Makapuku Forum

Makapuku Forum

Safari za Ndege kuhamisha Watu kutoka kwenye uwanja wa Ndege wa Kabul, Afghanistan zimerejea kama kawaida baada ya vurugu na taharuki ya jana kuisha ambapo picha hii inaonesha Raia wa Afghanistan wapatao 640 wakiwa angani ndani ya Ndege ya Kijeshi ya Marekani C-17 Globemaster III wakielekea Qatar.
Screenshot_20210818-051725_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-051740_GBInsta.jpg
 
Uganda imekubali ombi la Marekani la kuwapa hifadhi Wakimbizi 2,000 kutoka Afghanistan baada ya kuikimbia Nchi hiyo kutokana na wasiwasi juu ya utawala wa Taliban, Marekani imeiomba Uganda kuwapokea.

Naibu Waziri huyo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa Wakimbizi hao watakaa nchini Uganda kwa miezi mitatu kabla ya Marekani kuwahamisha sehemu nyengine ambapo hata hivyo haijajulikana ni lini Wakimbizi hao watawasili nchini Uganda.

Mataifa mengine yaliyokubali kuwapokea Wakimbizi wa Afghanistan ni pamoja na Albania na Kosovo ambayo nayo yaliombwa na Marekani kuwapa hifadhi ya muda Wakimbizi hao.
Screenshot_20210818-051848_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-051902_GBInsta.jpg
 
Msemaji wa kundi la Wanamgambo la Taliban Zabiullah Mujahid amesema Vyombo vyote vya habari Nchini humo viendelee kurusha matangazo kama kawaida lakini visirushe chochote kinachokwenda kinyume na Uislamu na pia wasirushe chochote kinachokwenda kinyume na matakwa ya Taifa hilo.

Vilevile Mujahid amesema hawatolipiza kisasi kwa Mtu yeyote, iwe ni Wanajeshi au wale wote waliofanya kazi na Majeshi ya kigeni “hatutosachi nyumba ya Mtu yeyote, hali kwenye Mji wa Kabul itarejea kwenye ukawaida wake hivi karibuni”
Screenshot_20210818-052022_GBInsta.jpg
 
Droo ya Kupanga Makundi AFCON 2021 imepangwa leo nchini Cameroon, Makundi na viwanja vimetajwa, mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya mwenyeji Cameroon dhidi ya Burkinafaso, fainali hizo zitachezwa kuanzia January 9 hadi February 6 2022
Screenshot_20210818-053929_GBInsta.jpg
 
Droo ya Kupanga Makundi AFCON 2021 imepangwa leo nchini Cameroon, Makundi na viwanja vimetajwa, mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya mwenyeji Cameroon dhidi ya Burkinafaso, fainali hizo zitachezwa kuanzia January 9 hadi February 6 2022
Screenshot_20210818-053929_GBInsta.jpg
 
Kukosewa kwa jina la tatu la mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha Lengai Ole Sabaya, kumesababisha malumbano ya kisheria na kuahirishwa kesi kwa muda.

Katika hati ya maelezo ya mashitaka, jina Sabaya limesomeka Sayaba na kusababisha kuibuka kwa malumbano ya kisheria.

Malumbano yalianza saa 4:04 asubuhi hadi saa 6 mchana baada ya upande wa Jamhuri kupitia Wakili Mwandamizi, Abdallah Chavula na Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka kuomba marekebisho madogo ya hati hiyo kutokana na kubaini makosa ya kiuchapaji.
Screenshot_20210818-054417_GBInsta.jpg
 
Msemaji wa Kundi la Wanamgambo la Taliban Zubihullah Mujahid amesema haki za Raia wote wa Afghanistan wakiwemo Wanawake, zitalindwa kwa mujibu wa sheria ya kiislamu na akawataka Waafghani wote hata wale waliofanya kazi na Nchi za kigeni kubakia nchini mwao na kuchangia kuijenga.

Mujahid alirudia mara kwa mara kauli yake kuwa kila kitu kitakuwa katika misingi ya sheria ya kiislamu ikiwemo sekta ya habari na akazihakikishia Nchi zote hasa Marekani kwamba Afghanistan haitaruhusu Makundi yoyote kutumia ardhi yake kuhujumu usalama wa Nchi nyingine.
Screenshot_20210818-150820_GBInsta.jpg
 
Wakati chanjo ya corona ikiendelea kutolewa katika Mataifa mbalimbali Duniani, chanjo ya Virusi vya UKIMWI (VVU) iliyokuwa inafanyiwa utafiti muda mrefu na Kampuni ya Moderna ya Marekani inatarajiwa kuanza kufanyiwa majaribio kwa Binadamu leo Jumatano.

Kampuni hiyo imetengeneza chanjo za aina mbili za UKIMWI ambazo zimefuzu hatua za awali za kimajaribio na hivyo kuanza kutumika kwa binadamu katika awamu ya tatu, chanjo hizo ni mRNA-1644 na mRNA-1644v2-Core ambazo zimeshachunguzwa na kufanyiwa majaribio ya awali na kuonekana salama kabla ya kujaribiwa kwa Binadamu kwa mara ya kwanza.

Chanjo hiyo itaanza kutolewa kwa Watu 56 wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 56 na majaribio yanatarajiwa kukamilika Mwaka 2023.
Screenshot_20210818-151458_GBInsta.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo 18 Agosti katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Lilongwe nchini Malawi.
Screenshot_20210818-151712_GBInsta.jpg
Screenshot_20210818-151739_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom