Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211217-111827_Instagram%20Lite.jpg
 
Madereva wa magari ambao wamekuwa wakisafiri kwenda majumbani mwao msimu huu wa sikukuu ikiwemo wenye IST wameonywa kuwa makini na ikiwezekana wale wasio na uzoefu kuacha kuendesha magari hasa kwenda umbali mrefu msimu wa sikukuu.

wenye ist zenu mnapata sana shida nchi hii
Screenshot_20211217-162407_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kwa muda usiojulikana kipindi cha Shule ya Uongozi kinachomilikiwa na Mbunge, Humphrey Polepole kwa makosa matatu likiwemo la kutoa taarifa ya upotoshaji kuhusu chanjo ya Uviko 19.

TCRA imesema pia imeamua kukifungia kituo hicho kinachorushwa kupitia mtandaoni kwa kutoa maneno ya uongo na udhalilishaji kuwa viongozi wengi waliyopo katika Serikali ya Awamu ya Sita ni waoga kusema ukweli kuhusu deni la taifa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui TCRA, Hans Gunze amesema leo Ijumaa Desemba 17, 2021 kuwa kosa lingine lililofanywa katika kipindi hicho ni kurusha maudhui yasemayo viongozi wa mikoa hawajafuata utaratibu wakati wa kuwahamisha machinga ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha badala yake ilikuwa ni dhuluma na unyanyasaji.
Screenshot_20211217-162555_Instagram.jpg
 
Kocha Msaidizi wa timu ya Simba, Selemani Matola amesema robo tatu ya wachezaji wa timu hiyo wanakabiliwa na ugonjwa wa mafua, kifua pamoja na homa.
Screenshot_20211217-162703_Instagram.jpg
 
"Jana nimepima nakukutwa na virusi vya Korona (COVID 19). Sina maumivu yoyote mpaka sasa zaidi ya mafua tu lakini nimekutwa positive.

Chanjo imesaidia kutopata madhara makubwa. Nimekaa eneo tengwa (isolation) ili kutoambukiza wengine mpaka hapo nitakapopima tena.

Nawaomba muendelee kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kunawa maji tiririka na kujiepusha na mikusanyiko.

Corona bado ipo, chukua tahadhari na walinde wengine"
Screenshot_20211217-162804_Instagram.jpg
 
Mvua zinazoendelea katika mikoa ya Dar na Pwani zimechangia kuongezeka kiasi cha maji katika bonde la mto Ruvu n kupunguza mgao.

Sambamba na mvua, oparesheni zilizofanywa kuwaondoa walioingilia mto huo na kuchepusha maji zimechangia kuongeza maji yanayokuja Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji ,Mhandisi Nadhifa Kemikimba wakati akifungua mkutano wa wadau wa maji kujadili namna ya kutunza bonde la mto Ruvu ambalo ndio chanzo kikuu cha maji kwa jiji la Dar.
Screenshot_20211217-162905_Instagram.jpg
 
Mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyotolewa na upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu na kupokea hati ya ukamataji mali.

Mbowe na wenzake hao, Halfan Bwire, Adamu Kasekwa na Mohamed Ling’wenya wanakabiliwa na kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Joachim Tiganga.

Uamuzi huo unahusu mapingamizi mawili ya mawakili wa utetezi katika kesi hiyo ambayo ni orodha ya vielelezo na mnyororo wa utunzaji vielelezo.

Akitoa uamuzi huo leo Ijumaa Desemba 17, 2021 Jaji Tiganga amesema mahakama inapokea kielelezo hicho na kinakuwa ni kidhibiti cha 14.
Screenshot_20211217-163004_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom