Makapuku Forum

Makapuku Forum

NEW NUMBER | PHILLIPE COUTNH

Barcelona wapo mbioni kumpa jezi namba nyota huyo raia wa Brazil Phillipe Coutinho huku wakiwa na imani kubwa juu ya kipaji chake
Screenshot_20210818-155301_GBInsta.jpg
 
Martin Odeergard anakaribia kujiunga na Arsenal akitokea Real Madrid kwa uhamisho wa kudumu

Odeergard leo hakufanya mazoezi na timu kutokana na kukamilisha harakati za uhamisho wake
Screenshot_20210818-160022_GBInsta.jpg
 
TAARIFA RASMI KUTOKA KWA CRISTIANO RONALDO|

" Nimekuwa nikifuatilia taarifa nyingi kunihusu mimi, niseme wazi kuwa ni kunikosea heshma, kujadili mustakabari wangu kupitia vyombo vya habari, sijaridhishwa"

"Kwa Real Madrid nimeandika historia, historia ambayo itasalia kwenye mioyo ya Mashabiki na wapenzi, itatunzwa pia kwenye Makumbusho pale Bernabeu"

"Mashabiki wa kweli wa Real Madrid wananipenda na kuniheshimu, kama ambavyo nawapenda na kuwaheshimu, kwa zaidi ya miaka tisa"

"Napenda changamoto na mara zote nipp tayari kwa changamoto, nipo na utayari na utimamu zaidi wa kuendelea kupambana kama siku zote"

"Sema kidogo, kazi zaidi"
Screenshot_20210818-160212_GBInsta.jpg
 
Kagera Sugar imekiri kuwa na mkataba wa mwaka mmoja na mchezaji Yusuph Mhilu ambaye hivi karibuni ametambulishwa na klabu ya Simba.

Katibu Mkuu wa Kagera Sugar Ally Masoud amesema hawana nia ya kuishtaki Simba badala yake wanataka kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo
Screenshot_20210818-160506_GBInsta.jpg
 
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amsema, wanatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki kabla ya mchezo maalum wa kutambulisha wachezaji pamoja na jezi za msimu mpya [Simba Day].

“Tunalifanyia kazi suala hilo la mechi za kirafiki ambayo ni ya kiufundi zaidi ili mwalimu na benchi la ufundi kuona kile ambacho amewapa wachezaji.”

“Tuna mpango wa kuendelea kutafuta hizo mechi, siku mbili tatu hizi tutajua tunacheza na nani.”
Screenshot_20210819-080125_Instagram%20Lite.jpg
 
Patrick Rweyemamu [Meneja wa Simba] amekanusha taarifa kwamba Simba imealikwa kushiriki mashindano maalum nchini Morocco ambako imewaka kambi ya maandalizi kuelekea msimu ujao.

“Sina taarifa wala sijui kama kuna hayo mashindano.”

Kuna taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa vilabu vya Simba na Yanga vimealikwa kushiriki kwenye mashindano maalum huko nchini Morocco.
Screenshot_20210819-080600_GBInsta.jpg
 
Mikono ya farhan jr

Huyo pichani ni YUSUPH MHILU, nyota wa zamani wa Kagera Sugar ambaye sasa yupo SIMBA

Well kwenye nchi yetu tuna vitu viwili SIGNING FEE na TRANSFER FEE, Mchezaji akiwa na mkataba basi utafanya vyote viwili

SIGNING FEE, ni ada ya kusaini! Hii anachukua Mchezaji mwenyewe na Simba walikubaliana kila kitu na Kijana na akapewa kinachomuhusu

TRANSFER FEE, hii ilipaswa alipwe Kagera kwakuwa Mchezaji alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja! Hii ni ada ya uhamisho, hapo sasa ni Simba vs Kagera

Anyways tuachane na hapo juu! Lakini kwenye Transfer Fee inategemea na vipengele vya kimkataba kati ya Mchezaji na klabu yake!

Hapo kuna kitu kinaitwa RELEASE CLAUSE! Picha lipo hapa, kwenye hii mkataba unasema ili Yusuph aondoke anapaswa kulipa Mshahara wa miezi ya kimkataba ambayo ni 12 zidisha kwa Mshahara

Ukifanya hivyo unakuwa umenunua mkataba wake na anakuwa huru kujiunga na timu yako

Ule utata mdogo ulikuwa Simba kusimamia kipengele cha mkataba (Release Clause) ambayo haikuwa kubwa kuliko ada ya uhamisho inayotakiwa
Screenshot_20210819-081045_GBInsta.jpg
 
Msaidizi wa Nabi, Kocha wa viungo wasepa Yanga kimyakimya
.
Japo Yanga wamekuwa kimya lakini taarifa za kuaminika ni kwamba kuna watu watatu muhimu katika benchi la ufundi la Yanga hawatakuwepo msimu ujao wameamusha kimyakimya.
.
Yanga haitakuwa na kocha msaidizi, Sighr Hamad lakini pia mtaalamu wa mazoezi ya viungo Jawad Sabri na daktari Msauzi wa viungo Fareed Cassem ambao kwa sababu mbalimbali za kupata kazi mpya hawatakuwa sehemu ya timu hiyo kwa msimu ujao.
Screenshot_20210819-081338_GBInsta.jpg
 
GOMES, SVEN KUKIPIGA JUMAMOSI HII
.
Habari ndo hiyo. Mabingwa wa nchi, Simba SC Jumamosi hii wanawasha mitambo dhidi ya FAR Rabat saa 10 jioni za Morocco sawa na saa 12 kwa Tanzania.
.
Kocha Didier Gomes amekiri kwamba kikosi chake kinazidi kuimarika kadri mazoezi yanavyochanganya na watakiwasha na FAR Rabat ya Kocha Sven Vandebroeck Jumamosi kama mechi ya kirafiki. Sven alikuwa na Simba kabla ya kuwakacha na kutua kwenye timu hiyo ndipo wakambeba Gomes akawapa makombe mawili.
.
Screenshot_20210819-081548_GBInsta.jpg
 
Arsenal yarudi tena kwa Ramsdale
.
Arsenal imeanza tena kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Sheffield United ili kuipata saini ya golikipa wa timu hiyo na England, Aaron Ramsdale, 23, katika dirisha hili baada ya Sheffield kukubali kupunguza pesa iliyokuwa inahitaji hapo awali.
.
Sheffield Kwa sasa ipo tayari kupokea Pauni milioni 24 na kumuuza tofauti na hapo awali ambapo ilihitaji Pauni milioni 35.
.
Arsenal imekuwa kwenye harakati za kutafuta golikipa tangu dirisha lilipofunguliwa huku uongozi wa The Gunners ukikosolewa kwa kumuuza kipa wao aliye katika kiwango cha Bora kabisa, Emiliano Martinez kwa klabu ya Aston Villa kwa Pauni milioni 20.
Screenshot_20210819-081710_GBInsta.jpg
 

.
Alphonso Davies (20) alijiunga na Bayern Munich mwaka 2018 na hadi sasa tayari ameshinda mataji 10.
.
Jana, akionyesha kiwango bora zaidi na akafanikiwa kushinda kwa mara ya pili kikombe cha Germany Super Cup.
.
Hivi kuna beki ya kushoto Bora kwasasa kuliko Davies __?
Screenshot_20210819-082208_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom