Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220102-063912_Opera%20Mini.jpg
 
Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki.

Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Afisa Habari na Mawasiliano.
Screenshot_20220103-111501_Instagram.jpg
 
"Juzi tarehe 26 nilikuwa kwenye shughuli nikazungumza baadhi ya mambo baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya Watu wakakata baadhi ya mambo wakawasilisha ujumbe nusu ambao umesababisha mjadala mkubwa katika Nchi yetu mjadala ule umesababisha usumbufu wa hapa na pale nimeona tukutane pamoja na mambo mengine niweke sawa jambo hilo lilivyokuwa"

"Nyinyi Waandishi mnaweza kufuatilia mkapata mkanda mzima, hapakuwa na jambo la kukashfu au kudharau juhudi zozote za Serikali, Serikali ni Baba yetu, Serikali ni Mama yetu tunahitaji Serikali na tunaiunga mkono" ——— asema Spika Job Ndugai Live muda huu Dodoma.
Screenshot_20220103-120233_Instagram.jpg
 
Mgonjwa wa kwanza mwenye mchanganyiko nadra wa magonjwa mawili ambayo ni mafua na coronavirus mchanganyiko ambao unaitwa "flurona" amegundulika nchini Israel, taarifa imesema Mgonjwa huyo ni Mwanamke mjamzito ambaye alikuwa hospitalini.

Mitandao mbalimbali imeripoti kwamba kugundulika kwa Mgonjwa Mtaalamu kumefanya Nchi mbalimbali kuanza kuwapa tahadhari Wananchi wake ikiwemo Australia ambako Mkuu wa magonjwa ya kuambukiza amewakumbusha Raia wa Nchi hiyo kwenda kupata chanjo za nyongeza baada ya uthibitisho kwamba sasa Watu wanaweza kupata COVID-19 na mafua kwa wakati mmoja.

Wataalamu wa afya wanasema Mwanamke huyo mjamzito nchini Israel anaaminika kuwa mgonjwa wa kwanza duniani aliyeshikwa na mafua na virusi vya corona vyote kwa wakati mmoja lakini hata hivyo Wataalamu wanaendelea kutafiti zaidi ili kubaini kama mchanganyiko huo unaweza kusababisha ukali wa ugonjwa.
Screenshot_20220103-120416_Instagram.jpg
 
Mwanamke mmoja kutoka mji wa California nchini Marekani, Fatima Madrigal amejifungua watoto mapacha wawili waliopishana dakika 15, mmoja akizaliwa mwaka 2021 na mwingine mwaka 2022.

Fatima na mumewe Robert Trujillo walipata watoto hao ambapo mmoja wa kiume alizaliwa Desemba 31 majira ya saa 5:45 usiku aliyepewa jina la Alfredo na baada ya dakika 15 ambayo ilikuwa ni saa 6 usiku na siku nyingine mpya na mwaka mpya wa 2022 walipata mtoto mwingine wa kike aliyepewa jina la Aylin.

"Kwangu ni ajabu kuwa hawa ni mapacha lakini si was siku wala mwaka mmoja," alisema Fatima katika taarifa iliyotolewa na hospitali alipojifungulia.
Screenshot_20220103-120537_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom