Makapuku Forum

Makapuku Forum



Mikono ya kihamu ya Farhan Jr

NIMEONA NINI SIMBA VS TP MAZEMBE?

Ni kwanza matokeo ya mahusiano! Nilisema kwenye NETWORKING wiki kadhaa nyuma! Nikasema CLUBS VS CLUBS (klabu dhidi ya Klabu)

Wakati CEO wa Simba alipiga picha na Mmiliki wa TP Mazembe ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa klabu duniani, Moise Katumbi Chapwe! Ni sehemu ya kujenga mahusiano yao

Mazembe aliwahi kuja nchini kwa SIMBA SUPERCUP! Sio rahisi kuileta klabu Tajiri nchini kwetu na ikacheza michuano bali ni matokeo ya mahusiano yenu mazuri

Niwape mifano ya duniani kote kuna mechi nyingi zinachezwa kuelekea msimu mpya kama ambavyo Simba Day wanayo yao hapa nchini

FC Barcelona wana mechi ya kombe inafahamika kama JOAN GAMPER ama JOAN GAMPER TROPHY! Mechi zao zinahusisha timu ambazo wao wana mahusiano nayo tu na sio timu ambazo hawana link nazo

Msimu huu wamecheza na Juventus, wana mahusiano mazuri sana tangu EUROPEAN SUPERLEAGUE! Licha ya kuwa Juventus hakuwa na msimu mzuri ila bado ni Juventus

Hakuna michuano nje ya inayoandaliwa na Mashirikisho ikahusisha watu ambao hawana mahusiano! Kuna Audi Cup ya Bayern Munich, kuna Emirates Cup ya Arsenal zote zinahusisha wale wenye mahusiano

Simba kumleta TP Mazembe nadhani ni hatua kubwa licha ya kuwa hawakuwa vizuri msimu uliopita lakini bado ni TP MAZEMBE tusisahau

TP MAZEMBE ipo nchini Morocco kwasasa, tayari hao Mazembe tunasema wabovu lakini wamecheza mechi na miamba WYDAD CASABLANCA, hao hao Mazembe tunaosema wabovu wanaanza hatua ya pili Klabu bingwa Afrika

Hao Mazembe tunaosema ni wabovu ila wapo nafasi ya tano kwa ubora Afrika wakiwa na points 1572, Mazembe tunaosema wabovu wamebeba Ligi ya Congo mara tatu mfululizo mpaka sasa

Wabovu hiyo kwioo??

View attachment 1929248
huyu kijana mikono yake na kichwa chake ni hatar
 
Nyieee mmewaona Simba tukutane simba day
Screenshot_20210908-205322_Instagram%20Lite.jpg
 
| ABDI BANDA MTIBWA SUGAR
.
Done Deal. Beki Abdi Banda aliyekuwa anacheza soka la kulipwa nchini Afrika kusini amejiunga rasmi na klabu ya Mtibwa Sugar inayoshiriki Ligi Kuu nchini.

Huyu bwana asingetusemea hovyo simba tungemfikiria tungemuweka hata benchi akiba ya maneno ni nzuri

Ooh sizitaki mbichi hizi haya kiko wapi mjifunze kwa banda jamani
Screenshot_20210908-211812_Instagram.jpg
 
| Wachezaji NANE raia wa Brazil wanaocheza katika Ligi Kuu England wamesimamishwa wikendi hii kuvitumikia vilabu vyao baada ya Shirikisho la soka la Brazil kuweka pingamizi Fifa kuwazuia wasicheze.
.
  • T Silva
  • Fred
  • Firmino, Allison, Fabinho
  • Ederson, Jesus
  • Raphinha
.
(Richarlison anaweza kucheza)
Screenshot_20210908-212729_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Manyara, linamshikilia Samwel Alfred (48), mkazi wa Kijiji cha Magara wilayani hapa kwa tuhuma za kumuua Michael Jackson (25) baada ya kumfumania akizini na mke wake, Habiba Saidi (22).

Mtuhumiwa huyo, inaelezwa kuwa alitekeleza mauaji hayo kwa kumkata kwa panga marehemu aliyemkuta akivunja amri ya sita na mkewe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP), Merrison Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea saa 10 alfajiri ya leo, Septemba 8.

Kamanda huyo amesema Alfred alimuaga mkewe Habiba saa 10 alfajiri kuwa anakwenda kukata kuni na kumuacha akiwa amelala lakini mkewe huyo akampigia simu hawara yake Michael Jackson aende nyumbani kwake wakafanye mapenzi.

“Baada ya Jackson kufika walizunguka kwenye banda la ng’ombe na kutandika mgorore chini na kuanza kufanya mapenzi ila ghafla mumewe akarudi na kuwafumania,” amesema Kamanda Mwakyoma.

Kwa sababu Alfred alikuwa na panga mkononi, kamanda alisema alilitumia kumkata sehemu mbalimbali za mwili mpaka akafariki dunia. Mkewe ambaye alikuwa anamzuia asiendelee kumjeruhi marehemu naye alikatwa mkono uliodondoka chini.
Screenshot_20210908-213132_Instagram.jpg
 
Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi la awali Serikali dhidi ya maombi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya kibali cha kufungua shauri la kupinga tozo kwenye miamala ya simu.

Hata hivyo wakati mahakama hiyo ikitupa pingamizi la Serikali, pia imeyatupa maombi kama hayo yaliyofunguliwa na Mwanaharakati Odero Charles Odero baada ya kukubaliana na hoja moja ya pingamizi la Serikali kuwa hati ya kiapo chake kilichokuwa kinaunga mkono maombi hayo ina kasoro za kisheria.

Uamuzi huo wa umetolewa leo Jumatano, Septemba 8,2021 na Jaji John Mgetta.
Screenshot_20210908-213348_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom