Makapuku Forum

Makapuku Forum

DID U KNOW | Michael Jordan anapata asilimia tano (5%) ya faida ambayo klabu ya PSG hupata kutokana na kuuza bidhaa zake.
.
Hadi Kufikia sasa, PSG imepata karibu Euro milioni 120 tangu jezi za Messi ziuzwe, ambapo Michael Jordan ameingiziwa Euro milioni 6 (Sh 16.3 bilioni) katika kipindi cha wiki moja
Screenshot_20210819-082842_GBInsta.jpg
 
Boxer aitaka namba ya Moloko
.
“Ukiangalia kule kulia wakati yuko Kibwana tu sikupata sana nafasi ya kucheza lakini sasa tunakuwa watatu baada ya Djuma kuja hakuna namna naona kutakuwa na ugumu wa kuwania nafasi kitu ambacho naweza kuja kuwa chaguo la tatu kwa kocha,
.
“Unajua hii nafasi ya beki wa kulia haikuwa nafasi yangu nilikuwa nacheza winga ya kulia lakini wakati ule kocha Zahera akaniomba nirudi kucheza nyuma baada ya kaka yangu Juma (Abdul) kuumia nafikiri sasa ni wakati wangu kurudi katika nafasi ileile nishindane na huyu Moloko,”

“Kama (Moloko) ana kasi hata mimi nina kasi,kitu kizuri sasa nimeimarika zaidi naweza pia kurudi kuja kukaba kwa nguvu nikitumia uzoefu wa kucheza kama beki wa kulia,nitaongea na kocha kumuomba hili mara tu tutakapoanza maandalizi ya huku Morocco akikubali watu watamuona Boxer mpya msimu ujao." amesema Paul Godfrey Boxer [Mwananchi]
Screenshot_20210819-083124_GBInsta.jpg
 
Joto laitibulia Yanga Morocco
.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, ambaye hata hivyo hakusafiri na timu, amesema amepokea taarifa kutoka kwa kocha mkuu kwamba hali ya joto kali katika mji huo imesababisha kubadili programu yao ya mazoezi.
.
"Kocha amesema wamefanya mazoezi asubuhi kwa muda mchache kutokana na joto kali, hivyo kuanzia leo, watalazimika kufanya mazoezi mapema sana asubuhi kabla ya jua kuchomoza na kisha hali ikiruhusu baada ya jua kuzama jioni.
.
Hali ya jijini Casablanca ilipo kambi ya Yanga kwa sasa inaelezwa ni joto kali tofauti na kambi ya Simba ilipo jijini Rabat nchini humo, ambayo haitofautiani sana na Dar es Salaam kwa sasa.
.
Kuhusu wachezaji ambao walikuwa hawajajiunga na kikosi hicho, Bumbuli alisema ni wawili tu ambao ni Khalid Aucho na Yannick Bangala Litombo, ambao wanatarajiwa kuwasili Morocco leo.
.
Screenshot_20210819-083551_GBInsta.jpg
 
PSG, Madrid kumjadili Mbappe wiki hii
.
PSG na Real Madrid zitafanya mazungumzo ndani ya wiki hii ili kujadili hatma ya straika wa PSG, Kylian Mbappe katika dirisha hili.
.
Mbappe aliyekataa kuongeza mkataba mpya, inaelezwa ameomba kuondoka baada ya Madrid kuonyesha nia ya kutaka kumsainisha.
.
Madrid ilianza kuiwania saini yake kwa muda mrefu na katika kipindi hiki inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsainisha kutokana na muda uliobakia kwenye mkataba wake na utayari wa mchezaji mwenyewe.
.
Mbappe mkataba wake unamalizika mwaka 2022 na ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa kikosi cha PSG.
Screenshot_20210819-083717_GBInsta.jpg
 
Kisa Yanga, Rivers United kujifua na Horoya, AS Vita
.
Rivers United ya Nigeria inayoanza na Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, itashiriki michuano mifupi nchini Benin ambayo AS Vita ya DR Congo na Horoya ya Guinea ni moja wa washiriki.
.
Rivers United wamethibitisha kushiriki michuano hiyo ya Chalenji ya Afrika Magharibi, kila timu ikijiandaa kwa msimu mpya.
.
Imepangwa kuanza kesho Alhamisi mpaka Jumatano ijayo nchini Benin. Timu shiriki ni Hearts of Oak (Ghana),Union Sportive de la Gendarmerie Nationale (Niger),Horoya Athletic Club (Guinea), Arta Solar 7 (Djibouti),Loto-Popo FC (Benin), Vita Club (Congo) na AS Sonabel FC (Burkina Faso). Zipo nyingine ni Les Buffles (Benin) na Rivers United FC (Nigeria).
Screenshot_20210819-083834_GBInsta.jpg
 
Hersi: Hizo jezi za mazoezi tu jamani!
.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Mhandisi Hersi Said ambao ndio wenye mamlaka katika kuzalisha na kuuza jezi za Yanga amesema jezi hizo zipo kwao muda mrefu ambazo ni maalum kwa ajili ya dharula katika mazoezi.
.
"Hizi sio jezi za kuuzwa na wala sio jezi zetu mpya watu wasichanganye mambo kwa kuwa wameziona leo tunazitumia huku.
.
"Jezi yetu mpya ya msimu ujao hatuwezi kuisambaza namna hii na hii jezi nikwambie ilikuja muda mrefu huko nyuma lakini tukasema tusiitumie sasa kuna wakati tulifikiria itumike katika mashindano ya Kagame lakini tukasema tutazitumia huku."
Screenshot_20210819-084058_GBInsta.jpg
 
Televisheni ya Taifa Tanzania (TBC) leo imetangaza kifo cha Mchambuzi maarufu wa soka, Mwalimu Alex Kashasha aliyefariki leo Agosti 19, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa TBC, Kashasha alikuwa Mtumishi wa Shirika hilo la Utangazaji Tanzania (TBC) hadi umauti ulipomfika., taarifa zaidi kukujia.
Screenshot_20210819-171736_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Cathbert Sendiga amepiga marufuku mikusanyiko na kuwaondoa Wananchi katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa Iringa walipofika kuchukua miili ya wapendwa wao, Sendiga amesema anachukua hatua hiyo kwa lengo la kuzuia maambukizi ya Covid 19.

Sendiga amepiga marufuku hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo na kukuta uwepo wa Watu wengi wanaoingia katika eneo hilo bila kuchukua tahadhari na kuagiza Watu wanaokwenda kuchukua miili ya Ndugu zao wasizidi Watu wanne na Ndugu wengine wabaki nyumbani. View attachment 1898293View attachment 1898294
Screenshot_20210819-171955_GBInsta.jpg
 
Aishi Manula, Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili, Wilbol Maskeke, Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Erasto Nyoni, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Kennedy Juma, Lusajo Mwaikenda, Abulrazack Mohamed, Mohamed Hussein, Nickson Kibabage, Edward Manyama.

Wengine ni Ayoub Lyanga, Meshack Mwamita, Novatus Dismas, Msamiru Yassin, Mudathir Yahya, Feisal Salum, Salum Abubakar, Zawadu Mauya, Iddy Selemani, Abdul Hamis, Mbwana Samatta, John Bocco, Simon Msuva.View attachment 1898301
Screenshot_20210819-172247_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makala ametoa siku ya jumapili wiki hii kua siku ya chanjo kimkoa ambayo itatolewa katika uwanja wa Taifa kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni kwa Watu wote bila kuangalia umri na endapo mda wa saa kumi watakua bado hawajamalizika mda utaongezwa mpaka wote wamalizike.

RC Makala amesema sababu ya kuweka siku ya jumapili Watu wachanjwe kwa hiari yao katika eneo la wazi baada ya kupokea malalamiko katika mitandao ya kijamii na simu kuwa Watu wanaenda lakini wanashindwa kupata kutokana na foleni kubwa na wanatakiwa katika majukumu mengine ya kazi, siku ya Jumapili kutakua na Wahudumu mia moja watakaotoa huduma ya chanjo.

Katika hatua nyingine amewaagiza Wakuu wa wilaya zote za Dar es salaam kuweka siku moja ambayo itawaruhusu Watumishi wote na Wananchi kupata chanjo kwa hiari yao kuwezesha Watu wengi kupata chanjo.
Screenshot_20210819-172450_GBInsta.jpg
 
Rais wa Marekani Joe Biden amesema anaweza kurefusha uwepo wa Wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan hata baada ya tarehe 31 Agosti mwaka huu, ambayo ndio muda wa mwisho.

Ameyasema hayo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ABC cha nchini Marekani, akijibu swali la nini kitafanyika ikiwa baada ya tarehe hiyo, watakuwepo raia wa Marekani wanaosalia kwenye ardhi ya Afghanistan.

Inaaminika kuwa hadi sasa wapo Wamarekani wapatao 15,000 nchini Afghanistan, Nchi ambayo iko chini ya udhibiti wa Taliban.

Biden amekataa ukosoaji dhidi ya utawala wake, kwamba haukufanya vya kutosha kuepusha mtafaruku na ghasia vilivyoambatana na kuondoka nchini Afghanistan baada ya Wataliban kuukamata mji wa Kabul.
Screenshot_20210819-172754_GBInsta.jpg
 
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania imesema imeanza utekelezaji wa kukusanya kodi ya majengo kwa kutumia mfumo mpya wa ukusanyaji kupitia ununuzi wa umeme, utekelezaji utaanza rasmi August 20,2021 na unafanyika chini ya usimamizi wa TRA kwa kushirikiana na TANESCO ukihusisha mita za aina zote za umeme.

Kwa njia hii mpya ya ukusanyaji wa kodi kila mnunuzi wa umeme atakatwa Tsh.1000 kwa Mwezi kwa nyumba ya kawaida na Tsh. 5000 kwa Mwezi kwa sakafu ya ghorofa, kwa wanaotumia mita za ankara watalipia kodi hii kwa pamoja katika ankara ya mwezi.View attachment 1898313
Screenshot_20210819-173032_GBInsta.jpg
 
Shirika la afya Duniani WHO limetoa msaada wa baiskeli 100 mkoani Kigoma kwa ajili ya Wahudumu wa afya ngazi ya jamii waliopo katika maeneo ya mipakani na katika kambi za Wakimbizi ili kuimarisha ufuatilia wa magonjwa ya mlipuko.

Akikabidhi baiskeli hizo kwa Mganga mkuu mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi million 27.7 kupitia mradi wa pamoja wa Kigoma Dkt Jailos Hiriza kutoka ofisi ya WHO Kigoma amesema baiskeli hizo zitakwenda katika Wilaya zote nane ili kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

Amesema wamelenga kupeleka baiskeli hizo katika maeneo ya mipakani pamoja na kambi za Wakimbizi kutokana na umuhimu wa maeneo hayo ambayo yamekuwa ni rahisi kupenyeza magonjwa ya mlipuko na kusambaa katika jamii.

Sekta ya afya Kigoma inakiri uwepo wa baiskeli hizo utasaidia Wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa kuwasadia kufika maeneo ya mbali ambayo yalikuwa ni changamoto katika kufikisha elimu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Covid 19 na mingineyo ambayo yamezikumba baadhi ya nchi zinazopakana na mkoa wa Kigoma.
Screenshot_20210819-173247_GBInsta.jpg
 
Watu 10 wamefariki dunia na nane kujeruhiwa baada ya gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kugongana uso kwa uso na gari la mizigo katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Ilalwe kata ya Bukombe wilayani Bukombe na kuhusisha gari la jeshi lililobeba ndugu waliotoka kwenye msiba wilaya ya Kahama likigongana na gari ya mizigo.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe, Said Nkumba amesema majeruhi Sita walihamishiwa katika hospitali ya Ushirombo na wawili wapo kituo cha afya Masumbwe na miongoni mwa marehemu yupo Mwanajeshi mmoja.

Miili ya waliopoteza maisha imehifadhiwa hospitali ya Masumbwe na chanzo cha ajali bado hakijafahamika na jeshi la polisi linandelea na uchunguzi kwenye eneo la tukio.
Screenshot_20210819-173452_GBInsta.jpg
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa anamiliki silaha aina ya Glock-17 kwa ajili ya kujilinda kutokana na kutishiwa kuuawa.

Akihojiwa na wakili wa Serikali mkuu, Tumaini Kweka leo Alhamisi Agosti 19, 2021 mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Odira Amworo, Sabaya amesema silaha hiyo alianza kuimiliki Machi 24, 2021.
Screenshot_20210819-173742_GBInsta.jpg
 
Watawala wasianzishe chokochoko ambazo zinaondoa utulivu, wasianzishe vita na makanisa, mara kuingilia Uhuru wa kuabudu mara utasikia watu wanakamatwa kanisani,hii sio sawa" Anthony Lusekelo

"Tuna shida ya kisiasa hapa Tanzania, vuguvugu la kisiasa limeanza, tuna shida ya Corona na Tozo, tusijitwishe mzigo mwingine. Uhusiano uliopo kati ya Serikali na taasisi za dini udumishwe udumishwe kwenye kasoro tututumie taratibu kusuluhisha" Anthony Lusekelo
Screenshot_20210819-174056_GBInsta.jpg
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.

Hayo yameeleza na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa kutofautisha mnunuzi wa umeme kama ni mwenye nyumba au mpangaji, hivyo kwa mwanzoni mpangaji anaweza kukatwa kodi hiyo kimakosa.

“Hiyo kodi inapaswa kulipwa na mwenye jengo lakini kwa mwanzo kumekuwepo na changamoto ya kujua ni yupi mwenye jengo ni yupi mpangaji kwa hiyo mwanzoni [mpangaji] unaweza ukapata ‘bill’… mwenye jengo afike ofisini aseme nyumba zangu ni moja, mbili, tatu, ili wenye zile mita ziondolewe,” amesema Lucas.

Lucas ameongeza kuwa mwenye jengo anaweza kulipia kodi ya nyumba za wapangaji taslimu shilingi 12,000 kwa kila nyumba ya kawaida kwa mwaka na namba za mita za wapangaji zitaondolewa kwenye mfumo, au kodi hiyo itahamishiwa kwenye mita yake.

Aidha, TRA imesema kuwa endapo mwenye jengo hatowasilisha taarifa za wapangaji TRA, wapangaji wanaweza kupeleka malalamiko yao kwamba wanatozwa kodi ya jengo kimakosa.

Viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja kutoka shilingi 10,000 iliyokuwa ikitozwa awali, na shilingi 6,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka 5,000. Hata hivyo kwa upande wa halmashauri za wilaya na miji midogo nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa shilingi 6,000.

Kwa utaratibu huo kila mnunuzi wa umeme atakatwa shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hiyo kwa pamoja katika Ankara zao za mwezi.View attachment 1898336
Screenshot_20210819-174341_GBInsta.jpg
 
Shirika la Fedha Duniani (IFM) limetangaza kusitisha misaada kwa Afghanistan kutokana na utawala wa Taliban kutotambuliwa kimataifa. Wafadhili wengine wameonesha nia ya kukata misaada ambayo kwa ujumla ni asilimia 43 ya pato la Taifa la Afghanistan.
Screenshot_20210819-174544_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom