Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Rais Joe Biden wa Marekani amezungumza leo baada ya Wanamgambo wa Taliban kuiweka Nchi mikononi mwao siku chache baada ya Majeshi ya Marekani kuondolewa Nchini humo.
Biden amewajibu wanaosema amekosea kuyaondoa Majeshi ya Marekani Nchini Afghanistan kwa kusema Wanajeshi wa Marekani hawatakiwi na hawatotakiwa kupigania vita na kufa kwenye vita ambayo Wanajeshi wa Afghanistan wenyewe hawajitoi kuipigania Nchi yao.
Ameitoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya Wanajeshi wa Afghanistan kujisalimisha kwa Wanamgambo wa Taliban na kuwarahisishia Wanamgambo kuiweka Nchi mikononi mwao.
Rais Biden pia amesema Wanajeshi wa Afghanistan walipewa mafunzo na Marekani na kila kitu walichohitaji kwenye vifaa vya kijeshi hata jeshi la anga lakini wameshindwa kupambana na Wanamgambo hao ambao hawana Jeshi la anga.