Makapuku Forum

Makapuku Forum

PRINCE DUBE FC PYRAMIDS
.
Kwa mujibu wa Jarida la Kickoff magazine limeripoti kuwa matajiri wa Ligi kuu ya Misri, FC Pyramids wameandaa ofa nono kwa ajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube (24).
.
Klabu hiyo inayomilikiwa na Taikuni Bilionea Salem Al Shamsi, kwa kutambua kwamba Dube bado ana mkataba wa miaka 3 na Azam ameweka mezani dola 800,000 zaidi ya Shilingi bilioni 1.8 ili kumnasa.
.
Dube katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara alihusika katika mabao 19, akifunga 14 na kutoa assists 5 kwenye michezo 22.
Screenshot_20210816-140546_GBInsta.jpg
 
Wakati majonzi yakiendelea kuwakumba Watu wa Haiti kufuatia kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi ambalo limesababisha vifo vya Watu 1,297 jana Jumapili, taarifa mpya kutoka Haiti ni kwamba leo usiku kunatarajiwa kuwa na Kimbunga.

Kimbunga hicho kilichopachikwa jina Grace kinatarajiwa kuipiga Haiti leo usiku, kikizidisha machungu ya wakaazi wa Nchi hiyo maskini.

Majanga haya yametokea wakati Nchi hiyo ikikumbwa na mzozo wa kisiasa kufuatiwa kuuawa kwa Rais wake, Jovenel Moise mwezi uliopita.

Waziri Mkuu Ariel Henry ametangaza hali ya dharura ya mwezi mzima na kuwataka Wahaiti kuonesha mshikamano.
Screenshot_20210816-141529_GBInsta.jpg
 
Idadi ya Watu waliofariki kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Nchini Haiti siku ya Jumamosi imeongezeka na kuzidi 1,200

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.2 katika kipimo cha Richter lililotokea Jumamosi na kuharibu maelfu ya nyumba na miundombinu ambapo Watu wengine 5,700 wamejeruhiwa huku maelfu wengine wakikosa za kujihifadhi.

Msiba huu mkubwa kwa Taifa umetokea ambapo pia Taifa hili linaomboleza kifo cha Rais wao ambae aliuwawa akiwa nyumbani kwake July 2021.
Screenshot_20210816-141718_GBInsta.jpg
 
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafanya kikao cha dharura leo kujadili hali nchini Afghanistan baada ya Wataliban kuuweka mji mkuu wa nchi hiyo, Kabul chini ya usimamizi wao jana.

Kikao hicho cha hadhara ambacho kitafuatiwa na kingine cha faragha vimependekezwa na Estonia pamoja na Norway.

Ofisi ya Katibu Mkuu wa umoja huo, Antonio Guterres imesema Kiongozi huyo anafuatilia yanayotokea Afghanistan na amewahimiza Wataliban na pande zote zinazohusika kuchukua kila tahadhari katika kuyalinda maisha ya Watu na kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya kibinadamu.

Ripoti kutoka Afghanistan zinasema kuwa Wataliban wamechukua udhibiti kamili wa Serikali baada ya aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Ashraf Ghani kuikimbia nchi hapo jana.

Marekani imeondoka katika Ubalozi wake kwenye Mji wa Kabul na kuwahamishia Raia wake katika uwanja wa ndege ambao sasa imeuweka chini ya ulinzi wake, Ujerumani pia imewaondoa Raia wake kutoka Afghanistan.
Screenshot_20210816-142008_GBInsta.jpg
 
Rais Samia leo anatarajia kuondoka Jijini Dodoma kuelekea Nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini kwa Africa (SADC) utakaofanyika kuanzia August 17-18 mwaka huu.

Katika Mkutano huo pamoja na mambo mengine Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC wataithibitisha Nchi ya Malawi kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja (August 2021 - August 2022)
Screenshot_20210816-142135_GBInsta.jpg
 
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amemtaka Rais wa sasa Joe Biden ajiuzulu akimtuhumu kusababisha Wanamgambo wa Taliban kupata nafasi ya kutawala Miji mbalimbali ya Afghanistan ikiwemo Mji Mkuu wa Kabul, hii ikiwa ni baada ya uamuzi wake kuliondoa Jeshi la Marekani nchini humo lililokaa kwa miaka takriban 20.

“Ni wakati umefika sasa kwa Joe Biden kujiuzulu kwa kile alichokisababisha kwa Watu wa Afghanistan na wala haitokuwa jambo kubwa maana hakuteuliwa kihalali tangu mwanzo, Biden ameshindwa pia kuidhibiti Corona, kupambana na masuala ya Uchumi na Wahamiaji” ———Trump

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ameikimbia Nchi yake ya Afghanistan jana baada ya Wanamgambo wa Taliban kuuzingira mji mkuu wa Kabul.
Screenshot_20210816-142251_GBInsta.jpg
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema hakuna malipo yoyote ambayo Mtu anatakiwa kulipa kwenye huduma ya upimaji pale TANESCO wanapokwenda kuchukua vipimo kwa ajili ya kumuunganishia umeme (survey).

TANESCO wamesema iwapo itatokea Mfanyakazi wake yeyote akataka ulipie kuna namba wamezitoa ili Mtu apige haraka bila kuchelewesha muda ambazo ni 0768985100 au 0222194400.

“Endapo utaombwa kulipia hiyo huduma tunaomba kupata taarifa za Mfanyakazi wa TANESCO”
Screenshot_20210816-142413_GBInsta.jpg
 
Tume ya Uchaguzi wa Zambia imemtangaza Kiongozi wa Upinzani, Hakainde Hichilema kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais uliofanyika Alhamisi iliyopita.

Rais aliyekuwepo Edgar Lungu, ametishia kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo, hata kabla ya matokeo rasmi kutangazwa, Wafuasi wa Hakainde Hichilema na Chama chake cha United Party for National Development, UPND walijimwaga katika mitaa ya mji mkuu Lusaka na kushangilia, ilipodhihirika kuwa mgombea wao alikuwa akielekea kwenye ushindi, hii ikiwa mara yake ya sita kujitosa katika kinyang'anyiro cha Urais wa Zambia.

Alfajir ya leo, mbele ya waandishi wa habari na wadau wengine, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia Esau Chilu, baada ya matokeo kutoka majimbo 155 kati ya 156, amemtangaza Hichilema kuwa mshindi.
Screenshot_20210816-142554_GBInsta.jpg
 
Wanajeshi wa Marekani wamepiga risasi hewani katika uwanja wa ndege wa Kabul, baada ya Maelfu ya Raia wa Afghanistan kukusanyika kwenye eneo hilo na kulazimisha kuingia kwenye ndege za Marekani tayari kutoroka Afghanistan baada ya Wanamgambo wa Taliban kudhibiti Miji mingi ya Nchi hiyo.

Ndege hizo za Marekani zimefika nchini humo kwa ajili ya kuwaondoa Maafisa wa Ubalozi wa Marekani na Raia wengine wa Marekani.

Mashuhuda wanadai Watu watano wamefariki kwenye vuta nikuvute hiyo, huku Wanajeshi wa Marekani wakiwa wameimarisha ulinzi wakati wakiwahamisha Watu wao.

Haijajulikana kama Watu hao waliuawa kwa risasi ama mkanyagano baada ya mashuhuda hao kusema mwanajeshi mmoja wa Marekani alifyatua risasi hewani ili kuwazuia abiria waliokuwa wakijaribu kulazimisha kuingia kwenye ndege.
Screenshot_20210816-153138_GBInsta.jpg
 
Beki mwenye uwezo na sifa za kuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC, Israel Mwenda (21) sasa ni rasmi kuwa ni mchezaji wa mabingwa wa nchi

Karibu Mwenda. Wanasimba tunaamini utaitendea haki jezi ya Simba.
Screenshot_20210816-154050_GBInsta.jpg
 
Wakati majonzi yakiendelea kuwakumba Watu wa Haiti kufuatia kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi ambalo limesababisha vifo vya Watu 1,297 jana Jumapili, taarifa mpya kutoka Haiti ni kwamba leo usiku kunatarajiwa kuwa na Kimbunga.

Kimbunga hicho kilichopachikwa jina Grace kinatarajiwa kuipiga Haiti leo usiku, kikizidisha machungu ya wakaazi wa Nchi hiyo maskini.

Majanga haya yametokea wakati Nchi hiyo ikikumbwa na mzozo wa kisiasa kufuatiwa kuuawa kwa Rais wake, Jovenel Moise mwezi uliopita.

Waziri Mkuu Ariel Henry ametangaza hali ya dharura ya mwezi mzima na kuwataka Wahaiti kuonesha mshikamano.View attachment 1894446
Majina ya Grace haya
 
Nchini Afghanistan Raia wameendelea kupata hofu baada ya Wanamgambo wa Taliban kuuzingira Mji Mkuu wa Taifa hilo Kabul.

Mataifa mengi yameanza kuhamisha Raia wao kutokana na hofu, huku Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini humo ACAA ikitangaza kufuta safari za ndege za kibiashara na kusema anga lake litatumiwa na ndege za kijeshi pekee, hadi pale kutakapotolewa tangazo jingine.

Mapema leo ACAA ilitangaza kufunga eneo linalotumiwa na wasafiri wa kiraia kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamid Karzai uliopo mjini Kabul.

Video zilizosambaa zinaonesha abiria waliofurika kiwanjani hapo wakivutana mashati, kila mmoja akitafuta angalau kijinafasi cha kujipitisha ili aingie kwenye ndege ya kijeshi iliyokuwa inawachukua watumishi wa ubalozi wa Marekani mjini Kabuli
Screenshot_20210817-053739_GBInsta.jpg
 
Rais wa Zambia, Edgar Lungu amempongeza Hakainde Hichilema ambaye ametangazwa kuwa Rais Mteule wa Nchi hiyo, awali Rais Lungu alisema atayapinga matokeo hayo.

Kiongozi wa Upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ameshinda uchaguzi wa Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika baada ya kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Mapema leo Hichilema ametangazwa kuwa Rais Mteule na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Zambia, baada ya kupata zaidi ya kura milioni 2.8 huku mpinzani wake Rais Edgar Lungu akipata kura milioni 1.8.

Huu ni mojawapo ya ushindi mkubwa zaidi katika historia ya uchaguzi nchini Zambia, katika chaguzi mbili zilizopita, mwaka 2015 na 2016 Hichilema alishindwa na Lungu kwa kura chache, kwa mujibu wa sheria za Zambia, Lungu anaweza kuyapinga matokeo hayo Mahakamani.
Screenshot_20210817-053903_GBInsta.jpg
 
Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim ametoa siku 4 kwa Ofisi ya TAKUKURU Temeke kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Mkurugenzi wa zamani wa Wilaya hiyo, Lusubilo Mwakabibi na wenzake kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika ujenzi wa barabara ya Kijichi Mwanamtoti yenye urefu wa Kilomita 1.8 ikiwa imejengwa kwa gharama ya Bilioni 5.4.

Waziri Majaliwa ametoa maagizo hayo leo wakati wa ziara yake katika wilaya ya Temeke ambapo amemuagiza Mkuu wa TAKUKURU Temeke kuwatafuta wahusika wote akiwemo Mkurugenzi huyo wa zamani kwa ajili ya kushitakiwa.

"Nawapa siku 4, tarehe 20 deadline watu waende Mahakamani, ita yeyote yule huyu aliyehamishwa hapa arudishwe, huyo Mkurugenzi aliyewekwa pembeni arudishwe na Msimamizi Msaidizi, Edward Haule rudisha wote peleka mahakamani hatuwezi kufanya mchezo hapa hizi fedha za wananchi” ———Majaliwa.
Screenshot_20210817-054016_GBInsta.jpg
 
Mshtakiwa namba moja kwenye kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili Mkuu wa Wilaya wa zamani Lengai Ole Sabaya amesema Polisi, waendesha mashtaka wamedanganywa na shitaka lililopo Mahakamani limetengenezwa kisiasa kwa sababu ya chuki hivyo ameomba Mahakama kumuachia huru.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi Moses Muhuna wakati akijitetea mbele ya Hakimu Mfawidhi Odira Amworo huku akilengwa na machozi amesema shtaka hilo limetengenezwa kutokana na siasa zilizopo kati ya Mkoa wa Arusha na Hai.

Sabaya amesema kwa wiki tatu akiwa Mkuu wa Wilaya Watu walitaka kumuua na hakuna asiyejua kwenye Mamlaka ya Tanzania ambapo akiongea huku akitokwa machozi amesema Mashahidi wameshindwa kuthibitisha kilichotokea na kwamba vitendo vyote vilivyotajwa hajavifanya hivyo Mahakama imuachie huru.
Screenshot_20210817-054158_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom