Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210825-065631_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210825-065811_Opera%20Mini.jpg
 
TRANSFER UPDATES| REAL MADRID MZIGONI KWA MBAPPE

Klabu ya Real Madrid imepeleka ofa rasmi kwa PSG ya Euro Million 160 ili kuinasa saini ya nyota huyo msimu huu wa majira ya kiangazi

PSG bado wana maamuzi yote juu ya hatma ya Mbappe na inasemekana wanataka kuipiga chini ofa hiyo, hawapo tayari kuuza

Mbappe amekataa ofa zaidi ya tatu za PSG na amewaambia wazi anahitaji kuondoka hivyo wakubali kumalizana na Real Madrid
Screenshot_20210825-083031_Instagram%20Lite.jpg
 
TRANSFER UPDATES| CRISTIANO NGOMA NGUMU

Wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes anapambana kupata timu ambayo mteja wake atacheza kuelekea msimu mpya

PSG hawana mpango na Ronaldo kwasasa, Manchester City wanaonekana kama sehemu ya yeye kwenda ila wao wanamtazama zaidi Harry Kane

Ikitokea City wamemkosa Kane, basi Ronaldo anaweza kuwa mbadala wake ila Juventus hawajapokea ofa yoyote mpaka sasa
Screenshot_20210825-083014_Instagram%20Lite.jpg
 
AME AAGA SIMBA KUTIMKIA KWA WALIMA MIWA
.
Beki Ibrahim Ame amefunguka baada ya uongozi wa Simba kumpa ruhusa ya kutafuta changamoto mpya kwenye timu nyingine.
.
Anatajwa kujiunga Mtibwa Sugar au Kagera Sugar kwa mkopo akitokea Simba: “Nimepewa nafasi ya kusaka timu ya kunipa changamoto msimu ujao baada ya kukaa benchi muda mrefu na tayari nipo kwenye mazungumzo na hizo timu
.
“Biashara pia walionyesha nia lakini dau lao halijaniridhisha hivyo ninachoweza kukwambia nitakuwa mchezaji wa walima miwa." amesema Ame.
.
Amesema mbali na kutaka kudhihirisha hilo pia lengo lake la kwenda kwa mkopo ni kuonekana na kupata nafasi ya kuitwa timu ya taifa huku akifafanua kuwa wachezaji wanaoitwa kikosi cha taifa haoni kama wanamzidi sana kiuwezo isipokuwa wao wanaonekana uwanjani na yeye amekuwa akikaa benchi.
Screenshot_20210825-084027_GBInsta.jpg
 
NABI: NIPENI MUDA BADO SIJAPATA MUUNGANIKO WA TIMU
.
Kocha mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi ametua nchini jana na kutamka kwamba bado hajapata muunganiko katika timu yake licha ya kuwa nchini Morocco kwenye maandalizi ya msimu mpya.
.
Akizungumza na waandishi wa habari, Nabi amesema; “Muunganiko wa timu bado, tunahitaji muda kama mwezi au miezi mitatu kwa sababu timu haijengwi kwa muda mfupi.
.
Wachezaji wote tuliowasajili ni wazuri kwa sababu tulikuwa tunawafuatilia, tukipata muda zaidi tutakuwa bora zaidi,” alisema Nabi.
.
Naye mshambuliaji Saido Ntibazonkiza alisema; “Kama kocha alivyosema muda ulikuwa mchache lakini tukiunganika vizuri tutakuwa bora zaidi, kikosi kipo vizuri.”
Screenshot_20210825-084148_GBInsta.jpg
 
Ruben Neves anukia Old Trafford
.
Manchester United inatarajia kuweka Pauni milioni 40 mezani ili kuipata saini ya kiungo wa Wolves na Ureno, Ruben Neves, 24, katika dirisha hili.
.
Kiungo huyo amekuwa mmoja kati ya wachezaji ambao kocha wa wababe hao Ole Gunnar Solskjaer anatamani sana kupata huduma zao katika dirisha hili. Mkataba wake unaisha 2024.
Screenshot_20210825-085034_GBInsta.jpg
 
Auba awekwa sokoni Arsenal
.
Arsenal ipo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza straika wao kutoka Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, 32, katika dirisha hili la usajili ikiwa mchezaji huyo atahitaji kuondoka klabuni hapo.
.
Arsenal inaonekana kupitia katika kipindi kigumu kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu ambayo imekuwa ikiyapata tangu kuanza kwa msimu huu ambapo haijashinda hata mechi moja.
.
Fedha ambazo itazipata kutokana na mauzo ya staa huyo ndizo inataka kuzitumia kusajili washambuliaji wengine inaowawinda sokoni hivi sasa.
Screenshot_20210825-085502_GBInsta.jpg
 
Man City nguvu zote kwa Kane
.
Manchester City imepanga kuwekeza nguvu zao zote kwenye dili la kumsainisha straika wa Tottenham Hotspur na England, Harry Kane, 28, kabla ya wiki hii kumalizika.
.
Kane ni miongoni mwa wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha Spurs na mabosi wa timu hiyo hawaonekani kutaka kumuachia kwa mkwanja wa chini ya ule walioweka kama bei yake.
.
Manchester City inahaha kuboresha eneo la ushambuliaji lililo na mapengo kwenye baadhi ya sehemu hususan ile ya straika. Mkataba wa Kane huko Man City unatarajiwa kumalizika majira ya kiangazi 2024.
Screenshot_20210825-085721_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom