Makapuku Forum

Makapuku Forum

UGANDA;

Waziri wa Jinsia, nchini Uganda Betty Amongi, amesema wanaume nchini humo wamekuwa wakiombea wakimbizi kutoka nchini Afghanistan wawasili salama na kwamba wamekuwa wakisambaza picha za wanawake hao warembo na kusema anatumaini hawatotoka chama cha wanaume bahili.
Screenshot_20210819-174708_GBInsta.jpg
 
Tishu aliyoitumia Lionel Messi kupanguza machozi wakati akilia katika hafla ya kuiaga Barcelona inauzwa kwa dola milioni 1


Messi ambaye alibubujikwa machozi wakati alipojawa na hisia za kuondoka Barcelona alipewa tishu hiyo na mkewe Antonella Messi katika kikao na waandishi wa habari .



Kwa mujibu wa Complete Sports, mtu aliyehudhuria kikao cha Messi wakati anaiaga Barcelona huko Catalonia alifanikiwa kupata tishu ambayo Messi alitumia kupanguza machozi na ndiye anayetakakulipwa kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa yeyote aliye tayari kuinunua .


Messi, ambaye ataingia katika historia kama mchezaji bora wa nyakati zote alilazimika kumaliza uhusiano wake wa miaka 21 na FC Barcelona kwa sababu ya sheria za usawa wa matumizi ya fedha za La Liga.

View attachment 1898348
Screenshot_20210819-175104_GBInsta.jpg
 
Kanisa Anglikana la Ghana limemfuta kazi kasisi mmoja aliyenaswa katika video moja iliyosambaa mitandaoni akiwabusu wanafunzi wa kike chuoni.


“Kanisa limesikitishwa na tukio la kufedhehesha lililotokea katika chuo cha mafunzo ya elimu cha mtakatifu Monica la Ashanti Ghana na sasa tumemsimamisha kazi Reverend Father Balthazar Obeng Larbi hadi uchunguzi ukamilike.”


Kanisa pia limechukua jukumu la kuwapa ushauri nasaha wanafunzi watatu waliohusika katika tukio hilo lililokiuka maadili ya Kanisa.

Screenshot_20210819-175302_GBInsta.jpg
 
TETESI |

Taarifa kutoka Morocco zinasema kwamba kocha msaidizi wa Yanga Sighr Hamad amevunja mkataba na klabu hiyo na hatakuwa sehemu ya benchi la ufundi kwa msimu ujao.

Mbali na kocha msaidizi lakini pia mtaalamu wa mazoezi ya viungo Jawad Sabri na daktari wa viungo Fareed Cassem kwa sababu mbalimbali wameamuama kuachana na timu hiyo .
Screenshot_20210819-175554_GBInsta.jpg
 
HATMA YA KYLIAN MBAPPE

"Kwangu mimi sipendi kusikia neno kuwa ndie future ya PSG, kwangu future ni sasa" inasemekana maneno ya Kinda Kylian Mbappe kwa CEO wa PSG

Kifupi kwenye mkutano wao Mbappe amewaomba wamruhusu aende Real Madrid kwakuwa huko ndipo future yake ilipo

Amewaambia wazi kuwa hatoongeza mkataba kama hatouzwa, hivyo ataondoka bure mwishoni mwa msimu huu
Screenshot_20210819-175734_GBInsta.jpg
 
GEITA GOLD: MINZIRO OUT, NDAYIRAGIJE IN
.
Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Etienne Ndayiragije amerejea tena nchini na anatarajia kukinoa kikosi cha Geita Gold kilichopanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao.
.
Ndayiragije ni mzoefu wa Ligi Kuu Bara baada ya kuwahi kuzinoa Mbao, KMC na Azam kwa nyakati tofauti.
.
Kama Geita itafanikiwa kumnasa Ndayiragije itakuwa jambo baya kwa Minziro ambaye amekuwa na rekodi ya kuzipandisha timu Ligi Kuu kisha kisha humtema.
Screenshot_20210819-180002_GBInsta.jpg
 
JUST IN

Habari kutoka Morocco zinasema kwamba Kiungo mkata umeme Serge Mukoko Tomombe (25) ameacha kufanya mazoezi katika siku chache zilizopita na hana furaha baada ya Uongozi wa Yanga kumzuia kwa kukataa ofa ya RS Berkane.
Screenshot_20210819-180125_GBInsta.jpg
 
Kabwili aibukia Taifa Star
.
Leo Kocha Mkuu Taifa Stars Kim Poulsen ametangaza kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu kombe la Dunia na jina la kipa namba tatu wa Yanga, Ramadhan Kabwili kuitwa.
.
Kabwili amejumuishwa kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho ambacho kitaingia kambini Agosti 24 kujiandaa na mechi mbili dhidi ya DR Congo na Madagascar mechi zitakazopigwa kati ya Seotemba 2-7 mwaka huu.
.
Makipa wengine ni Aishi Manula wa Simba, Metacha Mnata (Huru) na Wilbol Maseke (Azam).
Screenshot_20210819-180301_GBInsta.jpg
 
Fiston:

Uongozi Yanga umefeli kumuuza Kisinda
.
"Sawa tumeondoka Yanga lakini Tuisila uongozi ungejitahidi kumbakiza, alikuwa muhimu sana katika kupeleka mashambulizi, na ikizingatia Yanga sasa hivi inajijenga zaidi kuwa na kombinesheni nzuri,"
.
"Sawa kwenda timu nyingine sio mbaya kwa kuwa mpira ndio kazi yake, lakini sio wakati huu, kwanza alianza kuijua na kuisoma Ligi ya Tanzania," amesema Fiston ambaye bado yupo nchini licha ya kuachana na Yanga.

Screenshot_20210819-180519_GBInsta.jpg
 
SAD NEWS

Kipa wa Simba, Beno Kakolanya leo Agosti 19, 2021 amefiwa na mama yake mzazi anayeitwa Eva Mwankusye na msiba upo kwao Mbeya.
.
Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na kaka wa mchezaji huyo, Asajile Mwakalindile ambaye alikuwa na mama huyo muda wote.
Screenshot_20210819-180658_GBInsta.jpg
 
“Nakumbuka Simba waliniambia kila kitu na Kagera wameshamalizana na nisaini mkataba wa miaka mitatu, hata nilipowafahamisha waajiri wangu (Kagera Sugar) wakati huo hawakupinga jambo hilo.
.
“Hivyo mpaka nasaini na kutambulishwa niliamini tayari viongozi wa Simba na Kagera wamemalizana, lakini wakati huu ndio kuna jambo hilo linaendelea nadhani ni suala la kiutawala zaidi kuliko kwangu.”
.
- Yusuph Mhilu.
Screenshot_20210819-180811_GBInsta.jpg
 
BIASHARA KUTUMIA UWANJA WA KIRUMBA
.
Klabu ya Biashara United imechagua kutumia Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kama uwanja wa nyumbani kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
.
Timu hiyo ambayo itashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza imepangwa kuanzia hatua za awali ikianzia ugenini dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Septemba 10 na 12, huku mechi ya marudiano ikichezwa Septemba 17-19, mwaka huu.
.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Seleman Mataso amesema kuwa tayari wameshawasilisha barua TFF, huku wakiwa wamepata baraka zote kutoka kwa wasimamizi wa Uwanja wa CCM Kirumba.
Screenshot_20210819-181100_GBInsta.jpg
 
BANGALA ATUA USIKU MOROCCO
.
Yanga leo inafunga usajili wake baada ya staa wao wa mwisho mpya kutua usiku kuungana na timu hiyo.
.
Bangala atawasili nchini Morocco leo usiku majira ya saa tatu tayari kwa kumalizana kila kitu na timu hiyo iliyopiga kambi jijini Marrakech.
.
“Nitafika huko Morocco leo, nilikuwa huko ila niliomba muda niende nyumbani mara moja na viongozi wakanikubalia, sasa niko tayari kuanza maisha mapya na Yanga, nakuja." amesema staa huyo ambaye ni mbadala wa Lamine Moro.
Screenshot_20210819-181207_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom