Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210811-045752_GBInsta.jpg
 
Nyota 18 Simba watangulia Morocco
.
Mabingwa mara nne mfululizo Simba wameondoka na msafara wa watu 30 kwenda kuweka kambi nchini Morocco, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara (2021/22).
.
Katika msafara huo wachezaji ni 18, benchi la ufundi likiongozwa na kocha mkuu Didier Gomes, msaidizi wake Seleman Matola,meneja Patrick Lweimamu na viongozi wengine.
Screenshot_20210811-045916_GBInsta.jpg
 
Aucho, Diarra wasepa na Simba
.
Mastaa wa Yanga, Khalid Aucho na Djigui Diarra wamepishana na wachezaji wa Simba ambao walikuwa wanaondoka kwenda nchi Morocco kwa ajili ya kambi msimu mpya.
.
Aucho na Diarra walikuja nchini kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga na leo waliondoka kwenda kwao wakisubili ratiba ya kwenda kambini na wao nchini Morocco.
.
Screenshot_20210811-050028_GBInsta.jpg
 
KAGERE AFAGILIA KAMBI MOROCCO

“Morroco hali yake ni ya mabadiliko baridi joto hivyo imani yangu ni kuwa tutakuwa na hali nzuri ya kujiandaa na kuendeleza changamoto ya ushindani msimu ujao,”
.
“Mazuri ya timu ni kupata mataji na hilo limekamilika kwetu baada ya kutwaa Ligi na Shirikisho ubora wetu umoja na ushirikiano ndio siri ya haya yote msimu ujao utakuwa wa ushindani kutokana na sajili zinazoendelea."
.
- Meddie Kagere.
Screenshot_20210811-050407_GBInsta.jpg
 
Club ya PSG ya Ufaransa imemtambulisha rasmi Lionel Messi (34) kama Mchezaji wake mpya na kusaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi.

Messi ametambulishwa na kupewa jezi namba 30 ambapo hajataka kumvua jezi namba 10 Neymar kwa heshima ya swahiba wake huyo na kuamua kutumia jezi namba 30 aliyoanza kuitumia kwa mara ya kwanza Barcelona.

Mara nyingi Staa mkubwa anapojiunga na timu mpya hupewa namba ya jezi yake pendwa hata kama ina Mtu mwingine na imewahi kutokea kwa wengi kama Samatta na Ozil ndani ya Fenerbahce na hata Juventus alipowasili Ronaldo jezi namba 7 akaichukua kutoka kwa Juan Cuadrado.
Screenshot_20210811-051134_GBInsta.jpg
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Erick Hamis amesema Bandari ya Dar es salaam imevunja rekodi ya kupokea idadi kubwa ya magari (3743) yaliyoletwa kwa meli moja kubwa tangu kuanzishwa kwa Bandari hiyo.

“Meli imekuja na magari 3743 kitu ambacho hakijawahi kutokea ndani ya Meli moja, mara ya mwisho rekodi ambayo tunayo ni magari 2600, rekodi hii sio Dar es salaam tu haijawahi kufikishwa na Bandari yoyote Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, mara nyingine zinakuja Meli zinakwenda zinapakua Bandari nyingine huku zinakuja Meli ndogo lakini hii imetoka moja kwa moja kwenye Bandari za Japan imechukua magari kwenye Bandari tano imekuja imeshusha moja kwa moja DSM” ———Erick
Screenshot_20210811-144337_GBInsta.jpg
Screenshot_20210811-144408_GBInsta.jpg
 
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeratibu zoezi la hiari kwa Wadau wa sekta hizo kupatiwa chanjo ya Covid-19.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli kwamba kwa mazingira ya kazi zao wako katika hatari ya kuambukizwa.

“Shime kwao kujitokeza siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi kwa hiari yao wale waliojiandikisha katika Mabaraza na Idara zao husika”——— Dkt. Abbasi

Abbas amesema kwa wale waliokosa kujiandikisha awali wawe Wasanii au Wanahabari au Wanamichezo wajiandikishe mapema kupitia namba 0654063274 au barua pepe matiko.mniko@basata.go.tz ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Amefafanua kuwa Wasanii walio nje ya Dar es Salaam wataendelea kutumia utaratibu unaoendelea kutangazwa na Wizara ya Afya.
Screenshot_20210811-144609_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Tanga Siriel Mchembe amewaonya Wanaume wanaonyonya maziwa ya Wake zao ambao wapo kwenye kunyonyesha Watoto kuacha tabia hiyo kwasababu wanawafanya Watoto wasipate maziwa ya kutosha.

DC Mchembe ametoa kauli hiyo baada ya Wanawake wanaonyonyesha Wilayani Handeni kumuomba awasaidie kupaza sauti na kukemea Wanaume wao kuacha tabia ya kuwanyonya maziwa kwa madai ya kwamba yanaongeza nguvu za kiume.

Wanawake hao wametoa kauli hiyo kwa Mchembe kwenye maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika katika mji mdogo wa Mkata.

"Niwashauri Wanaume wanaonyonya maziwa ya Wake zao waache, wanatumia chakula cha Watoto na hiyo inasababisha mtoto kupata utapiamlo maana hawapati maziwa ya kutosha, hakikisheni mnashirikiana kwenye malezi haya mambo mengine acheni"——— Mchembe.
Screenshot_20210811-144800_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa wilaya ya Temeke JokateMwegelo ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Temeke katika kituo cha mabasi Mbagala rangi tatu leo Agosti 11.2021 kutoa elimu pamoja na kusimamia utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla juu ya kujikinga na ugonjwa wa covid-19 kwa kuhakikisha uvaaji barakoa na hatua nyingine za kujikinga na ugonjwa huo zinazingatiwa.
Screenshot_20210811-144942_GBInsta.jpg
Screenshot_20210811-145001_GBInsta.jpg
 
Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa na upotoshwaji mkubwa uliyofanywa na gazeti la Uhuru toleo Namba 24084 la leo Jumatano 11 Agosti, 2021, gazeti hili limepotosha sehemu ya mahojiano aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan na BBC.

Katika habari yake kuu limeandika kichwa cha habari “Sina wazo kuwania urais 2025- Samia” Huu ni upotoshwaji mkubwa na kumlisha maneno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan hakusema kabisa maneno hayo, hili ni kosa kubwa linalokwenda kinyume na sera inayoongoza vyombo hivyo, jambo ambalo halitavumiliwa hata kidogo hivyo HATUA KALI za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika katika uandaaji wake.

Gazeti la Uhuru ndiyo “Adam na Hawa” wa magazeti yote hapa nchini, linawajibika kuonesha weledi wa hali ya juu na sio vinginevyo.

Tunawaomba Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na watanzania kwa ujumla kupuuza habari hiyo kwani imeandikwa na watu wenye maslahi yao binafsi.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan fikra na nguvu zake kwa sasa zimejikita katika kuwatumikia watanzania na si vinginevyo” ——— Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Itikadi na Uenezi.
Screenshot_20210811-145155_GBInsta.jpg
Screenshot_20210811-145217_GBInsta.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mabula Joseph Mkazi wa Inyala Halmashauri ya Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya Mzazi mwenzake baada ya kukasirishwa na kauli za Mwanamke huyo kuwa hataki kuendelea na mahusiano .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Urlich Matei amesema tukio hilo la mauji lilitokea Agost 10 Mwaka huu Katika Kata ya Inyala ambapo Mtuhumiwa Mabula Joseph (31)alikuwa na ugomvi yeye na Mzazi mwenzake,Jema Mela (36) unaodhaniwa kuwa ni wivu wa Kimapenzi ambao ulipelekea kutokea kwa mauaji hayo.

“Katika eneo hilo kulikutwa panga moja na kopo lenye mabaki ya sumu aliyojaribu kujiua Mtuhumiwa baada ya kumuua mwenzake ingawa hakufanikiwa kujiua”
Screenshot_20210811-145418_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom