Makapuku Forum

Makapuku Forum

Huyu ni Cristiano Ronaldo ana miaka 36 na bado anacheza mpira na kuvunja rekodi mbalimbali

Mind you kama unataka kuwa kama Ronaldo

-Siku ambazo hana mechi analala mishale ya saa nne

-Ronaldo hatumii kilevi wala vinywaji baridi

-Ronaldo hana tattoo mwilini kwakuwa anahitaji kuchangia damu

-Ronaldo anaingia wa kwanza mazoezini na wa mwisho kuondoka

-Ronaldo hali kabisa nyama (Red meat)

-Ronaldo ana Daktari wake, Trainer wake, Mwanasheria wake, Kocha wake (wa kumpa programs)

Unataka kuwa kama Ronaldo?
Screenshot_20210823-151446_GBInsta.jpg
 
Kwenye debut yake pale AS ROMA, Tammy Abraham amepiga Assists mbili

Alikuwa kwenye ubora mkubwa sana, ndio maana Chelsea wameweka kipengele cha Buyback

Labda baada ya Lukaku, kijana atarudi kuchukua jezi yake
Screenshot_20210823-151611_GBInsta.jpg
 
JUST IN | Baadhi ya nyota wa Simba na Yanga leo Agosti 23 wamegongana uwanja wa ndege wa Mohamed V uliopo jijini Casablanca, Morocco na wote wanarudi na ndege moja.
.
Wachezaji wa Simba ni wale ambao wameitwa kutumikia timu za taifa katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2022.
Screenshot_20210823-151843_GBInsta.jpg
 
Beckham aanza kumshawishi Messi
.
Mmiliki wa Inter Miami, David Beckham amefanya mazungumzo na Lionel Messi ili kumshawishi ajiunge na timu yake baada ya mkataba wake na PSG kumalizika mwaka 2023.
.
Miami ilitamani kuipata huduma ya mwamba huyo katika dirisha hili lakini dili lilifeli baada ya PSG kuweka ofa nono ya mshahara.
.
Messi aliwahi kuweka wazi
kwamba anatamani sana kucheza Ligi Kuu ya Marekani, ameripotiwa kukubali ofa hiyo na mara baada ya kumalizana na PSG atajiunga na wababe hao.
Screenshot_20210823-151955_GBInsta.jpg
 
"Tangu tufike hapa tumekuwa na changamoto ya hali ya hewa hapa Marrakech sasa kuna joto kali sana sasa tumeona ni bora timu irudi nyumbani ambako hali yake ya hewa hata kama kutakuwa na joto lakini sio kama la huku.
.
"Tuna ratiba pia ya mechi ya wiki ya mwananchi ambayo itafanyika wiki hii mwishoni lakini pia mnajua kwamba tuna mechi ya hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa palepale nyumbani kwahiyo sababu hizi tumeiona ni bora maandalizi yetu yakafanyike palepale katika kumalizia.
.
-Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM mhandisi Hersi Said.
Screenshot_20210823-152059_GBInsta.jpg
 
PIGO | WACHEZAJI 14 YANGA WAKUTWA NA CORONA
.
Habari za uhakika zinasema wachezaji 14 wa Yanga SC wamekutwa na maambukizi ya Corona na watakaa karantini nchini Morocco kuendana na itifaki za ugonjwa huo nchini humo.
.
Kundi moja la wachezaji ambao hawana maambukizi linarudi leo na jingine litarudi baadae baada ya kumaliza karantini au kubainika maambukizi yameisha.
Screenshot_20210823-152233_GBInsta.jpg
 
"Tumemsajili Jesus Moloko ni hatari zaidi ya Tuisila Kisinda."
.
"Uhamisho wa Kisinda umetulipa zaidi mbali na mauzo ya mchezaji lakini pia hata Kambi tuliyopo Morocco imetokana na mauzo ya Kisinda.
.
- Injinia Hersi Said.
Screenshot_20210823-152353_GBInsta.jpg
 
