Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210812-064429_Opera%20Mini.jpg
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Dorothy Gwajima amesema Serikali imepunguza gharama za upimaji wa Ugonjwa wa Covid-19 Kwa Wasafiri kutoka USD 100 hadi USD 50 kwa kipimo Cha RT PCR, huu ukiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia ambaye aliagiza kupitiwa upya kwa gharama za upimaji ili kuwezesha Wasafiri wengi kupata huduma hiyo muhimu.

Dr. Gwajima amesema utekelezaji wa punguzo la gharama za upimaji wa Covid-19 utaanza rasmi August 16, 2021.

“Serikali imeondoa pia gharama za kipimo cha Antigen Rapid Test mipakani isipokuwa viwanja vya ndege ambapo wasafiri watalipia USD 10"———-Waziri Gwajima

“Sababu ya kushusha gharama ya upimaji inatokana na gharama za uendeshaji kutengwa na Serikali ya Tanzania kupitia Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022”———-Waziri Gwajima
Screenshot_20210812-160216_GBInsta.jpg
 
Bunge la Poland limepitisha Sheria ya kuzinyima ruhusa Nchi na Makampuni ya nje kumiliki vyombo vya habari vya nchini humo.

Wapinzani wamesema lengo la sheria hiyo ni kuinyamazisha Televisheni ya TVN inayomilikiwa na Kampuni ya Marekani, Discovery, Serikali ya Poland imeeleza kwamba shabaha ya hatua hiyo ni kuzizuia kampuni za China na Urusi kuvidhibiti vyombo vya habari vya nchini Poland.

Kulingana na sheria hiyo ya utatanishi kampuni na Nchi ambazo hazimo kwenye Umoja wa Ulaya hazitaruhusiwa kudhibiti vyombo vya habari nchini Poland.

Maelfu ya Watu waliandamana kwenye miji kadhaa ya Poland kuipinga sheria hiyo, Marekani pia imeikosoa sheria hiyo, muswada huo unasubiri ridhaa ya Baraza la Seneti ambako upinzani hauna nguvu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amemtaka Rais wa Poland Andrzej Duda asiupitishe mswada huo.
Screenshot_20210812-163956_GBInsta.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili Sylevester Nyegu, Daniel Mbura, hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea kesho Ijumaa Agosti 13, 2021.

Sabaya na wenzake wawili wanatuhumiwa kutenda makosa matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Screenshot_20210812-164302_GBInsta.jpg
 
Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam imetangaza rasmi kuanza kuwashusha abiria wote ambao wataonekana ndani ya vyombo vya usafiri wa umma bila kuvaa barakoa ikiwa katika kupambana na maambukizi ya kasi ya virusi vya Covid-19.

Vyombo vilivyotajwa ni pamoja na daladala, mabasi ya mwendokasi, mabasi yaendayo mikoani, vivuko vya majini ‘pantoni’.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Agosti 12, 2021 katika mdahalo wa kitaifa kuhusu Covid-19 unaoendelea kufanyika hivi sasa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNICC.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amesema zoezi hilo litafanyika kwa kusimamisha vyombo hivyo na kufanya ukaguzi.
Screenshot_20210812-164551_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom