu zilizopita, ni madeni ya Nchi na ni madeni ya Serikali lakini sio deni la Familia mojamoja"

"Sasa ukiwa unataja tu kwamba Rais wa Awamu ya Tatu alikopa akajenga Uwanja wa Ndege alipoondoka aliondoka na Uwanja wa Ndege ule!?, nyinyi mliopo mtalipa deni hilo na nyinyi ndio mnatumia Uwanja wa Ndege"

"Mh. Rais Samia wale wasiotambua kwamba unafungua uchumi ili Watoto wao wapate ajira wataendelea kuelewa hayo unayoyafanya siku ukifungua uchumi biashara zikakua Watoto wao wakapata ajira, utakapoiunganisha Nchi yetu ikapata fursa na uchumi ukakua watatambua kwamba hiki ulichokiwa unakifanya kina maana gani!?"——— Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba mbele ya Rais Samia Ikulu Dar es salaam leo
Screenshot_20220104-185215_Instagram.jpg
 
"Hakuna siku Mtanzania mmojammoja atagongewa hodi mlangoni kwamba tunakudai Shillingi hizi kwasababu Nchi yako ilikopa, haipo Nchi hiyo, hivi ni vitu vya Kitaasisi na vinaangaliwa kutoka kwenye mapato ya Kiserikali"

"Hakuna siku Mtanzania atafuatwa aambiwe wewe una ng'ombe wengi sana toa mmoja tulipie deni la Taifa haipo siku hiyo, inalipiwa kwenye mapato ya Serikali"——— Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba mbele ya Rais Samia Ikulu,Dar es alaam leo
Screenshot_20220104-185315_Instagram.jpg
 
"Nataka niwaambie nitatoa list mpya [ya mawaziri] karibuni. Wale ninaohisi wanaweza kwenda na mimi...nitakwenda nao. Lakini wale wote ninaohisi ndoto zao ni kule, na wanafanya kazi kwa ajili ya kule, nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje."- Rais Samia Suluhu
Screenshot_20220104-185546_Instagram.jpg
 
"Wakati mmenikabidhi huu mzigo, nilianza kusikia lugha zinasema serikali ya mpito, serikali ya mpito bungeni huko kwa kina Kassim. Nikarudi kwenye Katiba kuangalia serikali ya mpito imeandikwa wapi...sikuona. Nikasema 'anhaa, twendeni.'"- Rais Samia Suluhu
Screenshot_20220104-185546_Instagram.jpg
 
"Sifanyi kwa ajili ya [uchaguzi wa] 2025, nafanya nimeapa kuleta maendeleo kwa Watanzania."

- Rais Samia Suluhu Hassan akieleza sababu ya kujituma kutekeleza miradi ya kijamii na maendeleo
Screenshot_20220104-185546_Instagram.jpg
 
"Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025."- Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Tanzania kukopa
Screenshot_20220104-185546_Instagram.jpg
 
"Nawashukuru wenyeviti wa CCM kwa kusimama na kutetea mkopo ulioleta maendeleo kwenu. Walipotokea wakuhoji mlisimama mkajibu, mkijua kwamba kinachofanyika ni utekelezaji wa ilani.

Sasa mna mambo ya kwenda kifua mbele kwa wananchi kuwaambia CCM imefanya."- Rais Samia Suluhu
Screenshot_20220104-185546_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom