Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Naomba hii Taasisi iendeshwe kwa uwazi na kwa nidhamu ya hali ya juu hatuwezi kutoka kwenye ishu ya nidhamu, la tatu hakuna Mtu mkubwa kuliko Simba, Simba tumeikuta, sisi tutakufa tutaiacha Simba itaendelea, hatuwezi kukubali Mtu kuwa juu ya Simba na hiyo hata Mimi ‘Mo’ sio mkubwa kuliko Simba” ——— Mo Dewji.
Screenshot_20210730-133153_GBInsta.jpg
 
Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuchangia Elimu umefanyika mjini London chini ya uenyeji wa Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza na Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa kushirikiana na Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) ambapo Rais Mstaafu Kikwete ni Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya GPE.

Zaidi ya Dola Bilioni 4 zimeahidiwa kwa ajili ya kuboresha elimu duniani, Tanzania imewakilishwa na Prof. Ndalichako, Waziri wa Elimu wa Tanzania na Simai Mohammed Said, Waziri wa Elimu wa Zanzibar.
Screenshot_20210730-133341_GBInsta.jpg
Screenshot_20210730-133413_GBInsta.jpg
 
Naibu Waziri wa Afya Tanzania Dr. Godwin Mollel amesema mwitikio wa Watanzania kutaka kupata chanjo ya corona ni mkubwa na hadi sasa ni zaidi ya Watanzania milioni moja wamewasilisha maombi ya kuchanjwa.

"Mpaka sasa Wizara ya Afya kwa maombi ya Watu wanaotaka chanjo ni zaidi ya Milioni moja, nafikiri inapelekea meseji kwamba watu wanaoogopa chanjo ni perception ya mtu na mtu"———Naibu Waziri wizara ya Afya, Dr. Godwin Mollel
Screenshot_20210730-133631_GBInsta.jpg
 
"Sisi wizara ya Afya yeyote anayepinga kuhusu chanjo kama Mbunge,Askofu Gwajima kwangu mimi kama mtu wa wizara ya afya namuona kama client wangu ana mambo yake ambayo yanayohusu usalama wake, kwahiyo najiona kwa sehemu yangu natakiwa kufanya kazi zaidi ya kumfundisha, kuelimisha” ———Naibu Waziri wa Afya, Dr. Mollel.

“Kuna mgonjwa anakuja hospitali analetwa na ndugu unamwambia anywe dawa anakataa, huwezi kumwambia kwa ukali yeye ni mjinga na aondoke hapana, ni kuhakikisha napambana naye hadi akubali kwa hiari yake, akipata dawa akipona wengi wanarudi kushukuru ndio kama hawa wanaopinga chanjo”———Dkt. Mollel
Screenshot_20210730-134851_GBInsta.jpg
 
Nawapongeza mashabiki, wanachama na watanzania wanaoipenda Simba kwa mafanikio ya kuchukua ubingwa mara 4 mfululizo, CAF Champions League tumefika robo fainali mara mbili ndani ya miaka mitatu. Simba Queens imeshinda ubingwa wa Ligi ya Wanawake mara mbili mfululizo.

- Mohamed Dewji
Screenshot_20210730-135407_GBInsta.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia kijana aitwae Dickson Mungulu kwa tuhuma za kujiteka na kujiumiza sehemu ya shingo na mguuni kwa makusudi ili aishawishi familia yake wakiwemo Wazazi na Ndugu kumtumia shilingi milioni tatu ambayo aliandika sms ili ionekane Watekaji ndio wanaitaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema baada ya kumuhoji Mtuhumiwa alisema alikuwa anafanya hivyo ili aweze kupata kiasi hicho cha fedha kiweze kumsaidia kwenye madeni yanayomsumbua.

"Polisi ilipokea taarifa kutoka kwa Mtu mmoja ambae jina lake tunalihifadhi akidai Ndugu yake aitwae Dickson mwenye umri wa miaka 26 ametekwa na wamezipata taarifa kupitia sms iliyotumwa kutoka kwenye simu ya Dickson kwamba watume shilingi milioni 3 vinginevyo atauwawa"

"Baada ya kupokea taarifa hizo Polisi walifanya uchunguzi kwa kina na tarehe 28 July majira ya jioni tulifanikiwa kumpata Kijana aliyesadikika kwamba ametekwa eneo la Mworombo Arusha akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ambayo jina tumelihifadhi"

"Dickson aliemaliza shahada ya elimu katika Chuo Kikuu cha Makumira Arusha mwaka 2020 ilibainika alidanganya kwa kujiteka ili apate hiyo pesa ikamsaidie kulipa madeni, Polisi wanaendelea na upelelezi na ukikamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa ajili ya hatua za kisheria, natoa wito kwa Vijana wenye tabia kama iliyooneshwa na Dickson Polisi haitowafumbia macho wote wanaopotosha umma na kutoa taarifa za uzushi kwa jamii"View attachment 1873606


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu amemteua Rogatus Mativila kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akichukua nafasi ya Marehemu Mhandisi Patrick Mfugale.

Kabla ya uteuzi Mativila alikuwa Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).

Rais Samia amemteua pia Prof. Yunus Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)
Screenshot_20210730-140224_GBInsta.jpg
 
Mkutano wa wakuu wa nchi kuchangia elimu umefanyika leo mjini London chini ya uenyeji wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kushirikiana na Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) ambapo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ni Mwenyekiti mteule wa Bodi.

Zaidi ya Dola bilioni 4 zimeahidiwa kwa ajili ya kuboresha elimu duniani.
Screenshot_20210730-141227_GBInsta.jpg
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, Mo Dewji amekutana na Waandishi wa Habari leo Dar es salaam na kuzungumza mambo mbalimbali ambapo pamoja na mambo mengine amekabidhi Bilioni 20.

MO Dewji miaka minne iliyopita (December 3 2017) alishinda zabuni ya uwekezaji wa Simba SC na akakiri kuweka Tsh 20 ili kupata umiliki wa Simba SC 49% (hisa) dhamira hiyo ameitimiza leo kwa kutangaza rasmi kuweka hiyo pesa.

MO Dewji wakati anasubiri mfumo wa mabadiliko kukamilika Simba SC katika kipindi cha miaka minne ametumia Tsh Bilioni 21.3 sawa na Tsh Bilioni 5.3 kwa mwaka hizo ni nje ya Tsh Bilioni 20 za uwekezaji wake.

“Naona kwenye mitandao natukanwa Mo hana pesa hana pesa, sawa hamna shida , ila leo nakabidhi Bilioni 20, FCC ilisema Bilioni 19.6 ila nimesema nikikata Milioni 400 uchambuzi utaanza kwahiyo nimesema potelea mbali iwe Bilioni 20”———Mo Dewji
Screenshot_20210730-151031_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom