Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,077
- 464,004
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kocha Pablo Franco aliwasilisha ripoti akiweka bayana alichokiona tangu alipotua klabuni hapo, huku akitaja majina ya kufyekwa na vitu vinavyotakiwa kuboreshwa ikiwamo wachezaji wapya watatu ambao ni wakali kuliko waliopo kwa ajili ya michuano ya ndani na ya kimataifa.
Inaelezwa kuwa, huenda Simba ikaachana na wachezaji watatu wa kigeni wanaoweza kutolewa kwa mkopo ili nafasi zijazwe na majembe watatu wanaotakiwa, huku wanaotajwa ni beki wa kati Pascal Wawa, Duncan Nyoni na Pape Ousmane Sakho.
Simba imetinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuing’oa Red Arrows ya Zambia na Kocha Pablo anataka kuhakikisha inafika mbali zaidi kuliko msimu uliopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilipoishia ya robo fainali.
Taarifa zaidi zinasema Pablo katika usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa jana ametaka kiungo mshambuliaji (namba 8) mwenye uwezo zaidi wa Sadio Kanoute anayecheza nafasi hiyo mara kwa mara.
Pia amependekeza washambuliaji wa kati watakaocheza pacha yaani namba 9 na 10 wenye uwezo mkubwa wa kutupia nyavuni kuliko Meddie Kagere, John Bocco na Chriss Mugalu.