
farhan jr
CRISTIANO RONALDO NA SIMULIZI YA ALBERT FANTRAU
Kwanza kabisa chukua Biblia, kisha fungua LUKA 10:2 "Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache Kwa hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake"
Tafsiri fupi ni kuwa mavuno ni mengi ila Watenda kazi ni wachache! Tusahau kidogo kuhusu rejea hiyo, ikiwa imetimu saa 5:32 Asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki, ikiwa sawa na saa 3:32 Asubuhi Lisbon Ureno
Stori inarudi nyuma miaka ya 90! Visiwani huko Madeira, nyumbani kwa Cristiano Ronaldo! Jioni moja ya upepo mkali wa bahari ya Atlantic, juu ya milima ya volcano kuna mbungi itapigwa
Lakini kabla hawajaingia kwenye mechi kuna Scout mmoja aliwaita vijana wawili mbele ya Kocha wao! Akamuita Cristiano Ronaldo na fundi mali mwingine anaitwa Albert Fantrau, akawatazama kwanza kwa tabasamu
Kisha akawaambia nimetoka mbali huko Lisbon! Nimekuja visiwani kuwatazama ubora wenu, nimepata masimulizi yenu kuhusu miguu kama ya Eusebio na utashi kama Luis Figo, ila mimi nitaondoka na mmoja kati yenu, atakaefunga mabao mengi kuliko mwenzie
Ronaldo na Fantrau wakaingia uwanjani huku wakijua mmoja tu atapata nafasi ya kuondoka! Mechi ilipoanza ni Cristiano Ronaldo alianza kuweka bao la kwanza, kisha Fantrau akaweka chuma ya pili
Tayari mzani umebalance! Scout anatazama mechi, ilipigwa pande zuri kwa Fantrau akawachukua mabeki kisha Kipa, Cristiano alikuwa kwa kasi nae anasogea! Fantrau alipomuona CR7 akampa pande, Ronaldo akaweka chuma ya tatu (bao lake la pili)
Ronaldo kwa mshangao akamtazama Albert na kumuuliza, kwanini amempa yeye afunge? Kifupi Fantrau akasema "Ronaldo wewe ni bora zaidi yangu, nenda kapambane" Ronaldo aliondoka kupitia hapo
Lakini miaka mingi baadae Fantrau kwasasa anaishi maisha anayotaka, anakula bata zote kutokana na Ronaldo anaemfadhili Rafiki yake kwa kila kitu, amelipa vyema fadhila