BREAKING: WANANCHI WASITISHA KAMBI MOROCCO, KUREJEA DAR
.
Kwa mujibu wa Injinia Gersi Said, Uongozi wa Yanga umesitisha ratiba ya kambi yao ya nchini Morocco na sasa wanarejea jijini Dar es Salaam kumalizia maandalizi yao..
.
Hersi amesema kuitwa kwa baadhi ya wachezaji wao ambao wanatakiwa kujiunga na timu za taifa ndio sababu ya kwanza ambapo jumla ya wachezaji wao nane kuitwa timu za taifa.
.
Siku 5 tu kambi Morocco
Screenshot_20210823-152505_GBInsta.jpg
 
| Metacha KMC
.
Aliyekuwa kipa namba moja wa Yanga, Metacha Mnata anatarajia kuwa miongoni mwa nyota watakaovaa uzi wa KMC msimu ujao amejiunga na tumu hiyo akiwa mchezaji huru.
.
Metacha anaenda kuungana na mkongwe Juma Kaseja ambaye ndiye kipa namba moja wa wanakinondoni ambaye sasa ameongezewa changamoto.
.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo kimesema tayari kipa huyo amemwaga wino wa kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na muda wowote atatangazwa.
Screenshot_20210823-152747_GBInsta.jpg
 
Azam Festival ndo basi tena, wapaa kwenda Zambia
.
Baada ya kupiga tizi la maana Dar, kikosi cha Azam FC kinapaa leo kwenda Ndola, Zambia kuweka kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa, huku ikipiga chini tamasha lao lililoasisiwa mwaka jana, ambalo awali lilipangwa lifanyike Septemba 5.
.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, timu hiyo itaweka kambi ya wiki moja na itacheza mechi za kirafiki dhidi ya Red Arrows na utapigwa keshokutwa, kisha Agosti 29 itavaana na Zanaco, kabla ya Septemba 2 kuwavaa Forest Rangers na siku inayofuata watamalizana na Zesco United.
.
Baada ya mechi hizo, Azam itarejea nchini kuwahi pambano lao la mkondo wa kwanza la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed SC ya Somalia litakalochezwa kati Septemba 10- 12 na Zakazi alisema kutokana na ratiba kubana, hawatafanya tamasha la ‘Azam Festival’.
Screenshot_20210823-152922_GBInsta.jpg
Screenshot_20210823-152939_GBInsta.jpg
 
Beki wa zamani wa Arsenal na Chelsea, David Luiz, 34, yupo kwenye rada za Flamengo inayohitaji kumsajili katika dirisha hili kama mchezaji huru. Luiz kwa sasa hana mkataba na timu yoyote baada ya kumalizana na Arsenal katika dirisha hili.
.
Luiz ni miongoni mmoja kati ya wachezaji waliocheza kwa mafanikio ndani ya England.
Screenshot_20210823-153116_GBInsta.jpg
 
AC Milan imeandaa ofa ya Pauni milioni 45 ili kumsainisha kiungo wa Manchester City na Ureno, Bernardo Silva, 27, katika dirisha hili.
.
Silva ni miongoni mwa wachezaji walioomba kuuzwa katika dirisha hili ili kutafuta changamoto mpya. Mkataba wake unamalizika mwaka 2025.
.
Ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango bora katika msimu uliopita.
Screenshot_20210823-153208_GBInsta.jpg
 
Vurugu imetokea katika mchezo kati ya Nice na Marseille. Baada ya Dimitri Payet kutupiwa Chupa na mashabiki wa Nice na yeye kuichukua na kuitupa kwa mashabiki hao. Mashabiki wa nice walivamia uwanjani na kuanza kugawa dozi kwa wachezaji wa Marseille.
.
Wachezaji watatu wa Marseille walijeruhiwa. Huku wengine wakitolewa damu na kukwaruzwa. Marseille waligoma kurudi uwanjani na refa akaamua kumaliza mchezo.Nice walikua wanaongoza bao moja
Screenshot_20210823-153310_GBInsta.jpg
Screenshot_20210823-153327_GBInsta.jpg
 
Imeripotiwa kwamba Kundi la Wanamgambo la Taliban limesema muda wa mwisho kwa Majeshi ya Nchi za kigeni kuwa Nchini humo ni August 31 2021 na muda huo hautaongezwa, haya yanakuja wakati ambapo Uingereza imeitaka Marekani kuongeza muda wake wa kuwaondoa Watu nchini humo.

Msemaji wa Taliban ametoa kauli hiyo ya kutokubali kuuongeza muda huo wakati huu ambao Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kumshinikiza Rais wa Marekani Joe Biden kuhusiana na suala hilo katika mkutano wa dharura wa nchi saba zilizostawi kiviwanda G7 kesho Jumanne.

Wakati huohuo Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema karibu Raia 400 wa Afghanistan waliokuwa wanafanya kazi na umoja huo watapewa hifadhi kwenye Bara la Ulaya ambapo kwa sasa wanapelekwa Spain kufanyiwa vipimo na kisha kupelekwa katika Nchi tofauti za Ulaya zilizo tayari kuwapa vibali vya kuishi nchini mwao.
Screenshot_20210824-050652_GBInsta.jpg
 
Kundi la Taliban limesema kwamba halitotangaza Serikali yake mpya hadi pale Marekani itakapokamilisha kuviondoa vikosi vyake ambapo vyanzo viwili ndani ya kundi hilo vimelieleza Shirika la habari la AFP kuwa uundaji wa Serikali na Baraza la Mawaziri hauwezi kutangazwa ikiwa bado kuna Wanajeshi wa Marekani wapo Nchini humo.

Wakati huohuo Msemaji wa muda mrefu wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahid amewataka Maimamu nchini humo kuwapa uhakikisho Waafghani juu ya usalama wao na kuondoa propaganda zisizo na misingi zinazoenezwa na Marekani juu ya Taliban.
Screenshot_20210824-050854_GBInsta.jpg
 
Kamanda Mstaafu Kanda Maalum ya Dar es saalaam Kamishna Suleiman Kova leo kwenye Amplifaya ya Clouds FM ameelezea tukio la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima kuomba kubadilisha kiti na microphone vilivyokua vimeandaliwa kwa ajili yake kuvitumia wakati akihojiwa na Kamati ya Bunge Dodoma, Kova ameelezea tukio kama hili kwa kutumia uzoefu wake akiwa Polisi na kuhoji Watu mbalimbali wenye tuhuma.

"Wakati mwingine Mtu akishafanya jambo flani anakuwa na hisia flani ambazo sio za kawaida labda anafikiri nikikaa hapa naweza nikadhurika, ni tatizo la kisaikolojia kwa Mtu ambae ana msongo wa mawazo anakuwa hajiamini na haamini Mtu yeyote yule, kwahiyo anaweza kufanya jambo lolote lile”

"Mfano mimi zamani nilikua nahoji Wahalifu, akiletwa kwangu akisikia ni Kova anapoingizwa mule ndani anadondoka chini paap bila kumgusa, yani anaona amekutana na kitu cha hatari sana kutokana na yeye anavyoelewa, kama ni madhambi anayakumbuka yote" ——— Kamanda Mstaafu Kanda Maalum Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.
Screenshot_20210824-051146_GBInsta.jpg
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kuanzia leo August 23,2021 limeanzisha operesheni dhidi ya magari yaliyosajiliwa kwa namba za Serikali STJ, STK, STL, DFP, SU, SM na mengineyo yote yanayoendeshwa bila kutii sheria za usalama Barabarani.

Nyigesa amesema imebainika baadhi ya magari hayo yanaendeshwa kwa mwendokasi kuyapita magari mengine pasipo kuchukua tahadhari na yana madeni makubwa yaliyotokana na tozo za papo kwa papo (Notification) na hawataki kulipa kwa hiari.

“Kumekuwa na tabia mbaya ya uendashaji vibaya kwenye Barabara ya Morogoro na Bagamoyo na nyingine zinazopita Mkoani Pwani, Watu wanaotumia magari ya STJ, STL, STK, PT, MT,SUM n.k wanaendesha bila tahadhari, nasema uendelee kutii sheria za Barabarani ukifanya makosa tutakukamata kama Mhalifu hata uwe na mkubwa ndani ya gari, wewe unamuita Boss wako sisi wote tutawaita Wahalifu maana hakukukemea”

“Operesheni hii ni endelevu na itagusa kila gari ambalo linadaiwa na linaendeshwa pasipo kutii sheria na alama za usalama Barabarani” ——— RPC Wankyo.
Screenshot_20210824-051355_GBInsta.jpg
 
Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima amehojiwa kwa zaidi ya saa mbili na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge huku shauri lake likitarajiwa kuendelea kesho kutwa.

Baada ya mahojiano haya kufanyika Mwenyekiti wa Kamati hii Emmanuel Mwakasaka amesema wamemaliza kusikiza shauri la Askofu Gwajima kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili itafanyika kesho kutwa.

“Askofu Gwajima ametoa ushirikiano wa kutosha bado suala hili linaendelea kazi yetu kama kamati ni kuchunguza Mbunge anayekiuka maadili na kanuni za bunge tumemruhusu aende lakini shauri lake bado linaendelea” ——— Mwenyekiti Mwakasaka.

Mwenyekiti huyo amesema kwa sasa hawawezi kusema kama akikutwa na hatia atachukulia hatua gani au kupewa adhabu gani kwakuwa zipo nyingi na mwenye kazi hiyo ni Spika wa Bunge peke yake.
Screenshot_20210824-052510_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-052552_GBInsta.jpg
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetoa salamu za rambirambi kwa Ndugu Jamaa na Marafiki wa Wafanyakazi wake watano waliofariki kwenye ajali ya gari leo Old Vwawa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wakiwa wanalikimbiza gari ambalo lilidhaniwa kuwa na bidhaa za magendo.

Taarifa hii ya TRA imesema "Kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa majonzi na masikitiko makubwa natoa taarifa ya vifo vya Maofisa watano waliokua Watumishi katika Idara ya Ushuru na Forodha vilivyotokana na ajali mbaya ya gari alfajiri Augut 23 2021, waliofariki ni Benard Balagi Mushingi (40) Afisa Forodha (TRA Songwe)”

"Wengine ni Azaria Asakwe Sivonike (42) Dereva TRA Mbeya, Joel Isaya Mitondwa (36) Afisa Forodha TRA Mbeya, Said Mrisho Buddy (34) Afisa Forodha TRA Mbeya na Fahad Hassan Haji (26) Afisa Forodha Msaidizi TRA Mbeya"

"Familia ya TRA itaendelea kuwakumbuka Marehemu wote watano na kuenzi mchango wao katika kazi ya kukusanya mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu, sisi Watumishi wenzao vifo hivi vimetuacha na simanzi kubwa na pengo lisilozibika kirahisi kwa nguvu kazi tuliyoipoteza pamoja na kuzingatia maarifa na weledi waliokuwa nao" ——— Kamishna Mkuu Alphayo Kidata.
Screenshot_20210824-052854_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-052910_GBInsta.jpg
 
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini SACP Wilbroad Mutafungwa amemfungia leseni Dereva wa Basi la kampuni ya Sauli kwa muda wa miezi sita kutokana na kitendo chake cha kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari (Wrong Overtake) asubuhi leo akielekea Tunduma kutokea Dar na kusababisha ajali na Watu wanne kujeruhiwa.

Mutafungwa amesema kitendo hicho kilichofanywa na Dereva huyo ni ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na ameeleza kuwa Dereva huyo atatakiwa kukaa bila leseni kwa muda wa miezi sita na kurudi tena darasani.
Screenshot_20210824-053339_GBInsta.jpg
Screenshot_20210824-053416_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom