
farhan jr
Kuna vitu viwili vinafanyika kwenye project ya Simba chini ya CEO wao, bahati mbaya sana kuna mambo yasio maana sana yanapewa maana kuliko mambo muhimu yanayoendelea
Umewatazama vyema SIMBA kwenye dirisha la Usajili??__ Kuna mzani unatengenezwa kati ya BIASHARA na MAFANIKIO, ili vyote viende kwa pamoja na vilipe
Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi mapato makubwa hivi sasa ni dirisha la usajili ikiwemo ndio maana TP Mazembe wao wana kitu kinaitwa PRINCIPLE OF PERCENTAGE RESALE, sio kwamba hawana pesa ila mizani
Well kuna siku niliandika kuhusu Wachezaji muhimu wa Simba kuuzwa lakini nikiri wazi nilitazama kwa jicho moja tu, sikufumbua macho zaidi
Ni hivi Simba wamefanya mauzo makubwa sana kwa ukanda wetu, pengine mauzo ya kihistoria, wameingiza pesa nyingi sana kutoka kwa Wachezaji waliowapa mafanikio
Ukiwa mzani wa pesa umetiki vipi kuhusu mzani wa Mafanikio??___ ndipo hapo uitazame vyema akili ya Simba! Yule Peter Banda alikuwa Sherrif (Mkopo) klabu inayoshiriki UEFA CHAMPIONS LEAGUE, ana Under 23 lakini kasaini Simba
Watazame saini zao zingine za kimataifa wana umri mdogo sana (Footballing age) wamesajili zile njaa za kuhitaji mafanikio, hivyo mafanikio binafsi ya Mchezaji ndio mafanikio ya klabu
Wamechukua nyota watakaoingia na kuipa mafanikio Simba kwa muda mfupi sana, kama hawatoondoka na kuwaingizia pesa ya muda mfupi basi ni project ya muda mrefu ya kufanya vizuri ndani na nje
Umewaelewa vyema??___ wana utajiri wa network, exposure na platform ya kuuza mali zao popote hii ni BIASHARA NA MAFANIKIO kwa mpigo
ITAENDELEA.....