Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210824-070317_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210824-070328_Opera%20Mini.jpg
 
Watu wawili wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa darasa katika shule ya msingi Muungano kata ya Muungano Halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara walipokuwa wakibomoa darasa bovu ili kujenga darasa jipya.

Waliofariki ni Ali Bakari Magongo aliyeacha Watoto wawili na Wake wawili pamoja na Issa Ali Libwaka aliyeacha Watoto nane na Wake wawili wote wakiwa ni Wakazi wa kijiji cha Muungano.

RPC wa Mtwara, Mark Njera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwapa pole familia zilizowapoteza wapendwa wao na kutoa wito kwa Jamii kutumia Wataalamu wa majengo katika kazi kama hizo ili kuepusha madhara kama haya.
Screenshot_20210824-183547_GBInsta.jpg
 
Jeshi la Marekani limesema limehamisha idadi kubwa ya Watu kutoka Afghanistan jana Jumatatu, lakini vurugu katika uwanja wa ndege wa Kabul zimeathiri kwa kiasi fulani zoezi la kuwahamisha watu zaidi.

Afisa katika Ikulu ya Marekani amesema ndege 28 za kijeshi zimewahamisha watu wapatao 10,400 kutoka Afghanistan katika muda wa saa 24 zilizopita. Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani Jake Sullivan, amesema kuwa mazungumzo yanaendelea kati ya utawala wa rais Joe Biden na kundi la Taliban juu ya njia zaidi za kuwahamisha watu wengi wakiwemo raia wa Marekani kutoka Afghanistan.

Hata hivyo kundi la Taliban limeonya kuwa huenda likazuia Watu kuondoka nchini humo.

Msemaji wa Taliban Suhail Shaheen katika mahojiano na runinga ya Sky News ameionya Marekani dhidi ya kurefusha muda wa mwisho wa Agosti 31 wa kuviondoa vikosi vyake vya jeshi na kuwa kufanya hivyo kunaweza kukawa na athari.
Screenshot_20210824-183748_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-183823_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-183907_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-183922_GBInsta.jpg
 
Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao walifariki kutokana na ajali alfajiri ya jana mkoani Songwe wameagwa leo mkoani Mbeya.

Wafanyakazi hao ni Benard Balagi Mushingi (40) Afisa Forodha (TRA Songwe), Azaria Asakwe Sivonike (42) aliyekua Dereva TRA Mbeya, Joel Isaya Mitondwa (36) Afisa Forodha TRA Mbeya, Said Mrisho Buddy (34) Afisa Forodha TRA Mbeya na Fahad Hassan Haji (26) Afisa Forodha Msaidizi TRA Mbeya. RIPNduguzetu
Screenshot_20210824-184138_GBInsta.jpg
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Faustine Ndugulile amesema kuanzia sasa ni namba 100 pekee ndio itatumiwa kuwapigia Wateja wa Kampuni mbalimbali za simu na sio namba za kawaida ili kudhibiti uhalifu wa mitandao.

“Wananchi tuepuke kutoa ushirikiano kwa namba za simu za kawaida za huduma kwa Wateja” 100 ndio namba pekee ya huduma kwa Wateja.
Screenshot_20210824-184254_GBInsta.jpg
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeweka utaratibu wa kutatua changamoto za muungano kupitia mfumo rasmi wa vikao vya kamati ya pamoja kati ya pande hizo mbili, Waziri Mwigulu Nchemba ametoa kauli hiyo akiwa Zanzibar baada ya kumaliza ziara ya ukaguzi wa kiwanda cha maziwa cha fumba na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.

“Fedha za Uhamiaji zinazotokana na shughuli za uhamiaji zinazopatikana Zanzibar zilikuwa zinahesabika kwenye bajeti za muungano na matumizi yake yalikuwa yanaidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini baada ya kuonekana hilo haliko sawa tulipitisha utaratibu kuwa sasa zitakusanywa Zanzibar na zinapangiwa matumizi Zanzibar”———-Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba
Screenshot_20210824-184430_GBInsta.jpg
 
Kesi ya unyang’anyi wakutumia silaha inayomkabili aliyekuwa DC wa Hai Lengai ole Sabaya Silvesta Nyegu pamoja na Daniel Mbura imemalizika usikilizwaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo Hakimu amesema hukumu itakuwa October 01,2021.
Screenshot_20210824-184556_GBInsta.jpg
 
Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa ameingia ukumbi wa Spika uliopo jengo la utawala saa 8.43 mchana huu kuhojiwa katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge huku akiwa na vitabu vingi, vingine akiwa amevishika mkononi na vingine akibeba kwenye begi na baada ya kufika ndani ya ukumbi alifungua begi ambalo lilikuwa na vitabu.

Baadhi ya vitabu alivyobeba ni pamoja na vitabu vya kodi na Biblia Takatifu.
Screenshot_20210824-184702_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-184722_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-184737_GBInsta.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza Rais Mpya wa Zambia aliyeshinda akiwa Chama cha Upinzani Hakainde Hichilema baada ya kuapishwa kuwa Rais wa 7 wa Zambia katika Uwanja wa Taifa wa Mashujaa Lusaka Zambia leo Aug. 24,2021.
Screenshot_20210824-184953_GBInsta.jpg
 
Watu nane wanashikiliwa na Polisi Morogoro akiwemo aliyekua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Asajile Mwambambale ambapo alihamishiwa Wilaya ya Gairo na wengine sita watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwa wizi wa Mabati 1,172.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu ameseme tukio hilo limetokea Juni 17, 2021 ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kuiba Mabati hayo kwenye stoo ya Halmashauri hiyo huku milango ikiwa haijavunjwa.

Kamanda Musilimu amesema Mkurugenzi huyo kwa kushirikiana na watumishi wa kutoka idara ya ugavi 4 wanne na Maderva watatu walipewa fedha kwa ajili ya kununua Mabati hayo lakini badae iliripotiwa kuwa Mabati yameibwa huku milango ya stoo haijavunjwa ambapo kwa sasa watuhumiwa wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa Mahakamani.
Screenshot_20210824-185108_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-185125_GBInsta.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia Watu 17 kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwemo utapeli wa fedha kwa kutumia madini feki.

Hatua hiyo inatokana na Oparesheni inayoendeshwa na Jeshi hilo ikiongozwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro.

Ayo TV na millardayo.com zimezungumza na Kamanda Muliro ambapo amesema Oparesheni hiyo inalenga kuzuia vitendo vya
kihalifu na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

"Oparesheni hii inahusisha vikosi vya mbwa na farasi,askari wa miguu,doria za magari na pikipiki imeleta mafanikio ikiwemo tukio la kukamatwa kwa Watuhumiwa 13 wa makosa ya
kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu (utapeli) wa madini bandia” ——— Muliro.
Screenshot_20210824-185739_GBInsta.jpg
 
Ukipenga pua yako bila kitambaa au shashi jijini Nairobi, upo katika hatari ya kutozwa faini ya kati ya Sh10,000 na Sh500,000 au kifungo cha kati ya miezi sita hadi 12.

Kaimu Gavana wa Nairobi Anne Kananu, pamoja na viongozi wa bunge la kaunti, wakati wa kusaini Mswada wa Sheria ya Kero ya Umma 2021 kuwa sheria. Picha: John Papanoo / Imani Imanyara.

Hii inatumika pia wakati unapokamatwa ukikojoa katika maeneo yasiyoruhusiwa, kutema mate barabarani, kulala jikoni na maduka ya chakula, kati ya makosa mengine. Muswada wa Sheria ya Kero ya Umma, 2021 Hizi ni sehemu ya sheria na kanuni mpya ambazo zinalenga kuliweka jiji la Nairobi safi. Sheria hizo zinapatikana katika Mswada wa Kero ya Umma ya Kaunti ya Jiji la Nairobi, 2021 ambayo sasa imesainiwa kuwa sheria.
Screenshot_20210824-190618_GBInsta.jpg
 
Ukitema mate Kenya faini 200,000
-
Kwa mujibu wa Sheria mpya zilizopitishwa katika Jiji la Nairobi nchini Kenya, iwapo utakutwa unatema mate au kupenga kamasi jijini humo basi utalazimika kulipa fedha ya Kenya KSh 10,000 sawa na Sh 200,000 za Kitanzania.

Sheria hiyo imekuja baada ya kaimu gavana wa Jiji la Nairobi, Anne Kananu kusaini kuwa sheria mswada wa Jiji wa kuzuia Usumbufu katika maeneo ya Umma wa 2020 .

Sheria hizo na kanuni zake nyingi zinalenga kuhakikisha kwamba Jiji la Nairobi linadumisha hali ya juu ya usafi .

Aidha, kwa mujibu wa sheria hiyo, u aweza kwenda jela miezi sita au kulipa faini KSh 50,000 iwapo wewe ni mwenyeji au mgeni katika jiji hilo usipokuwa mwangalifu unaweza kwenda jela iwapo utakutwa umelala jijini ambako hutayarishwa chakula cha kuuza.
Screenshot_20210824-190807_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amepiga marufuku mavazi yasiyo na staha wilayani kwake na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo.
Screenshot_20210824-190928_GBInsta.jpg
 
"Ricardo Kaka anapendwa sana na Mashabiki wa AC Milan, ana sehemu kubwa moyoni mwao, wamecheza watu wengi wenye vipaji kama Franco Baressi na Paolo Maldini ila Kaka ni juu yao wote" Adrian Galliani

Unakubaliana nae kuwa Kaka, ndie Mchezaji bora zaidi kuwahi kuvaa uzi wa Rosonneri?
Screenshot_20210824-191725_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom