Makapuku Forum

Makapuku Forum

MIQUISSONE AAGA SIMBA
Screenshot_20210817-145628_GBInsta.jpg
Screenshot_20210817-145645_GBInsta.jpg
 
Mkono wa farhan jr

Kuna maswali mawili kwenye issue ya Luis Miquisson na Clatous Chama! Nadhani ni maswali mepesi sana yanayojibika kirahisi sana

Kwanini Simba hawajataja timu walizoenda?

Jibu jepesi hapo ni PRINCIPLE OF CONFIDENTIALITY na EXCLUSIVITY! Klabu kama Al Ahly na RS Berkane wana namna yao ya kutangaza wachezaji wao

Wana haki ya kupewa exclusive, hapo Simba amewaheshimu wanunuzi wake ili wabaki na exclusive zao kwakuwa biashara haitoishia hapa! Huo ndio weledi wa klabu kubwa, Simba wana kosa gani hapo?

Kwanini hawajataja bei? Ni hapo hapo Confidential kuna kitu kinaitwa UNDISCLOSED FEE! Nitajieni klabu inayotaja bei iliyouza Mchezaji wake duniani ni ipi

Sasa kwanini Simba wakatangaza kwa kutumia Public notice?

Well, jibu jepesi sana wiki chache zijazo majina ya wachezaji wapya yatatangazwa, Simba ametoa taarifa kufuta taharuki pale ambapo majina ya wachezaji hao yasipoonekana, kuna kosa kwa klabu kufuta taharuki?

Taarifa zimeshasambaa mitandaoni ikiwemo na picha za Wachezaji mfano Chama akiwa Berkane, sasa klabu kutoa taarifa ina ubaya gani

Lastly watu wanahoji mkataba wa SIMBA na Luis Miquisson, kuna tatizo?

Kama Miquisson sio Mchezaji wa Simba, well nani katoa taarifa ya Mchezaji kuondoka? Wametoa UD SONGO? wametoa MAMELODI SUNDOWNS? jibu ni kuwa wametoa SIMBA

Miquisson alisaini kandarasi ya miaka mitatu na nusu! Amecheza mwaka mmoja na nusu, Chama alikuwa na mkataba wa miaka miwili

Mkitaka kupata taarifa sahihi wala msipende sana kutumia WIKIPEDIA, anyone can edit
Screenshot_20210817-150132_GBInsta.jpg
 
Tambwe, Kutinyu kurejea Bongo kucheza Ligi daraja la Kwanza
.
Matajiri wa klabu ya DTB FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, wamethibitisha nia yao ya kuwarudisha nchini wachezaji maarufu Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu.
.
Tambwe na Kutinyu wanatarajiwa kutua nchini kuanzia wiki hii kwani wameshaelewana kila kitu na mabosi wa timu hiyo na wanakuja kusaini mkataba. wameamua kuja huku kwa sababu wameona timu hiyo inajipanga kupanda Ligi Kuu.
.
Screenshot_20210817-150822_GBInsta.jpg
 
BARAZA AMCHOMOA MLIPILI KAGERA
.
Kocha wa Kagera Sugar, Mkenya Francis Baraza amemruhusu beki wake Yusuph Mlipili kwenda kwa mkopo timu nyingine kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
.
Baraza ambaye alichukua mikoba ya kukinoa kikosi cha Kagera Sugar, Machi, mwaka huu akichukua nafasi ya Mecky Maxime amesema
amefanya uamuzi sahihi li kuokoa kipaji cha beki huyo wa zamani wa Simba.
.
Unadhani kwanini wachezaji wengi WANAFELI wanaotolewa kwa mkopo kutoka vilabu vya Simba na Yanga __?
Screenshot_20210817-151141_GBInsta.jpg
 
Thomas Tuchel
.
"Kusajili wachezaji ili kubalance kikosi chako ndo kinachokuwezesha kushinda mataji. Makocha wakubwa kama, Pep Guardiola na Jose Mourinho hufanya hivyo. Na mimi pia ninafanya hivyo.
.
"Ukifanya kusajili wachezaji kwa ajili ya kuburudisha umma, hautawahi kuwa kocha aliyefanikiwa kushinda mataji.”
Screenshot_20210817-151610_GBInsta.jpg
 
"Tumepata taarifa za msiba wa Mzee mwenzetu Basil Mramba, aliyewahi kuwa waziri, kwamba amefariki. Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na taifa zima kwa msiba huu ambao umelipata Taifa”

"Wazee wa CHADEMA tuna kauli mbiu inayosema Wazee ni hazina ya hekima na busara na kwa sababu hiyo ni wajibu wa kutumia hekima na busara ambazo Mungu ametujalia kwa kipawa au baraka za umri ambao ametupa tuishi ili tuweze kutoa ushauri, kuonya, kukemea inapobidi”

“Tunalaani kitendo kilichofanyika jumapili ya tarehe 15/08/2021 huko Mwanza ambao Jeshi la Polisi liliwakamata Wanachama na Viongozi wapatao 20 walipokuwa katika maeneo ya kanisa kwenye Parokia ya Roman Catholic Kawekamo Mwanza”

“Jambo hili limetokea zikiwa ni siku chache likiwa limetokea tena huko Mbeya na kufuatiwa na kukemewa na Katibu Mkuu wa TEC aliyeweza kuitolea ufafanuzina kusema kwamba haikuwepo sababu yoyote ya kuwakamata Viongozi au Wanachama waliokuwa wamevaa sare”

“Vitendo hivi vya uonevu, dhuluma, vitisho na ubaguzi si tu kwamba vinakiuka haki za watu zilizoainishwa katika Katiba ya JMT ibara ya 12 na 13 lakini vinaibua chuki na vinaweza kusababisha uhasama na kuhatarisha usalama” ——Roderick Lutembeka, Katibu Mkuu Baraza la Wazee CHADEMA.
Screenshot_20210818-050220_GBInsta.jpg
 
Abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Kigoma kwenda Mwanza kwa basi la abiria lenye namba za usajili T 794 AEM la kampuni ya Adventure, wamenusurika kifo baada ya basi hilo kupata ajali katika eneo la Kalenge Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera kupinduka.

Chanzo cha basi hilo kupinduka ni tairi kupasuka na basi kupoteza mwelekeo wake sahihi kisha kuanguka takribani mita 100 kutoka barabarani.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa sita mchana. Katika ajali hiyo watu kadhaa wameumia na kupelekwa katika zahanati ya Nyakanazi kwa ajili ya matibabu, Abiria wa basi hilo wameendelea na safari baada ya kampuni kuleta basi lingine.
Screenshot_20210818-050643_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-050659_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-050712_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-050727_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-050749_GBInsta.jpg
 
Msemaji wa sera za kigeni katika chama cha Kansela wa Ujerumani amesema ndege za kwanza za kijeshi za Ujerumani zimewahamisha Watu saba pekee kutoka Afghanistan kutokana na ghasia katika uwanja wa ndege wa Kabul, amesema kuwa Watu saba pekee ndio waliokolewa kutokana na ugumu wa oparesheni hiyo.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Annegret Kramp-Karrenbauer amesema lengo la kutumwa kwa Ndege hizo za kijeshi ni kusaidia kuwahamisha Watu "tunatarajia katika awamu ya pili pamoja na Marekani tutaweza kuwahamisha Watu wengi zaidi, Wanajeshi 600 watahusika katika shughuli za uokoaji"

"Kwa sasa ni muhimu tuweke kila kitu sawa ili kuwahamisha, sio tu Raia wa Ujerumani bali pia Watu walioko kwenye hatari na Wafanyakazi wengine muhimu tutajaribu kuwahamisha".
Screenshot_20210818-051040_GBInsta.jpg
 
Ndege za kijeshi zinazowabeba Wanadiplomasia na Raia kutoka Afghanistan zimeanza tena safari zake leo ikiwa ni siku moja baada ya maelfu ya Watu kuvamia uwanja wa ndege wa Kabul kwa matumaini ya kukimbia Nchi.

Ripoti zinasema kuwa idadi ya raia imepungua katika uwanja wa ndege wa Kabul siku moja baada ya kutokea tafrani wakati maelfu ya watu walipouvamia uwanja huo wa ndege kwa matumaini ya kukimbia nchi. Wanajeshi wa Marekani walijaribu kutawanya umati huo kwa kufyatua risasi huku wengi wao wakijaribu kuning'inia katika ndege ya kijeshi ya Marekani wakati ikianza kuondoka.

Hali hiyo ilisababisha safari za ndege kusitishwa Jumatatu wakati Watu watano walipofariki ingawa haikuwa wazi kama walipigwa risasi au walikufa kwa sababu ya mkanyagano, Ripoti nyingine za vyombo vya habari zinasema kuwa Watu wawili walianguka kutoka pembeni mwa ndege hiyo baada ya kupaa na kufariki.
Screenshot_20210818-051150_GBInsta.jpg
 
“Nimefurahi kutoa hotuba yangu ya kujitambulisha kwa Wakuu wa Nchi na Serikali nikiwa hapa Malawi kwa sababu Malawi ndio Taifa la kwanza ndani ya ukanda wetu wa SADC kuwa na Rais Mwanamke”

“Naamini kujitambulisha kwangu hapa naongeza msukumo kwa Wanawake wengi zaidi kujiamini na kuhamasika kushiriki kwenye vyombo vya kufanya maamuzi”

“Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ukanda wa SADC hatupaswi kuridhika, bado tunakabiliwa na changamoto nyingi, Jukumu la kutatua changamoto hizo tulizonazo ni letu sisi tuliyopewa dhamana ya kuongoza kwa kushirikiana na wananchi wetu “——— Rais Samia kwenye Mkutano wa SADC Nchini Malawi leo.
Screenshot_20210818-051420_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-051436_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-051454_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom